Hivi haya makundi ya wahuni ni nani anaye yaendekeza? Hebu jionee uharibifu wa Viti katika uwanja wa Taifa DSM wakati wa mchezo wa Yanga na Simba. Huu uhuni na wahuni wahusika wanapaswa wachukuliwe hatua stahiki. Haiwezekani mali ya Taifa inaharibiwa kiasi hiki, Ikumbukwe kuwa hii tabia si Mara ya kwanza kujitokeza. Hivyo Mamlaka zikishindwa kuchukua hatua stahiki wajue kuwa ipo siku hili litatojea tena.
Hiyo ndiyo maana ya mtu mweusi. Ustaarabu ni zero. Maana sijui wanafikiria kutumia nini, viti vina uhusiano gani na mchezo?? Lakini tatizo jinngine ninaloliona, kwann hivi viti ni rahisi sana kung'olewa? Nafikiri kuna tatizo la ubora pia katika ufungaji.