Uhusiano uliopo kati ya wasukuma na wanyamwezi

Uhusiano uliopo kati ya wasukuma na wanyamwezi

Ukitakaka kuelewa vizuri tafuta mdau akufundishe pande kuu za dunia yaani kaskazini (sukuma), mashariki (kiya), kusini ( dakama) na magharibi (ng'weli). Baada hapo ukasome ramani ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora (zote kabla ya enzi za Kikwete) ukishaelewa fanya kama unakaa katikati ya kanda hii na litazame eneo lote kwa kutamka Sukuma (hawa ndo wasukuma), kiya (unapata wanakiya, wanyantuzu), dakama (wadakama/wanyamwezi), g'weli (bhanang'weli/wasumbwa lakini kwa hawa wasumbwa usisahau kwenda kuwasoma tena "nguni speaking people jinsi walivyotoka Afrika Kusini na kufika Tanzania na jinsi walivyogawanyika baada ya kufika Tanzania ili uelewe wasumbwa/bhanang'weli vizuri katika wilaya ya Bukombe au Kahama ya enzi zile)
NB. Haya makabila yanashea vingi sana katika mambo ya utamaduni na mila. In short they are like two families descending from the same man.
Mkuu KAHAMA ni WA DAKAMA
 
Mkuu KAHAMA ni WA DAKAMA
Unachosema kinaweza kuwa sahihi kwa sababu kuna watu wako maeneo fulani hawajielewi kama ni wasukuma, wadakama, wanyamwezi au ntuzu people hii inatokana na wao kujiita kabila fulani wakati majirani zao wakiwaita na kuwatambua tofauti. Kwa mfano msukuma wa Shinyanga mjini akienda Bariadi ataitwa mdakama/mnyamwezi hali yeye anajiita msukuma. Uyu huyu wa Shinyanga mjini anamwita mwenzake wa kahama mnamweli hali watu wa kahama wakijua mnamweli ni yule wa magharibi ya Kahama yaani Lunzewe, Ushirombo na viunga vyake.
Hii inatokana na pande kuu za dunia kama nilivyosema awali na "magharibi yako wewe ina magharibi yake pia" hivyo aliye magharibi yako utamwita mnamweli wakati huyu unayemwita mnamweli anakataa kwa sababu yeye anachojua mnamweli ni yule aliye magharibi yake zaidi.
Wasukuma raha jamani a nice tribe itz. kuanzia Mwanza, Shinyanga, Tabora, Geita, na hata kwa wajukuu zetu akina mbwane, mihanyanyi ni uroda mtupu.
 
Mkuu kifupi kabila la wanyamwezi ni watu waliotoka magharibi mwa afrika,Niger-Congo,kabila mama ni Wanyamwezi,wasukuma ni tabaka lilikotoka kwenye kabila kubwa la wanyamwezi.Katika kabila kubwa la wanyamwezi kuna mashina(makabila matano) yametoka humo,na yanafanana kitabia,asili,lugha,desturi nk....................So take care
Mkuu, nimetafakari sana na kukubaliana nawe kwa asilimia 98, hizo 2 mpaka unithibitishie kama hivi sasa nikienda Niger nitawakuta Wanyamwezi? Nawasilisha makabila ya nchi hiyo kama ifuatavo "PEOPLE: Approximately 80% of the population are comprised of various Black African tribes which include the Hausa, Songhai, Djerma, Fulani, Beriberi-Manga and Tuareg. Ethnic aliens include minorities of Europeans, mainly French descendants."
 
Wasukuma linatokana na SUKUMA au fukuza. Hawa walifukuzwa toka Tabora na kuanza kutafuta pahala pa kuishi na ndoo maana ni waharibifu wa mazingira.

Bora ungekaa kimya tu.

You know something next to nothing.

Sukuma ni North(Kaskazini),Wasukuma tafsiri yake ni Northerners(wa Kaskazini)

Kwa taarifa yako kuna branch ya kabila hili wanaitwa WADAKAMA yaani Southerners kutokana na DAKAMA ambayo Ni South.

Kwa maelezo hayo kuna uwezekano kumewahi kuwepo kabila X ambalo lilitawanyika katika pande nne za dunia.

Walioelekea North waliitwa Northerners(Wasukuma)

Walioelekea South ni Southerners (Wadakama)

Walioelekea East ni Wanyantuzu.

Walioelekea Magharibi ni Wasumbwa etc

So ulichoandika ni maneno ya kijiweni tu.
 
Nakushauri uisome mada hii kuanzia mwanzo. Na tatizo kubwa tulilonalo ni serikali kupiga marufuku kufundisha lugha zetu za ASILI. Hii tumelishwa sumu na wenzetu ambao wanatulisha vya kwao tuvione vya thamani.
 
Wanyamwezi na Wasukuma kwa asili wote wakalimu tofauti ni pale Mnyamwezi wa mjini alipoambukizwa tabia za mwaarabu ambazo ni utamaduni wa nchi nyingine.Lakini Mnyamwezi wa Kijijini na Msukuma hakuna anayesubiri kukaribisha msosi ukifika wewe unanawa na kula tu.
Kwa asili wote wawili Chakula nikitu cha kawaida kinaliwa hadharani wapita njia wanakaribishwa. Tofauti zimesababiswa na mwingiliano zaidi na jamii nyingine mfano Tabora wasukuma ni wengi sana ila wanaishi ndanindani sana na wengi nikama Masai kwa mavazi na niwafugaji.
Mnyamwezi alikuwa mpiga kazi sana ila mwarabu alimwambukiza kunata hata bibi yangu hawezi kula ugali uliosongwa kwa unga huu wa Azam kwamba ni mchafu.Akisonga ugali wake unaweza fikiri hukunawa na kurudi tena kunawa maana nimweupe yaani ukigusa tu alama.
 
Naona wachangiaji pamoja na wengine kuwa Wasukuma/Wanyamwezi bado hawaijui historia. Kwa kifupi asili ya Wasukuma ni Abyssinia (Ethiopia ya leo) na sio Afrika magharibi wala Congo.
Walitokea Ethiopia kupitia Sudan ya leo, Bahima (Uganda) mpaka sehemu za Ziwa Victoria.
Alafu kuna mdau kama ana chuki na Wanyantuzu alafu hajatoa sababu za kueleweka kwanini anasema sio Wasukuma
 
Mkuu, nimetafakari sana na kukubaliana nawe kwa asilimia 98, hizo 2 mpaka unithibitishie kama hivi sasa nikienda Niger nitawakuta Wanyamwezi? Nawasilisha makabila ya nchi hiyo kama ifuatavo "PEOPLE: Approximately 80% of the population are comprised of various Black African tribes which include the Hausa, Songhai, Djerma, Fulani, Beriberi-Manga and Tuareg. Ethnic aliens include minorities of Europeans, mainly French descendants."
Sio lazima uwakute kwa jina hilohilo la wanyamwezi,kwasababu hilo jina walipewa na watu wa pwani,wakimaanisha watu wanaokuja kutoka magharibi kunakotoka mwezi.Mbona wazulu wapo hapa bongo kwa jina la wangoni?
 
Me huwa nauliza kwa nini mataifa ya maghalibi yanaitwa unyamwezini mfano tukimuona akon pamoja na kumtambua asili yake ni senegal ila tunamuita mnyamwezi nini chanzo haswa
Wanyamwezi na Wasukuma sote ni jamii uliyotoka katika "The Congo-Niger Delta" ambayo inaambaa kuanzia Kongo Kinshasa hadi Afrika Magharibi huko Niger; Senegal ni jirani na Niger Delta huko Afrika Magharibi ndo maana ya uhusiano uliopo.
 
Naona wachangiaji pamoja na wengine kuwa Wasukuma/Wanyamwezi bado hawaijui historia. Kwa kifupi asili ya Wasukuma ni Abyssinia (Ethiopia ya leo) na sio Afrika magharibi wala Congo.
Walitokea Ethiopia kupitia Sudan ya leo, Bahima (Uganda) mpaka sehemu za Ziwa Victoria.
Alafu kuna mdau kama ana chuki na Wanyantuzu alafu hajatoa sababu za kueleweka kwanini anasema sio Wasukuma
Wasukuma ni jamii ya wa wabantu toka Afrika magharibi na si pande za Ethiopia mkuu. Wasukuma hawana uhusiano na mhabeshi hata kidogo uwe wa kimamshi ya maneno au tamaduni ila wabantu.
Leo hii msukuma hatapata shida kujifunza Kilingala, Kikasai, na makabila ya yaliyoko kwenye Congo-Niger Delta kwa sababu ndiko asili yake.
Hao unaowata Abyssinia uhusiano hamna japokuwa ni kweli kuna watu waliohama toka Afrika Magharibi na Kati na kuingia Sudan na Ethiopia na kisha kuja Kenya, Uganda na Tanzania lakini jamii yao kubwa ndo wale wanaoitwa masai, wakurya, na makabila mengi ya Arusha asili yao ikiwa si ubantu.
 
Wanyamwezi na Wasukuma kwa asili wote wakalimu tofauti ni pale Mnyamwezi wa mjini alipoambukizwa tabia za mwaarabu ambazo ni utamaduni wa nchi nyingine.Lakini Mnyamwezi wa Kijijini na Msukuma hakuna anayesubiri kukaribisha msosi ukifika wewe unanawa na kula tu.
Kwa asili wote wawili Chakula nikitu cha kawaida kinaliwa hadharani wapita njia wanakaribishwa. Tofauti zimesababiswa na mwingiliano zaidi na jamii nyingine mfano Tabora wasukuma ni wengi sana ila wanaishi ndanindani sana na wengi nikama Masai kwa mavazi na niwafugaji.
Mnyamwezi alikuwa mpiga kazi sana ila mwarabu alimwambukiza kunata hata bibi yangu hawezi kula ugali uliosongwa kwa unga huu wa Azam kwamba ni mchafu.Akisonga ugali wake unaweza fikiri hukunawa na kurudi tena kunawa maana nimweupe yaani ukigusa tu alama.
Yaah, ugali wetu huliwa nje ili wapita njia nao wale na fahari yetu ni pale mpita njia anapokula na kushiba then akiaga atembee hatua chache tu na kuomba pooo ili akachimbe dawa katika kichaka jirani.
Akichimba dawa hatua chache tu baada ya kutoka katika familia hiyo hapo magufuli wa familia anacheka sasa na kuwaambia vijana wake, "ameshiba kweli kweli huyooo anaingia kunya kichakani" na hii ndo furaha kwa familia hiyo. NB hii ni kwa zamani sana ila ndo why jamaa wanaonekana wakarimu sana leo.
 
Hizo za ukarimu ni RECORD za wapi wana Jamvi? Mimi nimekaa huko kwao karibia kote kwa muda mrefu zaidi ya miaka 13 nataka niwaambie Record ya ukarimu mnayosema ni uongo labda nanyi ni wasukuma lkn Wasukuma wanaroho nzuri wakiwa nje ya Ardhi yao yaani wakiwa ugenini lkn wakiwa kwao wanaroho mbaya na kimsingi hawafai kuigwa.
NB. Nimeishi mwanza kisesa,misungwi,bariadi maswa na Tabora Mjini ndiko niliko soma O level.
Kwa ufupi ni wanafiki.
 
Wasukuma ni jamii ya wa wabantu toka Afrika magharibi na si pande za Ethiopia mkuu. Wasukuma hawana uhusiano na mhabeshi hata kidogo uwe wa kimamshi ya maneno au tamaduni ila wabantu.
Leo hii msukuma hatapata shida kujifunza Kilingala, Kikasai, na makabila ya yaliyoko kwenye Congo-Niger Delta kwa sababu ndiko asili yake.
Hao unaowata Abyssinia uhusiano hamna japokuwa ni kweli kuna watu waliohama toka Afrika Magharibi na Kati na kuingia Sudan na Ethiopia na kisha kuja Kenya, Uganda na Tanzania lakini jamii yao kubwa ndo wale wanaoitwa masai, wakurya, na makabila mengi ya Arusha asili yao ikiwa si ubantu.
Hivi ulishawai kwnda Sukuma Museum, Bujora - Mwanza? maana naona unabisha tu
 
Hivi ulishawai kwnda Sukuma Museum, Bujora - Mwanza? maana naona unabisha tu
Acha kukariri stori za wanafiki wachache waliopotosha ukweli. Angalia hata uhusiano wa hizi jamii Bantu, Nubian na wasukuma; nani yukokaribu zaidi na wasukuma katika lugha za asili-mbantu au mnairoti?
 
Nafikiri watanzania wengi ni wazamiaji,tumetoka nchi mbalimbali kwa sababu mbalimbali...Mfano Waha ni waburundi,Wamanyema ni wakongo,Wahaya ni waganda,Wajaluo ni wakenya,Wachagga ni Wakikuyu wa Kenya,Wamakonde ni wamsumbiji..the list goes on and on...
kwanini isiwe kuwa wakikuyu ndo wametoka kwa wachaga?
 
Back
Top Bottom