Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Pamoja na hukumu bado wahusika wakuu hawajapatikana.Kama kweli serikali inataka kujua hii chain, wasiwanyonge wakikaa gerezani kwa muda hawa watasema A to Z kwakuwa watajutia na kumrudia Mungu wao na watafunguka mpaka serikali ishangae unless wataka kufunika kombe kuwaokoa vigogo.
 

* wa Jamhuri ila baadae ikagundulika naye alikuwa na mawasiliano na Karama. Na waliomtaja ni watuhumiwa wengine. Anaweza kubisha kwamba watuhumiwa walimtaja Kama kumkomoa baada ya kusema alimuona ongiste akimpiga risasi Lotter"

Hii sio rahisi, maama ushahidi uliomfunga sio wa kutaja, na lazima wana ushahidi aliongea na huyo mwingine, hakuna motive ingine ya kuongea isipokuwa uhusika katika mauajia, ila wa bureau de change anaweza kutoka ila sio rahisi
 
Sasa rasmi nimethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa wewe ni mpumbavu, yaani pamoja na mwandishi kuandika kwa mtiririko mzuri kabisa ila wewe ulikuwa busy kutafuta jina lenye asili ya kaskazini ulipigie kambi?what a stupid creature?
Walikua ni wa wapi? Si hapa Arusha,ili ujue sikuogopi.. njoo DM nikuelekeze nilipo nione utafanya nini kama upo hapa Arusha mjini, unaukasirikia ukweli
 
Hadi sasa sijaona mahali panapoonesha mahakama inajibu swali la kwa nini wahusika wote hao wahusike kumuua mtu mmoja tu...

Je, wauaji ni majangili wa meno ya tembo?

Je, wauaji ni majambazi wanaochukua kazi za malipo za kuua watu?
Hata mimi
Nimeitafuta sana hii connection. Mahakama ingetuambia hawa waliwahi kuwa na historia ya ujangili etc. Kuna vitu chini ya carpet havijapata mfagiaji
 
Hadi sasa sijaona mahali panapoonesha mahakama inajibu swali la kwa nini wahusika wote hao wahusike kumuua mtu mmoja tu...

Je, wauaji ni majangili wa meno ya tembo?

Je, wauaji ni majambazi wanaochukua kazi za malipo za kuua watu?
Wamekula njama. Japo muuaji ni mmoja so hao watu wote walikuwa wanajua mpango wa mauaji
 

Namfahamu Godfrey Salamba,baba yake ni marehemu Askari Trafic.

Alianza wizi mdogo mdogo akiwa na umri mdogo kati ya miaka 17 mpak 24.

Baada ya kuishi kwa Dada yake Late Mama Peter alikimbilia Shinyanga na kuunda genge la kuwapora wafugaji fedha hasa wanapotoka katika minada.

Baada ya mafanikio makubwa ya uporaji alijenga na kununua nyumba kadhaa Jijini Dar.

Mama yake kipindi chote akiishi maeneo ya Mwananyamala katika chumba kimoja.Baada ya kufiwa na mume wake miaka ya late 1980s.

Kabla ya hili tukio la mauaji tulionana maeneo ya Kaloleni Arusha akimiliki Toyota Land Cruiser 105.Alionekana ni mwenye harakati nyingi huku kila akiongea na simu ambazo hazikuwa za kawaida.Tulikuwa tukimkwepa sana kwakuwa zilikuwepo taarifa za uhakika katika Gari yake alikuwa na silaha na mavazi ya jeshi.

Godfrey mara kadhaa alikuwa akipata nafuu za kisheria kwakuwa marehemu Baba yake alikuwa ni Askari.Godfrey ni msukuma wizi/ ujambazi hauna kabila wala ukanda.
 
Hata wakisema hawawezi geuza lolote lile, hawa kosa lao ni kuua,kula njama ya kuua
 
Namfahamu Issa Ismail Machips.
Huyu ni msomali kwa asili na mwanaCCM kindaki ndaki.

Jina la machips asili yake ni kumiliki mghahawa wa chakula stand Jijini Arusha.Kupitia CCM aliweza kupewa kibali cha ujenzi Banda kitu ambacho hakikuwa cha kawaida.

Machips ni kizazi cha pili cha wasomali waliokuja/hamia Tanganyika kabla ya uhuru.Wazee wao wengi waliweka makazi yao maeneo ya Monduli,Engaruka,Loliondo,Hai na maeneo ya mipakani hasa Kenya.Wengi walijihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo,Faru na ngozi za wanyama kama Simba,Chui ....

Katika kipindi cha utawala wa kikoloni jamii yao ilikuwa juu sana kiuchumi ingawa hawakujihusha sana na masuala ya elimu ukiacha familia chache.Matokeo yake baada ya biashara ujangili kubanwa familia nyingi zilikikuta zimeingia katika umasikini na wengine kukimbilia Ulaya na USA.

Kwa hakika machips na genge lake wataka rufaa baada ya miaka miwili au mitatu watakuwa uraiani wakifurahia mema ya nchi.

Na amini wametiwa hatiani kwasababu aliyeuwawa alikuwa MZUNGU laiti angekuwa mmatumbi mwenzetu Majaji wetu wa michongo wangesema hakuna ushahidi wa uhakika.

Ngongo safarini Ibanda Kyerwa Park.
 
20
20M tu zenye mgao watu 11 zimetoa uhai wa mtu?
 
Kwanza tujue Lotter ni nani na alikuws anafanya kazi gani. Hapa ndio tutajua motive ilikuwa nini? Wanaweza kumuua bila kutumwa pia kutegemeana na sababu ya kumuua.
 
Namfahamu Issa Ismail Machips.
Huyu ni msomali kwa asili na mwanaCCM kindaki ndaki.
Actually siwafahamu hao woote lakini ningekuwa sahihi kama ningesema hao woote watakuwa wana ccm.

Wana ujasiri sana hao wanachama
 
Namfahamu Makoi,asili yake Kibosho akimiliki maduka kadhaa ya madawa (Pharmacy) ingawa hata kidato cha pili hakumaliza.

Kupitia biashara zake za madawa alijikuta akipanda haraka haraka kibiashara kumbe nyuma ya pazia alikuwa na biashara nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…