Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Haakuna shaka yoyote, kwa sasa hivi tunaona Watanzania wengi, wanaojiita wasomi, wanaojiita mawakili wakitowa maoni yao kwa lugha ambazo ni za kuudhi, kukebehi, kukejeli mapa kutusi...
Ukweli siku zote huwa unauma.
 
Haakuna shaka yoyote, kwa sasa hivi tunaona Watanzania wengi, wanaojiita wasomi, wanaojiita mawakili wakitowa maoni yao kwa lugha ambazo ni za kuudhi, kukebehi, kukejeli mapa kutusi.

Haya yanayoendelea si maoni tena bali ni vunjifu wa amani uliokusudiwa. Uhuru wa maoni ni lazima uwe na mipaka.

Mtu anajiita mwanasheria msomi au wakili msomi , mwanasiasa, anasimama kwenye majukwaa ya habari na kurusha matangazo yaliyojaa chuki kuwa nchi inauzwa, au bandari inauzwa, Wazanzibari waniuza nchi. Na cha kushangaza sana waziri wa habari amekaa kimya. Waziri wa sheria amekaa kimya. Waziri wa mambo ya ndani amekaa kimya, waziri wa ulinzi amekaa kimya.

Nashauri, vyombo vya habari vyote vinavyorusha matangazo ya chuki vichukuliwe hatua kali za kisheria. Wale wote wanaosimama majukwaani na kufanya uchokozi wa makusudi wachukuliwe hatua za kisheria.

Mpaka sisi tuliozowea mitandao ya kijamii tunawashangaa moderators wapo kimya, watu wanaporusha matusi na kejeli mpaka kwa Rais na mawaziri wake. Hivi hatuyaoni? Au tunapenda huu uchokozi uendelee mpaka uzae madhara?

Kuuwasha moto ni kwepesi sana, kazi inakuja katika kuuzima.


Mimi nadhani wale wote wanaodai nchi imeuzwa waende mahakamani au kwa wao kupeleka madai au serikali iwaite mahakamani waje kuonesha nchi imeuzwa wapi na kwa lipi zaidi?


Nahisi kuna watu wapo nyuma ya pazia amabao wanadhani labda yataishia kiwepesi wepesi yakiachiwa yaendelee. Sasa hivi tayari chuki za wazi zinajionesha kati ya Wasio EWaisslam na Waislam, wasio Waarabu na Waarabu, Wabara na Wazanzibari. watu wa pwani na wasio wa pwani.


Hivi hayo yote kweli yamesababishwa na makubaliano ya Dubai na Tanzania yaliyopitishwa bungeni au kuna yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo hatuyaelewi?

Tunaionmba serikali ichukuwe hatua za dhati, kila anaerusha au kuongea chuki akajieleze kwa ushahi wa hayo ayasemayo, kama hana ushahidi aseme ukweli ni na nani yupo nyuma yake anaemlipa au kumchochea kufanya hivyo.

Serikali itumie mbinu za kawaida na zisizo za kawaida za kiusalama ili kulinda raia wa nchi hii kujiingiza katika chuki na migogoro isiyo ya lazima. Huu ni mtego wa panya watania waliokuwemo na wasiokuwemo.

Naamini katika uwazi na ukweli na naamini katika uhuru wa maoni na habari, lakini kila uhuru ni lazima uwe na mipaka yake. Naona au Tanzania hatuna mipaka ya kujielezza maoni yetu aukama tunayo ama hatuijuwi au tunaiwachiie makusudi mipaka inavukwa?


Serikali, hususa Waziri wa habari, Nape Nnauye tueleze tupo bado ndani ya mipaka ya sheria au tumekiuka? Kama bado upo ndani ya mipaka ya sheria za uhuru wa maoni, tunaomba shertia zikafanyiwe ukarabati. Ili tuwe nchi yenhe kuheshimu utowaji mapni yetu uwe wa kuheshimiana.

Wewe kama hupendi nilichosema au kufanya mimi nifahamisheni usinitukane.

Moderators wa JF tunaomba majukwa haya siasa na habari mchanganyiko yapewe kipa umbele ili yasiwe ni chimbuko la maafa.
Kila mtu ashinde mechi zake , wewe unavyobwabwaja uongo humu tunakunyamazia basi ndio unajiona una haki kuliko wengine , Vumilia na mawe ya wengine
 
Samia kaingiaje hapa. Inaonyesha huyo ndiye target wala si bandari na kwa bahati nzuri mama wa watu kapiga kimyaaa, mnazidi kuumia. Mnatamani awajibu lakini ndo kwanza anaendelea na yake.
Samia kaingiaje? Yeye ndo kiongozi namba 1 nchini.

Naam, kwa nafasi aliyonayo ni moja kwa moja yeye ndo anakuwa shabaha.

Mamako mzazi hatumjui. Hatuna raghba ya kutaka kumjua. Na hakuna mtu anayemlenga kwa lolote lile.

Samia ni Rais. It comes with the territory.

Can’t handle it? Quit and go home.
 
lazima sheria zitumike. Mbona wakati wa Magufuli ndio ilisainiwa MoU ya kwanza baina ta Dubai na Tanzania na hatukuona yeyote aliyesema chochote?
Kila jambo umekuwa ukim- refer magufuli. Kama wewe (nyie) mnamsema magufuli kwa madudu na sie tutawasema kwa madudu. Kama magufuli alifanya mabaya na nyie mnaiga shauri yenu sisi tutawaambieni ukweli kwamba hapa mnakosea hatutaangalia eti mbona magufuli alifanya.

Kuhusu suala la kufuata sheria muanze nyie. Haiwezekani mtu mmoja nchi hii au kakikundi fulani kafanye yale wanayojisikia kwa manufaa yao tu na sie tubaki tunaangalia. Fuateni sheria, andaeni mikataba na makubaliano kwa manufaa ya wananchi wote sio kwaajili ya manufuaa ya wachache na kutafuta uungwaji mkono na pesa za uchaguzi 2025.

Haikubaliki na haitakubalika.
 
Haakuna shaka yoyote, kwa sasa hivi tunaona Watanzania wengi, wanaojiita wasomi, wanaojiita mawakili wakitowa maoni yao kwa lugha ambazo ni za kuudhi, kukebehi, kukejeli mapa kutusi...
Tangia ule Nauli yangu na kutotokea Uwanjani nikakushusha thamani
 
Back
Top Bottom