Mkuu kifupi kabila la wanyamwezi ni watu waliotoka magharibi mwa afrika,Niger-Congo,kabila mama ni Wanyamwezi,wasukuma ni tabaka lilikotoka kwenye kabila kubwa la wanyamwezi.Katika kabila kubwa la wanyamwezi kuna mashina(makabila matano) yametoka humo,na yanafanana kitabia,asili,lugha,desturi nk.Mashina hayo ni kabila la Wanyamwezi,wakonongo,wakimbu,wasumbwa na wasukuma.Wanyamwezi walipotoka magharibi mwa afrika waliweka makazi Tabora kabla ya kuanza kusambaa kuelekea kaskazini magharibi(ukanda wa ziwa).Hivyo mpaka sasa Tanzania kabila linaloongoza kuwa na watu wengi ni Wasukuma,wakifuatiwa na kabila la pili kwa ukubwa ni wanyamwezi.Makabila haya kwa kifupi yanaongoza kwa kuchapa kazi na ukarimu..ndio maana toka Enzi wanasema 'mzigo mzito mpe mnyamwezi',na hata marekani(ambayo inasifika kwa watu wake ukarimu wa kusaidia watu wengine inaitwa 'unyamwezini',hela yao ya dola inaitwa 'mnyamwezi', au mtu akiwa anamzungumzia rafiki yake wa ukweli utasikia akisema 'mnyamwezi wangu'. Lakini pia ndio makabila yanaongoza kwa ushujaa na mapambano,ndio maana machifu wao ni maarufu zaidi kuliko wa makabila mengine kama chifu mirambo na jeshi lake la wavuta bangi 'maarufu kama warugaruga',chifu Isike,chifu Mihayo,chifu Fundikira nk. Makabila haya yanasifika kwa kilimo na ufugaji,pia kwa ukarimu wa hali ya juu hususani wasukuma.Hakuna kabila wakarimu kama wasukuma,labda ndio maana Mungu nae amewazidishia katika ardhi yao kuna kila aina ya neema,chakula cha kutosha,masamaki,madhahabu,mapamba,mang'ombe,maasali,mahela... nk. Ila pia hawako nyuma kwenye uchawi na mizimu hasa kama umewaonea au umewaibia.Inawezekana ni mauchawi waliyotoka nayo huko afrika magharibi na njiani walipopitia congo kuingia Tanzania.So take care