joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Sio kweli mengi uliyoyazungumza hapa, sijui nianze na lipi maanake umezungumza mambo mengi mchanganyiko, tuanze na raw materials, Tanzania hatuhitaji kusafirisha raw materials kwenda nje ya nchi, tunachohitaji ni kuwa na viwanda ili tuuze bidhaa zilizosindikwa, kuwauzia Kenya raw materials, sio win win wala sio jambo zuri, mbona wao hawatuuzii raw materials, unadhani hawana?True lakini kumbuka Kikwete alisema ni wakati anahutubia bunge Kenya, kila mtu anamuhitaji mwenzake huwezi kuendelea bila kushirikiana. Kenya ni second big invester kwetu kama sikosei kwa maneno ya JK. Waarabu wanaweka mazingira mazuri kwa investment na land ni sehemu tu. Sisi bila kutengeneza mazingira rafiki na kuongea Direct investment hatuwezi kufika mbali. Na kama wa Kenya wanataka raw materials kwetu hiyo ni good news ni soko why not. Pia tukumbuke Kenya wali survive hata wakati wa ujamaa kwetu na mipaka ilifungwa lakini wakatuzidi so ni win win situation.
Kuhusu kuhitajiana, ni muhimu sana kushirikiana, lakini ni lazima ushirikiano huo uzingatie makubaliano yenye tija kwa nchi zote, sio kulenga upande mmoja tu kwa maslahi yake, na hiyo ndiyo tabia ya nchi ya Kenya, huwa inajali maslahi yake bila kujali nchi zingine hii ni kwa sababu uchumi wa Kenya ni wa kibepari, kwa mfano nchi za EAC zilikubaliana kwa pamoja kupiga marufuku nguo za mitumba baada ya kujiridhisha kwamba tunauwezo wa kuzalisha nguo za kutosha humu EAC, Marekani ikasema nchi yoyote itakayopiga marufuku mitumba itaondolewa ktk mpango wa AGOA, Kenya bila kushauriana na wenzake haraka ikavunja ule mkataba wa kupiga marufuku mitumba, sasa hivi Kenya ni nchi pekee iliyojitoa kwa kuigopa Marekani, sasa hiyo ni nchi ya kuitegemea?.
Kuhusu Ujamaa kwamba walituzidi, wewe ndugu yangu ndiyo hujui kabisa uchumi unavyokwenda. Sisi tulivyopata uhuru hatukuamua kujenga uchumi moja kwa moja kama Kenya, tulianza na kujenga msingi imara wa nchi, ili iweze kuhimili uchumi endelevu na wenye nguvu, tulishughulikia umoja wa kitaifa ili tupate amani ya kudumu, tukaondoa ukabila, tukakataza watu kujichukulia ardhi kiholela, tukaondoa tabaka la matajiri na masikini. Baada ya kukamilisha hayo ndiyo tukaanza kujenga uchumi, wewe mwenyewe ni shahidi jinsi uchumi wetu unavyopanda steady ans surely. Kenya wao walianza kujenga uchumi bila kujenga misingi imara, mwanzoni walifanya vizuri, ila sasa unaona kinachotokea?, uchumi ulijengwa juu ya msingi wa mchanga sio mawe sasa umeanza kuporomoka