Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Yaani hawa jf wanahusika moja kwa moja kutuziba midomo sie tunaosapoti mkataba na kuwaachia huru wanaopinga wakitukana na kumtukana hadi rais, nasema wala siogopi hata kufutiwa umembr hawa ni double standard
 
Yaani tubadili sheria tuishi kikoloni kwenye nchi yetu kwaajili ya kumfaidisha nani?viongozi wafanye mbo yenye maslahi kwa Taifa zima kwakuwa wao siyo wamiliki wa nchi,wao ndiyo wanafanya mambo ya kuudhi halafu hatua achukuliwe anaelalamika Mali yake ina dalili za kupotea?wanaohusika WAJIBU HOJA ZA WANANCHI,hayo mambo mengine yanazaliwa kwa Dhana tu kwakuwa mambo yanaonekana kama hayaendi sawa.
Viongozi waache kiburi,wawajibu wanaotoa hoja/maoni,kwanini iwe kama wanafungwa mdomo wakati wao wanakuwepo kwa muda tu,na wataondoka katika nyadhi zao ila wananchi wanabaki na wadhifa wao katika muda wote wanaokuwa hai,shauri kwa hekima,usiegemee hata kama huenda ni mnufaika.
 
kabla ya DPW haya hayakuwepo, ni kwamba kelele ni kwa sababu watu wana dukuduku na dpw. hawakushirikishwa sawasawa kabla ya kuingia kwenye hili dude la kinyonyaji inalotufunga sisi na watoto wetu na wajukuu zetu mikono, miguu na macho na fikira for over 100 years to come.
 
Hilo ni sawa kabisa, lakini si linatakiwa lijadiliwe kiamani, kila mwenye hoja aiseme hoja yake bila jazba wala uchochezi au kuomesha chuki kwa wengine?

Au wewe unaridhika na lugha za uchokozi (provoking) zinazowachiwa kutumika hivi sasa?
Mkimaliza kuuza vya Tanganyika mkauze na huko Paje
 
Hilo ni sawa kabisa, lakini si linatakiwa lijadiliwe kiamani, kila mwenye hoja aiseme hoja yake bila jazba wala uchochezi au kuomesha chuki kwa wengine?

Au wewe unaridhika na lugha za uchokozi (provoking) zinazowachiwa kutumika hivi sasa?
Hivi karibuni nimesikia vifuatavyo:
1. Katibu wa Idara ya Hamasa wa UVCMM akiwa Geita amesema katika mkutano wa hadhara kuwa watagawana mbavu na vidole vya Mange Kimambi. Amesema wataruka na Mbowe na amemuita mhuni na mlevi. Na amekazia kuwa hamna wa kuwafanya kitu wakifanya yote hayo.
2. Kiongozi wa UWT akiwa jukwaani Njombe amesema kuna watu wanaoishi katika nchi ambazo watu wanaoana jinsia moja halafu wanadiriki kukosoa mkataba wa Bandari. Amesema itabidi wawaangalie maana inawezekana nao ni wale wale.

Sikukusikia ukilalamika pale viongozi wa upinzani wanapotusiwa ( nchini kwetu mtu kuitwa shoga, mlevi, mhuni ni matusi) na kutishiwa kuwa watadhuliwa ( labda kama kuruka nae ina maana nyingine). Kutishia kumuua mtu (ukimnyofoa mbavu atapoteza uhai) hata kama alikukosea vipi ni kosa la jinai. Wote tunajua mara nyingi lugha za Mange Kimambi hazipendezi lakini hiyo haimpi mtu haki ya kumtishia uhai wake. Yote haya Faiza hukuyakemea.

Hauwezi kudai heshima kutoka kwa jirani wakati hauwakemei watoto wako wakimtukana. Wakina Mbowe, Lissu na wengine ni viongozi katika taifa hili na wanastahili hiyo hiyo heshima ambayo mnadai kwa viongozi wa chama chenu. Kufumbia macho matusi, vitisho na maneno ya kichochezi ya makada wenu yanawaondolea moral authority ya kukemea viongozi wenu wakitukanwa. Matusi na vitisho kweli havifai, tunatakiwa tuwakemee wote wanaotukana na kuwatisha wenzao bila kujali ni wa chama gani.

Amandla...
 
Tatizo lako umekaa kiuislamu na uarabu tuu. Umejaa ubaguzi mpaka kwenye unyayo
 
Nape.mwenyewe alimua kujivika ujingakwenye mjadala..wengine wameiga!
Cha ajabu wanaotetea Wizi wa Waarabu Ndio wanaongoza ktk orodha Yao..Imqgine Mpuuzi mmoja naibukana kusema Bandari ni ya Wazaramo!?
 
Mhh ul Mkataba wa Ban@ r
Uhuru wa machawa na kusifia uwe na mipaka kinacho endelea sasa ni ujinga ujinga..
Chawa wana kawaida ya kumganda mtu mchafu!
 
Ukitaka kuheshimiwa, anza kwanza kuheshimu wengine.

Ule mkataba wa bandari na DP, ni dharau na matusi makubwa kwa Watanganyika. Ni kuwafanya Watangamyika mapunguani wasio weza kufanya lolote hata kama wakifanyiwa uovu wa nna gani!

Watawala wanatuona wananchi hatuna akili wala ubinadamu kama walio nao wao. Anayekudharau kiasi hicho, unaweza kumheshimu?
 

Kabisa Mkuu, Huwezi kuheshimiwa kama huheshimu wengine.
Yaani anataka kufuja raslimali ya taifa anaambiwa sio sawa yeye yanajifanya eti anaziba masikio.
Sasa atazibuliwa hayo masikio yake Kwa matusi na kejeli hadi ayafungulie.
Usifikirie yupo anapanuapanua miguu Kwa Amer
 
Siyo uchokozi tu, ni uhaini
 
Bi Kinyogoli ungeanza wewe mwenyewe kwenye nafsi yako, Wewe ndiyo mwanzilishi wa kebehi zote hizo kuwananga watu na madhehebu yao, upwanI, udini nk. Sasa yamekushinda unaanza kukimbilia Kwa refarii, moto mliuwasha wenyewe.
 
Usipaniki!! Huna sababu ya kupaniki!! Wnye sababu ya kupaniki ni wale wanaoona mchana kweupe nchi ikiingizwa kwenye mkataba usioonesha namna ya kutoka, kuna namna ya kuingia tu!! Hata kukiwaka moto mlango wa kutokea haupo, halafu unategemea watu wakae kimya!! Hivi kwa kuwa bandari ni suala la muungano, kama tukisema na bandari zote za Zanzibar ziwamo kwenye huu mkataba huko Zanzibar watafurahia?? Na kwa nini Zanzibar hawajalalamika kuutokuingizwa kwenye huu mkataba kama ni kweli una manufaa?? Naomba ukae kimya wazalendo wanapoipigania nchi yao!! Unataka serikali itumie mbinu za kawaida na zisizo za kawaida za kiusalama, tuambie ni mbinu zipi sio za kawaida? au unamaanisha kuua watu? Tafadhali unyamaze, waache watu wapiganie kulinda rasilimali za nchi yao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…