Uhusiano wa CHADEMA, Tundu Lissu na Ubelgiji: Kwanini Tundu Lissu alikimbia ubalozi wa Ujerumani?

Uhusiano wa CHADEMA, Tundu Lissu na Ubelgiji: Kwanini Tundu Lissu alikimbia ubalozi wa Ujerumani?

We ni msomi, lakini mpiga filimbi wa hemelini. Topic ndefu, summary ya material content it is hardly a paragraph. Umepamba waanzilishi na wasababishaji wa matatizo ya waafrica, si Wazungu, ni viongozi wabinafsi wa Africa. Wanasimama majukwaani kusema yasiyo mioyoni mwao.
 
Kwamba rais akiwa magufuli atawafanya hao unaowaita mabeberu kutoweza kuchuma hizo rasilimali zako??.

Kwa taarifa yako there's nothing to take in Tanzania,kama kipo wakiamua hata angekuwepo nyerere sasa hv wangechukua na hamna cha kufanya.
Mmh kwa mwenendo huu ndio mlitegemea CHADEMA tuwape nchi kweli, watu mnaojikomba kwa Wazungu kiasi hiki, watu msiokuwa na uzalendo kwa nchi yenu. Kwa maana hiyo Mzungu angetaka Rasilimali yoyote chini ya utawala wenu mgemgawia bila shida yeyote. Wapuuzi nyie mlitaka kuturudisha kwenye ukoloni wa Wazungu.
 
Nimekuja kukwimbia tuu shati lako limenifanya nisisome uzi wako.
 
Mmh kwa mwenendo huu ndo mlitegemea Chadema tuwape nchi kweli, watu mnaojikomba kwa wazungu kiasi hiki, watu msiokuwa na uzalendo kwa nchi yenu. Kwa maana hiyo mzungu angetaka rasimali yoyote chini ya utawala wenu mgemgawia bila shida yeyote. Wapuuzi nyie mlitaka kuturudisha kwenye ukoloni wa wazungu.
Hakuna anakubali kutawaliwa, binadamu amezaliwa huru. Inaumiza zaidi mkoloni anapokuwa ni mtu ulie mpa dhamana ya kuongoza akakugeuka.
 
Ila UNGEJIKITA kuifafanua na kuielezea Ilani ya chama cha mapinduzi USINGEONEKANA MPUMBAVU.
Na watu kama nyie Ili UPUMBAVU UTOKE SHARTI MPIGWE NA RADI.

Nina waswasi na Masters yako kiingereza chako NI KIBOVU MNO.
NI NGUMU KUPATA UTEUZI.
 
Tanzania is Next level linapokuja suala la hujuma na uchokonozi wa amani yake. Tuache kutumika kama vibaraka bila kujitambua, ninachokiona vijana wengi tusio na kipato au kazi tumekuwa na husuda saaaana na wale wenye nacho.

Kwa akili yetu fupi tunadhani akija kiongozi mpya tulioko nje ndio tutaingia ndani na kutusua!
Tupambane kujikwamua kiuchumi Vijana, hizi blaaaa blaaa za Kisiasa ni Nonsense.

Tutumie vizuri fursa zetu bado nafasi nyingi sana za Uzalishaji Tanzania ziko wazi, Vijana mnang'ang'ania kukaa Sinza, Kino, Tabata nk wakati maisha yenyewe ya Udalali wa kuungaunga na ubishoo, hatimaye unajiingiza kwenye Wizi, Utapeli au Ushoga. Njooni Kitunda tufuge kuku asubuhi unaokota mayai na kupeleka Mjini kwa Baiekeli/Benz lako unauza maisha yanasonga.

Kukaaa na kuanza kumjadili Mwanaume mwenzako Ombaomba/Mkimbizi aliyeko Ng'ambo akitafuta kwa mbinu za Umatonya ni Upuuzi.

Tufanyekazi, tuache porojo huu ni Msimu wa Mvua kama huna Shamba njoo Vikindu nikupe shamba ulime Mihogo.
 
Bima ya Afya kwa kila Mtanzania na Millioni 50 kila kijiji zinaanza kutolewa lini mleta mada?
 
Kwani sasa hivi hayo madini ni ya kwetu? Au kinachokuchanganya ni neno Ubeligiji? Hata hivi tunavyozungumza madini si ya kwetu, labda kodi na mrabaha tunayoambulia kwa asilimia ndogo. Na hata kiongozi wa sasa hawezi kufanya kitu. Na waliogawa madini hayo ni viongozi waandamizi wa CCM si CHADEMA
 
Makampuni ya Ubelgiji yanayofaidi rasilimali za madini ya nchini DRC ni yapi kwa majina?
 
Nadhani huenda huna taarifa za kutosha kuhusu uchimbaji wa madini nchini DRC - Ubelgiji haina makampuni mengi kama unavyosema - kampuni za uchimbaji madini zipo nyingi na zinatoka maeneo mengi ya dunia:-

= Katanga mining - Canada,
= Raid - China
= Mutanda mining - Ubia
 
No wonder wewe ni masikini, akina Bharessa na kina Mo wala hawaoni shida kuweka dhamana magorofa na mashamba yao ili kupata mikopo kwa ajiri ya ku-fund project zao, but masikini wa kipato na akili unadhani kuweka mali yako dhamana bank ni kuiuza au kuigawa.

I am so sorry
 
Mimi ndiyo maana I don't rate Lissu. Ni msaliti mmoja mbaya sana kuwahi kutokea hapa nchini kwetu, yeye na Lissu na Maalim Seif.
 
Umeeandika mengi umepuyanga umeparanga ila hakuna hata point.

Kwa maana hata angekimbilia Ubalozi wa Marekani ungesema au angeenda Ubalozi wa Ufaransa ungesema

Pumba tupu najuta kusoma
 
Bandiko lako nimeiona la kipuuzi,unapodai CHADEMA walitaka kumdhuru Tundu Lissu, serikali ikampa ulinzi? haya mapenzi ya serikali kwa TL yameanza lini? yalikuwa wapi wakati aliposhambuliwa mchana kweupeee, na risasi 18+

Na Kama CHADEMA walikuwa na njama za kumdhuru TL, sasa siingekuwa vzr mkawakamata na ushahidi, na kuwaaibisha mbele ya Umma? mbona huwa mnawafunga kuwapiga kwa sababu za kitoto? harafu itokee opportunity Kama hii kuwakamata CHADEMA wakitenda jinai, msiwakamate?!! haiingii akilini.

CHADEMA haijawahi kutawala nchi hii, CCM mpo tangu uhuru, unawakumbuka net group solution, wanyama hai kuuzwa nje? Wananchi kuzikwa hai nyamongo? Richmond, EPA.

Nenda katafute kipato kwa Elimu yako, sio kusubili uteuzi, hizi njaa zitawaua vijana, vijana siku hizi mnsendekeza njaa sana, siwalaumu kitaa kugumu, lakini hata Kama unatetea chama chako, jaribu kutumia hoja zenye mashiko, sio hizi story za kisingeli, au za kibongofleva,
 
Lissu kila akihutubia kuharibu amani alikua anatumia msemo fulani hivi, mwanzoni sikua namuelewa ila leo mleta mada hii umenifanya nielewe. Alipenda kusema tutafanya hili na lile mpaka "Dunia ituelewe" kumbe dunia yake ni ubelgiji na marekani!! Loh!! huyu baba ana roho mbaya sana, hafai hata kua mtendaji wa kijiji.
Mnahisi mna hati miliki ya nchi hii? Nani alimpiga Lissu risasi?
 
Ina Maana kweli hujui kwa nini Lissu aliikimbia nchi hii. Hii haiitaji elimu hata ya chekechea. Pole.
 
Back
Top Bottom