Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Toka uanze mjadala wa DP world, umekuwa na makosa mengi ya kiuandishi.

Mfano Uzi huu una makosa zaidi ya 10, na wewe ilikuwa kinara wa kuwarekebisha watu wanaokosea.

Kuhusu DP world sina cha kuongeza wala kuongeza, mtavyokubaliana ndio hivyo hivyo
Amezeeka. Anaandika huku anatetemeka/anatetema.Apewe ugoro wake.
 
Hilo ni sawa kabisa, lakini si linatakiwa lijadiliwe kiamani, kila mwenye hoja aiseme hoja yake bila jazba wala uchochezi au kuomesha chuki kwa wengine?

Au wewe unaridhika na lugha za uchokozi (provoking) zinazowachiwa kutumika hivi sasa?
Lugha sio nzuri..Ila pia tofauti ya kauli zinazotolewa ndio zinaharibu. Kila mtu amekuwa ni msemaji, Kila mtu mpaka wanapishana kauli.
 
Sipati picha kama ungekuwa mod jf ingekuwaje maana hayo unayoita 'maafa' mods wenyewe hawajayaona na ndio maana hawafuti nyuzi hizo.

Nijuavyo mie mods hufuta nyuzi zote zenye kuleta maafa muda mfupi tu baada ya kusambazwa
Mimi nikiwa moderator, kwanza watu hawatokula ban, ntakuwa nabadili lugha tu, nafuta post za matusi na zenye uchochezi wa kijinga, ikiwa mtu hasikii baada ya kumuonya matra tatu, hapo ndipo ban itafatia.

Mbona hata mimi nimeshapigwa ban sana JF mpaka nikaitwa JF ban #!. Mimi nishafungiwa maisha kuchangia JGF akaja kuniombea Obama alivyokuja Tanzania. Kumbe alikuwa ananisoma kabla hajaja Tanzania.
 
Unaona lugha hiyo, hao "wezi" ni nani na nani na wamekuibia nini?

Duniani wezi kweli wapo lakini unamshutumu mtu bila ushahidi sheria haikuruhusu na unaweza kuchukuliwa hatua. Usifikiri nyuma ya hii mitandao tumejificha kiasi cha tukitakikana hatuwezi kupatikana.
Nenda pale kwenye twitter ya Lisu ameweka ushahidi namna kula zilivyoibiwa pale kawe kwa Halima. Acha ujinga
 
Acheni watu watoe madukuduku yao.

Hofu ya nini kama mnaamini mama yenu anachofanya ni sawa?

Kama mnakubali asifiwe basi pia kubalini asemwe kwa namna yoyote ile.

Mnaumia nini akisemwa?

Kama hamtaki asemwe mwambieni aache kazi arudi Unguja akacheze na wajukuu zake.
 
Haakuna shaka yoyote, kwa sasa hivi tunaona Watanzania wengi, wanaojiita wasomi, wanaojiita mawakili wakitowa maoni yao kwa lugha ambazo ni za kuudhi, kukebehi, kukejeli mapa kutusi...
Aione Dr, wakili msomi, msomi wa Harvard, Rais mstaafu.
 
Sawa kabisa, kila mmoja wetu ana maoni yake, na ni vizuri kwenye maoni tusijumuishe, uweke huyo mwana siasa na alichokifanya ambacho wewe hukioni sawa, ndiyo nguvu ya hoja.

lakini kutukana na kuchochea kwa lugha za maudhi kunajenga au kunabomoa?
Kiukweli huwa nakerwa mno na Aina ya wanasiasa wa hivyo, wanaacha kujenga hoja za kisiasa zenye kulenga maslahi mapana kwa watanzania wote, wamebaki kuleta matabaka kwa wananchi.... Watu wa hivi hawafai kabisa
 
Unaona lugha hiyo, hao "wezi" ni nani na nani na wamekuibia nini?

Duniani wezi kweli wapo lakini unamshutumu mtu bila ushahidi sheria haikuruhusu na unaweza kuchukuliwa hatua. Usifikiri nyuma ya hii mitandao tumejificha kiasi cha tukitakikana hatuwezi kupatikana.
Achana kutisha watu hovyo kisa umekura hongo na waarabu wa Walodi wewe....sio kipindi cha Jiwe hiki.
 
Acheni watu watoe madukuduku yao.

Hofu ya nini kama mnaamini mama yenu anachofanya ni sawa...
Uliona kuna mtu au chombo chochote kimemzuia yoyote kutoa maoni? Lakini kutoa maoni kwa njia ya matusi, kejeli kwa viongozi, dharau hiyo si njia sahihi za kutoa maoni. Kumbuka inapoishia haki yako ya kutoa maoni ndipo inapoanzia haki ya mwingine.
 
Nani katukana?

Na kejeli kwa viongozi si jinai!

Maneno ya dharau si jinai.

Acheni watu waongee.

Kuwaziba watu midomo ni dalili ya kushindwa hoja.

Na unaposhindwa hoja basi unaanza kutumia maguvu tu.
 
Uliona kuna mtu au chombo chochote kimemzuia yoyote kutoa maoni? Lakini kutoa maoni kwa njia ya matusi, kejeli kwa viongozi, dharau hiyo si njia sahihi za kutoa maoni. Kumbuka inapoishia haki yako ya kutoa maoni ndipo inapoanzia haki ya mwingine.
Kama hawataki kejeli basi wasitukejeli watanzania kwa kuingia mikataba mibovu
 
Kwanini hao wanaotukanwa nao wasiende mahakamani kama ambavyo unashauri wanasema nchi imeuzwa waende mahakamani?. Kama Kuna Sheria zinavunjwa shauri waende mahakamani kama ambavyo B Membe alifanya Kwa Musiba nasio ujinga unaoandika hapa.
 
Haakuna shaka yoyote, kwa sasa hivi tunaona Watanzania wengi, wanaojiita wasomi, wanaojiita mawakili wakitowa maoni yao kwa lugha ambazo ni za kuudhi, kukebehi, kukejeli mapa kutusi...
Kama hawataki kukejeliwa au kutusiwa waache kuwakejeli au kuwatusi watanzania kwa kuongoza vibaya kwa mfano kuingia mikataba mibovu.sio wao tu hata machawa wao kama wewe watakejeliwa wenyewe wakiwakejeli watanzania.
 
Dawa hapa ni kuondoa huo mkataba au MOU na kuacha kabisa mawazo hayo. Ni hiyo mikaba mingine 16 ni bora iwekwe wazi hadharani vinginevyo wenye nchi wameshaamka. Bandari ni issue kubwa inaweza kuibua nchi aliyokuwa anaililia Rev Mtikila....TANGANYIKA...Nchi hii ilikuwa tamu sana jamani, mimi nimewahi kuandikia ubao ulioandikwa hapo juu Government of Tanganyika na kwenye kalamu ya risasi na kalamu za nibu na vidau vyake na madaftari. Vifaa vyote hivi tulikuwa tunapewa bure na serikali
 
Asante Sana kwa kuandika jambo Jambo ambalo lilikuwa linaniumiza Sana moyo wangu, Najiuliza kwanini vyombo vya habari vinarusha maudhui pasipo kuyachuja na kuangalia Kama Yana Afya kwa walaji? Kwanini matusi na lugha za dhihaka ,kejeri ,matusi na udhalilishaji kwa Rais wetu na viongozi wa serikali yetu yalihusiwe na kurushwa hewani? Kwanini watu wanatoa matusi na wanaachwa?

Mamlaka husika zipo wapi? Zinasimamia Nini? Zinataka mpaka kitokee Nini ndio ziamke katika usingizini? Mpaka kufanyike Nini ndio watu watimize wajibu wao? Tunatengeneza Taifa la namna gani?

Rwanda watu walichinjana na kuuana kutokana na uchochezi ulio kuwa unaenezwa na vyombo vya habari na baadhi ya viongozi ambao walifumbiwa macho pasipo kukemewa? Tangia lini na wapi na kwa Sheria IPi ya mwaka gani ambapo matusi na udhalilishaji umekuwa Uhuru wa habari?

Kwanini tuache mbegu ya chuki,ubaguzi,udini,ukanda na ujinsia uenezwe na kusambazwa na watu na vyombo vya habari pasipo mamlaka kuchukua hatua?

Kwanini tunataka kulipasua Taifa letu? Kinachofangika siyo Uhuru Wala Demokrasia maana Uhuru au Demokrasia haiwezi ikawa katika kumtukana au kuwatukana watu na kiwavunjia heshima na utu wao. Haya mambo Ni lazima yakome na kukemewa kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom