Uhujumu Uchumi: Idd Simba na wenzake waachiwa huru katika kesi ya kuhujumu shirika la UDA

Uhujumu Uchumi: Idd Simba na wenzake waachiwa huru katika kesi ya kuhujumu shirika la UDA

Mindi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2008
Posts
3,523
Reaction score
4,992
Kesi ya kuhujumu uchumi na kuisababishia UDA hasara ya Sh. bilioni 8.4 dhidi ya waziri wa zamani Iddi Simba na wenzake imefutwa kwa amri ya DPP.

My Take:
Nikiangalia jinsi kesi ilivyokuwa na ukweli kwamba imefutwa na DPP, inasisitiza kile ambacho kimekuwa kikipigiwa kelele: DPP yupo pale kwa maslahi ya makundi fulani na siyo maslahi ya taifa.

=========

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemwachia huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la UDA, Idd Simba na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo kosa la uhujumu uchumi kwa maelezo kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea kuwashitaki.

Mbali na Simba ambaye anatetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam na mwanasiasa mkongwe nchini,wengine ni Mkurugenzi Salum Mwaking’inda, Meneja wa shirika hilo Victor Milanzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group Ltd, Simon Kisena ambao wanatetewa na Romani Masumbuko.

Amri ya kufutiwa kesi hiyo ya uhujumu uchumi Na.3/2013 ilitolewa jana asubuhi na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Ilvin Mugeta muda mfupi baada ya wakili wa serikali Awamu Mbagwa kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya upande wa jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa na kuwa hata hivyo upande wa jamhuri hautaweza kuwasomea tena maelezo hayo ya awali kama ilivyokuwa imepangwa na mahakama kwasababu Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Elizer Feleshi amewasilisha mahakamani hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea kuwashitakiwa washitakiwa wote chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Baada ya wakili huyo wa serikali Mbagwa kutoa hati hiyo , wakili Mugeta alimpatia fursa wakili wa Idd Simba, Alex Mgongolwa azungumzie hati hiyo, Mgongolwa alieleza kuwa upande wa utetezi hawana pingamizi la hati hiyo idi mradi tu upande wa jamhuri usije kuwasumbua tena wateja wao.

Akitoa amri ya mahakama, Hakimu Mugeta alisema kwasababu kesi hiyo ni ya jinai na ilifunguliwa na upande wa jamhuri na upande huo wa jamhuri kupitia DPP-Dk.Feleshi amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao, mahakama yake haina mamlaka ya kupingana na hati hiyo ya DPP hivyo mahakama yake kwa kauli moja inatamka kuwafitia kesi hiyo ya uhujuju uchumi washitakiwa wote hivyo kuanzia jana washitakiwa hao wapo huru.

Hata hivyo wakati hakimu huyo akitoa amri hiyo Kisena hakuwepo mahakamani hapo bila ya kutoa taarifa yoyote na itakumbukwa kuwa Mei 20 mwaka huu, Hakimu Mugeta alitoa hati ya kukamatwa kwa Kisena ili aje aunganishwe kwenye kesi hiyo mpya Na.3/2013 iliyofunguliwa Aprili 30 mwaka huu, ambapo Kisena aliongezwa katika kesi hiyo na kufanya idadi ya washitakiwa kuwa wanne kwani Mei 28 mwaka jana wakati kesi hiyo ilipofunguliwa rasmi washitakiwa walikuwa ni watatu tu yaani Simba, Mwaking’inda na Milanzi.

Mei 20 mwaka huu, kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa lakini ilishindikana kwasababu Kisena hakuwa amefika mahakamani licha ya Aprili 30 mwaka huu, aliunganishwa katika kesi hiyo ya jinai, hali iliyosababisha siku hiyo ya Mei 20 mwaka huu, wakili wa serikali Mbagwa kuiomba hati ya kukamatwa kwa Kisena na mawakili wa utetezi nao kugeuka mbogo na kuungana na upande wa jamhuri kutaka Kisena akamatwe aje aunganishwe na kesi hiyo ili washitakiwa wote kwa pamoja waweze kusomewa maelezo ya awali kwani wanaamini serikali inafahamu Kisena anapoishi na anapofanyia shughuli zake, hoja ambayo ilikubaliwa na hakimu Mugeta ambaye alitoa amri ya kukamatwa kwa Kisena na siku hiyi hakimu Mugeta aliarisha kesi hiyo hadi Juni 4 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Mwandishi wa habari hii ambaye ameifuatilia kesi hii tangu ilipofunguliwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo hapo

Mei 29 mwaka jana hadi jana kesi hiyo imefikia tamati,Juni 4 mwaka huu kesi hiyo ilipokuja kwaajili ya kusomewa maelezo ya awali lakini pia ,washitakiwa hakuweza kusomewa kwasabababu hakimu Mugeta alikuwa nje ya ofisi kikazi, Kisena hakufika mahakamani na kesi hiyo iliarishwa hadi jana ilipokuja kwaajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali na maelezo hayo ya awali hayakuweza kusomewa kwasababu DPP aliwasilisha hati ya kuwafutia kesi washitakiwa hao kwasababu hana haja ya kuendelea kuwashitaki , pia Kisena hakuwa amekamatwa na wanausalama kama amri ya mahakama ilivyokuwa imeelekeza na wala hakuwepo mahakamani hapo.

Akizungumzia uamuzi huo wa DPP-Dk.Feleshi wa kuwafutia kesi wateja wake, nje ya viwanja vya mahakama hiyo, Wakili Mgongolwa alisema anapongeza uamuzi huo wa DPP kwani ni uamuzi mzuri na pia ni matumizi mazuri ya sheria pale tu DPP anapoona hana mashahidi thabiti wa kuja kujenga kesi yake atumie kifungu hicho kufuta kesi kwani DPP kuendelea kuwa na kesi za jinai mahakamani ambazo anaona kabisa hana mashahdi thabiti wa kuwaleta mahakamani kuja kujenga kesi yake ,hayo ndiyo matumuzi mabaya ya sheria kwani pia hali hiyo itaisababishia serikali gharama za kuwaleta mashahidi na kuongeza mrundikano wa mashauri mahakamani.

‘Minampongeza Dk.Feleshi kwa uamuzi wake huu wa kuwafutia wateja wetu kesi hii ambayo ilikuwa ikifuatiliwa na umma wa watanzania wengi…..DPP ametumia sheria vizuri tena kwa maslahi ya taifa hili kwa kuamua kuifuta kesi hii na ninamshauri pia pale DPP anapoona kuna mashauri mengine ambayo hana hajaya kuendelea nayo pia atumie kifungu hicho kuzifuta ‘alisema wakili Mgongolwa.

Aprili 30 mwaka huu, upande wa jamhuri uliifuta kesi ya awali ya matumuzi mabaya ya madaraka iliyokuwa ikimkabili Simba na wenzake wawili na kisha kufungua kesi mpya yenye mashitaka sita yakiwemo mashitaka ya rushwa na uhujumu uchumi na kisha kumuunganisha Kisena katika kesi hiyo ambapo katika kesi ya awali iliyofutwa Kisena alikuwa ni shahidi wa upande wa jamhuri na hivyo kufanya kesi hiyo ya makosa ya rushwa, uhujumu uchumi kuwa na jumla ya washitakiwa wa nne hivi sasa.
Wakili Mwandamizi wa Serikali Oswalid Tibabyekomya akiwasomea upya mashitaka yao katika kesi hiyo mpya Na.3/2013 alidai washitakiwa wanakabiliwa na makosa ya rushwa,uhujumu uchumi,matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh. Bilioni 8.4. Na kwamba Tibabyekomya alieleza kuwa baada ya kuyachambua makosa hayo wamebaini kuwa yanaangukia katika Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ya kesi mpya , shtaka la kwanza la kula njama linawahusu Simba na Milanzi na Kisena.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Septemba 2009 na Januari 2010, jijini Dar es Salaam, kwa pamoja walikula njama za kutenda kosa la vitendo vya rushwa, kinyume cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Kwa mujibu wa hati hiyo ya mashtaka, shtaka la pili la vitendo vya rushwa linamhusu Kisena peke yake, hata hivyo shtaka hilo halikusomwa kutokana na mshtakiwa huyo kutokuwapo mahakamani.

Shtaka la tatu ni la vitendo vya rushwa ambalo linawahusu Simba na Milanzi. Wakili Mbagwa alidai kuwa kati ya Septemba 2009 na Januari 2010, walikubali kupokea Sh. Milioni 320 milioni kutoka kwa Kisena ushawishi wa kuiuzia Simon Group hisa za UDA ambazo zilikuwa bado hazijagawiwa.Katika shtaka la nne ambalo ni la matumizi mabaya ya madaraka, linawahusu Simba , Mwaking’inda na Milanzi.
 
Kesi ya kuhujumu uchumi na kuisababishia UDA hasara ya Sh. bilioni 8.4 dhidi ya waziri wa zamani Iddi Simba na wenzake imefutwa kwa amri ya DPP.

Source: Breaking News kutoka MWANANCHI

My Take:
Nikiangalia jinsi kesi ilivyokuwa na ukweli kwamba imefutwa na DPP, inasisitiza kile ambacho kimekuwa kikipigiwa kelele: DPP yupo pale kwa maslahi ya makundi fulani na siyo maslahi ya taifa.

CC Mzee Mwanakijiji
 
Last edited by a moderator:
Ndo umelijua leo? Huyu kawekwa kwa maslahi ya watu fulani
 
Subiri za akina Mramba na mwenzake Yona nazo zitafutwa tuu au mpaka mwisho watahukumiwa miezi kadhaa kasha watakuwa huru
 
Kesi ya kuhujumu uchumi na kuisababishia UDA hasara ya Sh. bilioni 8.4 dhidi ya waziri wa zamani Iddi Simba na wenzake imefutwa kwa amri ya DPP.

Source: Breaking News kutoka MWANANCHI

My Take:
Nikiangalia jinsi kesi ilivyokuwa na ukweli kwamba imefutwa na DPP, inasisitiza kile ambacho kimekuwa kikipigiwa kelele: DPP yupo pale kwa maslahi ya makundi fulani na siyo maslahi ya taifa.

Mhmmmmmm ndo zao hao
 
Kwanza kosa la Uhujumu Uchumi, huwa halina dhamana, sasa nilishanga hata watu hawakushtuka baada ya hawa watu kupewa dhamana. Watanzania tulipaswa kuichukulia ile Dhamana waliyopewa kama red flag.
I saw this coming
 
idd smba alfungwa kwa hujuma za rdhwan ili smon group wachukue uda hakuwa na kes ya kujbu rz almkomoa kwa sababu idd smba alkuwa anataka uda iendeshwe kwa faida ila rdhwan kuptia smon goup chn ya smon ksena wakamftn idd smba kwa kumbambkzia kesi akiwa ktk kesi wakajiuzia udda chap sasa wameona wamwachie ni sawa na alchofanyiwa lawrence mafuru CeO wa NBC aliyekataa kuipa tenda ya kuendesha kes za nbc kampun ya GRK law Chambers ya rdhwan kwan alsema ni changa na haina wataalam /wanasheria makin rdhwan kupitia bodi ya udhamini ya nbc wakamsmamisha kazi baada ya GRK CHAMBERS(kampun ya rzwan kikwete) kuchukua tenda NBC rdhwan kuptia bod wakamrudsha ila kutokana na ststus na elmu nzur ya mafuru amabaye anauzka kwa kila taasisi kubwa akaresgn akakataa kuendlea na kaz
 
katika watu ambao ni hatari kwa maslai ya watanzania ni huyu eliaza feleshi - dpp..... anakula kiulaini alafu anaumiza watu!!!
 
Ulitegemea aliwatani Idd Simba afungwe,yeye ndo Mwenyekiti wa Wazee wa Dsm!yaani wale ambao JK Huongea nao Diamond Jubilee...
 
Kwanza kosa la Uhujumu Uchumi, huwa halina dhamana, sasa nilishanga hata watu hawakushtuka baada ya hawa watu kupewa dhamana. Watanzania tulipaswa kuichukulia ile Dhamana waliyopewa kama red flag.
I saw this coming
Ukiangalia mazingira ya kufutwa kwake pia utasikia harufu ya chooni kabisaaa. Maana macho na masikio yote sasa hivi yako Arusha. what more perfect time kupitisha uoza bila watu ku-mind sana - hata kama watanzania sio watu wa ku-mind, na wana kumbukumbu fupi? Come to think of it - kwa bajeti mbovu kama ile ilivyokuwa, is it coincidental kwamba kipindi cha kuijaidili CHADEMA ambao ndio huongoza mashambulizi makali kwa Serikali, makamanda wote hawapo bungeni? just wondering...
 
idd smba alfungwa kwa hujuma za rdhwan ili smon group wachukue uda hakuwa na kes ya kujbu rz almkomoa kwa sababu idd smba alkuwa anataka uda iendeshwe kwa faida ila rdhwan kuptia smon goup chn ya smon ksena wakamftn idd smba kwa kumbambkzia kesi akiwa ktk kesi wakajiuzia udda chap sasa wameona wamwachie ni sawa na alchofanyiwa lawrence mafuru CeO wa NBC aliyekataa kuipa tenda ya kuendesha kes za nbc kampun ya GRK law Chambers ya rdhwan kwan alsema ni changa na haina wataalam /wanasheria makin rdhwan kupitia bodi ya udhamini ya nbc wakamsmamisha kazi baada ya GRK CHAMBERS(kampun ya rzwan kikwete) kuchukua tenda NBC rdhwan kuptia bod wakamrudsha ila kutokana na ststus na elmu nzur ya mafuru amabaye anauzka kwa kila taasisi kubwa akaresgn akakataa kuendlea na kaz

Mkuu nimeipenda post yako ila uandishi mkuu haujakaa vyema hivyo vifupisho
 
Kesi ya kuhujumu uchumi na kuisababishia UDA hasara ya Sh. bilioni 8.4 dhidi ya waziri wa zamani Iddi Simba na wenzake imefutwa kwa amri ya DPP.

Source: Breaking News kutoka MWANANCHI

My Take:
Nikiangalia jinsi kesi ilivyokuwa na ukweli kwamba imefutwa na DPP, inasisitiza kile ambacho kimekuwa kikipigiwa kelele: DPP yupo pale kwa maslahi ya makundi fulani na siyo maslahi ya taifa.
Ilifika mahali Wachina waliomba maiti ya Mao ifukuliwe ili waichape viboko! Sidhani kama haitakuja kutokea huku kwetu baada ya huyu wa kwetu kufa huko baadae!
 
Inamaana UDA ndio Ishaenda Hivyooo!

Yani huyu ushahidi si ulikuwa wazi kabisa live hela ya umma ndani ya akaunti yake.
Pia kauza mali za umma bila ruhusa ya mwenye mali(Umma)
 
Kesi ya kuhujumu uchumi na kuisababishia UDA hasara ya Sh. bilioni 8.4 dhidi ya waziri wa zamani Iddi Simba na wenzake imefutwa kwa amri ya DPP.

Source: Breaking News kutoka MWANANCHI

My Take:
Nikiangalia jinsi kesi ilivyokuwa na ukweli kwamba imefutwa na DPP, inasisitiza kile ambacho kimekuwa kikipigiwa kelele: DPP yupo pale kwa maslahi ya makundi fulani na siyo maslahi ya taifa.

Aisee!! Kama ni hivi nimeanza kuamini maneno ya Dr Hosea wa TAKUKURU, aliposema kuwa Serikali imemshika mikono hawezi fanya lolote dhidi ya mafisadi wakubwa. Kweli hii nchi imeoza, mbona ushahidi wa huyu mzee ulikuwa wazi? si ndio huyu alijiamishia mamilioni kwenye account yake toka account ya UDA?
 
​hongera Iddy Simba, watakupelekaje mahakamani wakati wenyewe wanauza Unga na wako Kitalani tuu
 
Kesi ya kuhujumu uchumi na kuisababishia UDA hasara ya Sh. bilioni 8.4 dhidi ya waziri wa zamani Iddi Simba na wenzake imefutwa kwa amri ya DPP.

Source: Breaking News kutoka MWANANCHI

My Take:
Nikiangalia jinsi kesi ilivyokuwa na ukweli kwamba imefutwa na DPP, inasisitiza kile ambacho kimekuwa kikipigiwa kelele: DPP yupo pale kwa maslahi ya makundi fulani na siyo maslahi ya taifa.
Mwenye fedha sio mwenzio!!
 
Halafu the same DPP anamwekea kipingamizi Lwakatare kwa issues za kizushi kama ufisadi anatumia mamlaka visivyo. He is politically operating
 
Back
Top Bottom