Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Serikali itumie mbinu za kawaida na zisizo za kawaida za kiusalama ili kulinda raia wa nchi hii kujiingiza katika chuki na migogoro isiyo ya lazima. Huu ni mtego wa panya watania waliokuwemo na wasiokuwemo.
Mfano wa mbinu zisizo za kawaida ni zipi ?
 
Acha kushabikia maharamia wezi. Kuwa mzalendo wa nchi yako.
 
Bandari za zanzibar hazimo kwa sababu wanasema kila mmoja anasimamia bandari zake

..kila mmoja anasimamia bandari zake kivipi wakati hizi za kwetu zaidi ya 60 zinasimamiwa na Mbarawa, Mzanzibari?

..bandari za Zanzibar sidhani kama zinazidi 5 zinasimamiwa na Wazanzibari.

..bandari za Tanganyika ziko zaidi ya 60 nazo zinasimamiwa na Mzanzibari.

..Jamani HAKI iko wapi?
 
Mbona hata mimi nimeshapigwa ban sana JF mpaka nikaitwa JF ban #!. Mimi nishafungiwa maisha kuchangia JGF akaja kuniombea Obama alivyokuja Tanzania. Kumbe alikuwa ananisoma kabla hajaja Tanzania.
Kumbe connection ilikunusuru?.
 
Sisi jeshi la polisi tunapokea listi ya wale wanaoichafua dp world na kukwamisha nia njema ya rais. Tunakuomba ukiwapata hao wanaoisema dp world au wanaojadili mkataba wetu utuletee majina ili tuchukue hatua za haraka.
 
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, hao wazanzibari ni Watanzania pia.
 
Huyu Faizafox hana tofauti na wale magaidi wanaojilipua ili kuwatekeza watu wa dini tofauti wakidai wanaupigania uislam ilihali wanampigania shetani. Siku zote chuki zake huanzia kwenye utofauti wa imani za kidini.

Wapo waislam wanaoifuata dini yao kwa unyofu bila ubaguzi wala chuki. Hawa akina Faizafox ni uzao wa shetani waliofifisha akili na utashi.
 
Kuna jambo muhimu sana ambalo hukulizingatia kufuatia jambo hili. Lilipowafakia wananchi tu liliibua maswali mengi kwa kipindi kifupi sana. Kama serikali ingechukua hatua stahiki mara moja, jambo hili lisingeelekea mbali na kuharibika namna hii au kwa kiwango hiki. Mpaka leo taifa halijapata maelezo kutoka mamlaka ya juu ya nchi wakati ni jambo zito na linalosababisha mpasuko wa hatari.
 
Sawa lakini kuhusu kuwa sii Mkataba ni Makubaliano hayo yameswema na wenyewe wenye serikali
 
You have said it all.
 
Haki ipo kwa sababu vya Tanganyika nyote ni vyamuungano na huyo Mbara ni waaziri wa wizara ya Muungano
 
Mtu anajiita mwanasheria msomi au wakili msomi , mwanasiasa, anasimama kwenye majukwaa ya habari na kurusha matangazo yaliyojaa chuki kuwa nchi inauzwa, au bandari inauzwa, Wazanzibari waniuza nchi.
Maoni ya mtu hayawezi kuwa chuki isipokuwa kwa mtazamo binafsi.
Ili kumaliza utata wa hilo kuna chombo chenye mamlaka ya kuamua, yaani Mahakama

Wanaotoa maoni wajibiwe kwa hoja, kama nchi haijauzwa ijibiwe kwa hoja n.k.
Nashauri, vyombo vya habari vyote vinavyorusha matangazo ya chuki vichukuliwe hatua kali za kisheria.
Matangazo ya chuki ni yapi? Kusema nchi imeuzwa ni chuki? Mbona kila siku tumesikia wengine wakisema Tanganyika ni mkoloni na hatukuwahi kusikia ni chuki seuse kusema bandari inauzwa.
Kwa defnition yako maoni ya chuki ni yapi!
Wale wote wanaosimama majukwaani na kufanya uchokozi wa makusudi wachukuliwe hatua za kisheria.
Hii imeanza wakati wa Bandari! Kiongozi wa UVCCM alisimama jukwaani na kusema wapinzani wapigwe risasi, tuliona watu kitetea uovu wa watu kuuwawa n.k. hatukukusikia ukisema ni chuki, leo mtu akisema bandari imeuzwa hilo ni chuki!
Mpaka sisi tuliozowea mitandao ya kijamii tunawashangaa moderators wapo kimya, watu wanaporusha matusi na kejeli mpaka kwa Rais na mawaziri wake. Hivi hatuyaoni? Au tunapenda huu uchokozi uendelee mpaka uzae madhara?
Uchochezi upi? Kusema Bandari imeuzwa ni uchochezi huo!
Kuuwasha moto ni kwepesi sana, kazi inakuja katika kuuzima.
Nakubaliana nawe kabisa, lakini huo moto umeuona leo? Mbona moto unawaka kule Zanzibar kwa maneno yenye indhara, mitusi na kashfa kwa muda mrefu tu, leo kusema bandari imeuzwa ndio unaona moto!
Mimi nadhani wale wote wanaodai nchi imeuzwa waende mahakamani au kwa wao kupeleka madai au serikali iwaite mahakamani waje kuonesha nchi imeuzwa wapi na kwa lipi zaidi?
Serikali inapaswa kuwashtaki kwa kanuni moja , '' Jukumu la kuthibitisha tuhuma lipo kwa mlalamikaji'
The onus is on the complainant to prove guilty
Nope! hili la udini na urangi limejengwa kama ngao tu na limekuzwa na hao hao waliolileta.
Kila siku na wewe ukiwemo tunamsema Nyerere kwa ujamaa, si kwa ukatoliki au uzanaki bali kwa Urais wake
Tunamsema Mwinyi kwa kuachia mambo yaende tu si kwa Uislam au Uzanzibar bali kwa urais wake
Tunamsema Mkapa kwa kuuza viwanda, si kwa ukatoliki bali kwa Urais wake
Tunamsema Kikwete kwa udhaifu na kupalilia rushwa, si kwa Uislama wake bali Urais wake
Tunamsema Magufuku kwa ubaguzi wa kikabila na kidini si kwa ukatoliki wake bali kwa Urais
Rais SSH hawezi kuwa tofauti na watangulizi wake, ni Rais kama waliopita na atapata haki yake
Hivi hayo yote kweli yamesababishwa na makubaliano ya Dubai na Tanzania yaliyopitishwa bungeni au kuna yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo hatuyaelewi?
Swali zuri sana, na kwakweli nakubaliana nawe kabisa. Haya tunayoyaona ni matokeo ya duku duku na ilipopatikana nafasi ndipo watu wanatema nyongo.

Rais SSH tangu ameingia madarakani ni kama JPM. Kuna mambo mengi sana yanafanyika nyuma ya pazia, hili limefunua tu . Kuna Nepotism sana na revenge katika mambo ya nchi .

Kwa mfano, kuna uvunjaji mkubwa wa katiba akifumbia macho. Ni yale yale ya Mwinyi
SSH amejisahau kuwa ni Rais wa JMT na kudhani ni Rais wa Zanzibar katika JMT. Kosa kubwa sana
Tunaionmba serikali ichukuwe hatua za dhati, kila anaerusha au kuongea chuki akajieleze kwa ushahi wa hayo ayasemayo, kama hana ushahidi aseme ukweli ni na nani yupo nyuma yake anaemlipa au kumchochea kufanya hivyo.
Hapana, serikali iwapeleke mahakamani kuthibitisha tuhuma! Serikali haiwezi kuwa 'Polisi, mwendesha mashtaka na hakimu' . Kabla ya kwenda mahakamani labda wewe utueleze chuki ni kitu gani katika hili la bandari?
Serikali itumie mbinu za kawaida na zisizo za kawaida za kiusalama ili kulinda raia wa nchi hii kujiingiza katika chuki na migogoro isiyo ya lazima. Huu ni mtego wa panya watania waliokuwemo na wasiokuwemo.
Kuna mgogoro gani watu kujadili rasilimali zao?
Naamini katika uwazi na ukweli na naamini katika uhuru wa maoni na habari, lakini kila uhuru ni lazima uwe na mipaka yake. Naona au Tanzania hatuna mipaka ya kujielezza maoni yetu aukama tunayo ama hatuijuwi au tunaiwachiie makusudi mipaka inavukwa?
Kusema bandari imeuzwa ni kuvuka mipaka. Tatizo hapa ni moja, kwamba, unashauri watu wapigwe marufuku kujadili jambo bila kujua huko ni kuwaondolea uhuru wa kujieleza , maoni n.k.
Kuna sheria zilizotungwa dhidi ya ''chuki' hizo zitumike baada ya kuthibitishwa na mahakama
Moderators wa JF tunaomba majukwa haya siasa na habari mchanganyiko yapewe kipa umbele ili yasiwe ni chimbuko la maafa.
I concur with you


JokaKuu Pascal Mayalla
 


kwanini wasijubu hoja ndiyo uhuru huo. Mipaka pale tu wanaposhidwa hoja?. Hii ni lini Tanzania umesikia CCM yeyote akiambiwa haya maneno wakati kila wakati wanatukana wapinzani! Lini mwana CCM kapelekwa mahakamani kwa kusema mambo ya kizushi kwa upinzani. Wapinzani wameitwa mpaka magaidi mlikuwa wapi wakati huo, wameitwa mabeberu mlikuwa wapi wakati huo mbona wale waliachwa. Sasa mnataka kunyamazisha watu wasomi wenye hoja ya mkataba mbaya!!! Mpinzani gani amewahi kushikwa huko Canada au US Kwa kusema nchi imeuzwa!
 
Ni kweli kabisa
Hii hali imefika sehemu mbaya.
Serikali inatakiwa ichukue hatua ya haraka sana, wasiwafumbie macho hao wachafuzi
 
Ukiona hao uliowataja mawaziri wamekaa kimya ujue kweli nchi imeuzwa na hao mawaziri wameungana na wazalendo wenzao kupinga huo uuzwaji wa maliasili za tanganyika na hawa wanzabibari wala urojo
ukimya una mshindo.

Subiri "counter".



Mzee anakumbuka enzi zake za jeshini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…