Uhusiano wangu na baba yangu

Nidhamu ya uoga. Mzazi nae ni mwanadamu so akifanya mambo ya kipumbavu anakuwa ni mpumbavu sababu anafanya upumbavu.

Utakuwa sahihi ukisema sio sawa kushindana na mzazi ambaye amechagua kuwa mpumbavu bali ni vema kumkwepa ili mambo yake yasikuathiri kisaikolojia.

Tukiishi kwa misingi hii hata wewe kesho ukija kuwa na watoto wako utakuwa makini namna unawalea hautawaletea vituko.

Ila tumerithishana mifumo sumu( Toxic Systems) ambayo inafanya watu baadhi kuishi kwa maumivu sana jambo ambalo si sahihi.
 
We mzee unatype kwa kutumia macho na vidole gani khaaaaaah?!
 
Baada ya ule msamaha wa kwanza ulikaa miaka mitano bila kwenda nyumbani kumuona baba yako halafu bado hujui kosa lako, ndio maana mama yako aliachwa na baba yako nadhani naye alikua na akili kama zako

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
LOL!!! BEST COMMENT 😍
 
Ushauri mzuri sana huu....huyu mleta uzi anaangalia alipoangukia badala alipojikwaa....tatizo lilianza alipokataa kwenda polisi na mbaya zaidi akaondoka nyumbani.....hapa ndo alipoharibu na kwa mzazi yeyote hiyo ilikuwa dharau kabisa na ipo wazi hiyo.....dharau ikaendelea alipokaidi kwenda alipomwambia aende kuomba msamaha kwa baba zake wakubwa na shangazi zake.....!!Mi namshauri ajishushe arudi kwa baba ake wakayamalize.... otherwise dunia itamfundisha kama ulivyomsema what's comes around goes around.....yatakuja kumrudia kwa watt zake halafu ndo atajua vzr.
 
Kwani ungeenda kwa dada'ke na kaka'ke na kuzuru kaburi la bibi yako ungepungukiwa nini?

Kwa kufanya kiburi na kukataa hilo ndipo ulipomuumiza muumiza baba'ko, kwa muono wake na makuzi yake, ambayo ni tofauti na yako, umemvunjia hadhi yake kwa ndugu zake.

Vijana mnakuwa na yenu mapya na wazazi wenu walilelewa na mila na desturi zao, hata kama hamkubaliani nazo haina sababu ya kuwafanyia kiburi.

Nashukuru, Kiislam tunafundishwa kutoka kwenye Qur'an kuwa kwa wazazi hatutakiwi hata kuwagunia "mnhh" licha ya kuwajibu na kupingana nao, mradi haitutowi kwenye Uislam wetu.

Rudi, fata aliyokushauri baba'ko "to the dot" . Wachana na kiburi.
 
WEWE ni mjeuri na una kiburi,,ungekua unataka amani na baba Yako pindi amekupa masharti yake sijui ukamuombe msamaaa nana na nani kwanza ndio urudi kwake ungetekeleza...ajabu ww ukampuuza sijui kwann ila inaonekana ni kiburi chako Cha ndani..

Uyo ni baba Ako tu,,unasema una familia subiri na ww ilo toto lako litakuja kukutenga mpaka ukome..kijana acha kiburi na ujuaji Rudi Kwa baba Ako mnynyekeee msikilize na myajenge..na nenda kama mtoto sio kujiona mkubwa mwenzake kisa una kifamilia.
 
Mama yako mzazi una mawasiliano nae? Mahusiano yako na yeye yapoje
 
Umesoma lakini alichokiandika au umetoa tu ushauri boss?
Sijajua ulitaka uone ushauri gani,
1. Kalelewa upande wa baba
2. Waliishi dar
3. Alioomaliza chuo alikua na mishe anachelwa kurudi baba hakupenda hilo
4. Kaamua kuhama na sasa anafamilia
5. Alifiwa na ndugu hawakuja
6. Yeye ako na amani kabisa ila anataka kujua amekosea wapi.

Ulitaka nimwambieje? Kama sio kuyajenga na baba ake kama anaona inafaa?
 
Kama ulichoeleza hapa ni sahihi hakuna kitu ulichoficha basi Mimi binafsi sioni tatzo??

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Sorry to say ila una shida nyingi.

Ulipofanyiwa mpango wa upolisi na baba yako ukaruka mita 1000 na kuondoka nyumbani tatizo lilianzia hapa.
Sijui historia ya nyuma ya maisha yenu ila ni ile aina ya watoto ambao tayari wana black mentality juu ya wamama wa kambo.tayari uliishaona baba hakutakii mema tangu alipoamua kuachana na mama yako.

Angalia ndugu zako wote wanakutenga si kwa sababu wameambiwa na baba yako ila ni ukweli wewe ni kimeo,sema hujui ama hutaki na hauko tayari kujua.

Unasema unaomba msamaha,sijajua ni msamaha wa namna gani,ila inaonekana ni ule msamaha wa shinikizo..

Sikushauri ukomae na utaratibu huo wa maisha,jenga ukaribu na ndugu zako kisha mzee,inawezekana hujakaa sawa kiuchumi ndio sababu kila akikuangalia anapata hasira jinsi ulivyoamua maamuzi ya kimbuzi kwa kutomsikiliza,ungeenda upolisi kisha uendelee na shule huku ukisaidia wengine na yeye pia,badala yake ukawa kijana wa kulala uwani na kurudi saa tano usiku[emoji23][emoji23]
 
Wewe wewe wewe mleta mada narudia tena km BANDOKITITA, Jana nilikuambia na leo nakuambia. Mtoto kwa mzazi hakui, mzazi huwa hakosei(wahenga walisema), na mzazi ni Mungu wako wa 2 baada ya unaemuabudu. Hivi unajua kwa nini baada ya mama yako kuachana na baba yako bado baba yako alihakikisha damu yake haipotei akamwambia mama yako aondoke ila amuachie watoto wake ambao ni nyie. Unadhani km asingekuwa na mapenzi na wewe unafikiri angeshindwa kumwambia wewe uende na mama yako alafu wadogo zako ndiyo abaki nao? Kawalea kwa tabu bila mama yenu mzazi alafu leo unakuja kumlipa ujeuri.

Ngoja nikuulize, km angekuwa ni mama yako kakufanyia uliyoeleza hapa na akakuambia ukaombe msamaha ungekataa? Tena hata jf usingekuja kuandika upuuzi huu. Nyie ndiyo watoto mliojaa ujinga kuwa "nani km mama" ndiyo maana unamdharau baba yako. Nina uhakika km angekuwa ni mama yako mzazi usingemfanyia haya uliyofanya kwa baba yako sema umeona ni baba tena mnaowaita majina ya Kila aina yasiyo na staha km "dingi, mshuwa, Mzee, nk" ndiyo maana umemdharau bila kujua kuwa ipo sku na wewe utazeeka na majina hayo yote yatakuhusu.

Na kinachooneka kinakupa kibri kwa sasa ni hicho ki-degree chako na kikazi ulicho nako bila kujua vyote hivyo havina maana km hujiheshimu na kuheshimu wazazi wako. Hata huyo MKE uliye naye hayuko Smart kichwani, anawezaj kuishi na wewe bila kujua kwenu Wala mzazi wako then she's comfortable kana kwamba wewe ni mtoto yatima? Au ni wale wanawake wa "sogeabtukae". Mwanamke anaejitambua asilani abadani asingekubali kukaa na wewe bila kwenda kumpeleka kwa wazazi wako. Usijifanye kuwa mwerefu sn wakati mbele ni giza. Hivi watoto wako wakikua watajifunza nini kutoka kwako? Jana nilikuambia "what goes around comes around". Take care, "Dunia ni mti mkavu kiumbe usiuegemee." Usibabaike na hivyo vihela kidogo ulivyo navyo.

Kwa hiyo unasubiri baba yako afe ndo ukaombe msamaha kwenye kaburi lake au hata msibani hutaenda na mirathi huitaji. Kumbuka huyo siyo kaka, dada, au mdogo wako kwamba unaweza ku-take easy na maisha yakaenda. Huyo ni mzazi wako unaetembelea damu yake ktk mwili wako na una DNA yake.

Km unajifanya wa kisasa wa kizazi Cha wahuni na ushoga basi endelea kukaza shingo ipo siku hata hao wadogo zako watakuona bwege.

Nimemaliza.
 
Ningekujibu ila basi. Haya mtu mzima.
 
Aaahaahaaa
 
Kituko hiki kikupate wewe na familia yako
 
kituko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…