Hakuna lolote wezi wa uchaguzi hao
Hebu angalia makabila ya watu hawa, Nyerere, Ali Hassani Mwinyi, Willium Mkapa, Jakaya Kikwete, Joseph Magufuli, Samia Hassani, Malecela, Msuya, Sumaye, Majaliwa, Mwigulu, Lowassa, Warioba. Chama kama hiki kuanguka sio rahisi. Hakuna kabila limejirudia hapo kwenye nafasi za Urais, Makamu Rais, Waziri Mkuu, waziri wa fedha. Nenda kaangalie wakuu wa majeshi, majaji wakuu, maspika, wakuu wa usalama, mawaziri, nk. Inclusion yao inawasaidia sana kuwa imara.
mataifa na vyama vingine Afrika vinahangaika sana kwakuwa kuna jamii wanazifungia nje ya mfumo yao. Jamii hizo zinajihisi zimetengwa na zinabaguliwa. Kilio ambacho kinasikika kwa mbaaaaali sana ndani ya CCM ni namna dhehebu moja la kikristo linavyopata nafasi ya urais na makamu wa Rais. Ni sifa zinaamua au kuna maandalizi fulani. hata hivyo hilo sio tatizo kwakuwa hata hilo dhehebu ni watu wa makabila hayahaya ya watanzania.
Kwa mjumuisho huu CCM inaweza kumfukuza yeyote hata ikibidi mwenyekiti wao na Rais wa nchi bila kuyumba. Haka kufa kwa Rais JPM kama kungetokea kwa vyama vingine ndani na nje ya nchi hizi za Kiafrika ungeona kindumbwendumbwe.
View: https://youtu.be/Ml7AEcAIgPY?si=WwK8eUKMujJ7bLgG