Baljurashi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2017
- 2,411
- 3,941
Mnasoma dini lakini kuna vitu hamuelewi, pengine hamtumii fikra vema, mtume kakataza uasi ikiwa tu serikali ya pale inatenda haki. Pitia mafundisho yake mengi utang'amua jambo.
Mtume kakataza uasi hata kama mtawala ni dhalimu;
Hudhayfah ibn al-Yaman reported: I asked, “O Messenger of Allah, we were living in an evil time and Allah brought us good in which we live now. Will there be evil after this good?” The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, “Yes.” I said, “And any good after this evil?” The Prophet said, “Yes.” I said, “And any evil after this good?” The Prophet said, “Yes.” I said, “How will it be?” The Prophet said, “After me, leaders will come who do not follow my guidance or my Sunnah. Some of their men will have the hearts of devils in a human body.” I said, “O Messenger of Allah, what should I do if I live to see that time?” The Prophet said, “You should listen and obey the ruler, even if he strikes your back and takes your wealth, even still listen and obey.”
Source: Ṣaḥīḥ Muslim 1847
Haifai kufanya uasi dhidi ya mtawala hata kama atakuwa muovu na dhalimu.
Kuna hikma kubwa juu ya hili. Watu tumeamrishwa kuwa na subra kunako dhulma ya mtawala.
Hivi kila mtu akiona hatendewi haki akaamua kuasi, kutakuwa na utulivu na amani? Kwenye jamii zetu hizi watu wengi hata hawajui nini maana ya haki, na hapo sijasema kuhusu matamanio ya nafsi za watu kuna watu kwao wanafuata matamanio yao, haki kwao ni kile kinachotamaniwa na nafsi zao kwa wakati huo.
Kujificha nyuma ya "kupigania haki" ndio kumekuwa kukitumiwa na wanaowafanyia uasi watawala tokea zamani huko, baadhi ya watawala walikuwa wema kabisa na waadilifu tena wachaMungu ambao uchaMungu wao umethibiti ila kuna watu waliwasingizia kuwa hawatendi haki na wakafanya uasi dhidi yao.
Dhul Khuwaysira ambaye ndie baba wa makhawaarij (watu wanaowafanyia uasi watawala) alimuambia Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) "tenda haki"!! Can you imagine alimuambia kwa ujasiri kabisa Mtume Wa Allah atende haki wakati Mtume ameaminiwa na Allah Aliye Juu ya Mbingu Saba!!
Na Mtume alitabiri kudhihiri kwa hawa khawaarij ambao kawapa wasifu mbaya sana na akawaita mbwa wa motoni. Na Mtume akawaambia Waislam wamsikilize mtawala hata kama atakuwa ni dhalimu na hata kama mtawala atakuwa ni muovu. Na hata kama mtawala atampendelea mtu juu yetu. Bado tukaambiwa tuwe na subra na tusikilize na tutii.
Ila khawaarij wao wanajitoa katika twaa ya mtawala na mara nyingi hujificha nyuma ya "haki" na wanajuzisha kufanya uasi dhidi yake. Kama baba yao Dhul Khuwaysira alimtuhumu Mtume katika uadilifu wake (Swala na Salamu ziwe juu yake Mtume) nani atasalimika baada ya Mtume??
Kuna hikma kubwa kwa Mtume kukataza kujitoa katika twaa ya kiongozi hata kama huyo kiongozi kiuhalisia kabisa ni dhalimu. Ni katika kuichunga Dini, Nafsi, Mali, Akili na Nasabu/Heshima (vitu vilivyokuja kuchungwa na kulindwa na Shari'ah). Ni katika kuchunga uhai, heshima na damu za Waislam, damu ya Muislam ina thamani kuliko Al Ka'aba Tukufu. Kuchunga mali zao na ustawi wao.
Na kujitoa katika twaa ya mtawala na kumfanyia uasi kunasababisha fitna ambayo inakuja kuharibu kabisa vile vinavyochungwa na Shariah.
Khawaarij walipomfanyia uasi Swahaba Mtukufu kabisa aliyebashiriwa Pepo akiwa hai, Swahaba ambaye Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) alimuozesha binti zake wawili (nyakati mbili tofauti), Swahaba ambaye mpaka Malaika walikuwa wakimuonea haya, Uthmaan Ibn 'Affan (Allah Amridhie), makhawaarij walipomfanyia uasi na wakamuua, kukaibuka fitna na mgawanyiko katika Ummah huu mpaka leo hii.
Hutanabahi na hilo!!
Ndio maana Mtume aliwapa wasifu mbaya makhawaarij na akawaita mbwa wa motoni. Shari yao ni kubwa!
Wewe huoni mpaka Leo uasi dhidi ya watawala ulivyoziharibu baadhi ya nchi za kiislam?
Mtume Muhammad ﷺ amesema:
"Atakayeona jambo ovu, na alibadilishie kwa mkono wake; akishindwa basi kwa ulimi wake; na akishindwa basi kwa moyo wake, na huko ndiko ni udhaifu wa imani."
(Imepokewa na Imam Muslim)
Zingatia hapo nilipobold.
Halafu je, Salaf (Maswahaba na Wanafunzi wao na Wanafunzi wa Wanafunzi wao) walielewaje maneno hayo.
Kuzuia munkar kumefungamanishwa na uwezo. Wanaoondoa munkar kwa mkono ni wale wenye mamlaka kama watawala, au baba kwa familia yake kwa yale anayoyaweza. Ukishindwa (yaani ukiwa huna huo uwezo) basi kwa mdomo na hili ni kwa wanachuoni na wenye elimu kwa kadri ya elimu yao. Kama imeshindikana basi tuchukie moyoni.
Huoni wewe Waislam walipokuwa Makkah na hawana uwezo hawakupigana, wala kufanya maandamano na migomo na uasi. Na walikuwa wakiona munkar mkubwa kabisa kuliko wowote ule ambao ni Shirki? Masanamu yalikuwa yanawekwa kwenye Al Ka'aba na Waislam wakiona, walifanyaje?
Na mtawala tushafundishwa namna ya kumnasihi. Soma hadith ifuatayo;
The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, “Whoever intends to advise one with authority, he should not do so publicly. Rather, he should take him by the hand and advise him in private. If he accepts the advice, all is well. If he does not accept it, he has fulfilled his duty.” Source: Musnad Aḥmad 14909 Grade: Sahih (authentic) according to Al-Albani
Mtawala hasemwi kwenye majukwaa au mitandaoni. Ukitaka kumnasihi mfuate umnasihi kwa siri uso kwa uso, ukipata hiyo fursa, au umuandikie kwa siri. Kinyume na hapo unapaswa kuwa na subra.
Haifai maandamano, migomo, mapinduzi, au uasi. Kuna madhara makubwa mno katika haya. Madhara ambayo Shari'ah ya Kiislam imekuja kuyaondoa na kuyazuia.
Na mwisho maandamano kama maandamano ni jambo ambalo halina asili katika Shari'ah ya Kiislam ni haramu kabisa.
Na haifai kabisa kujitoa katika twaa ya mtawala na kumfanyia uasi au kumsema hadharani au kuchochea watu dhidi yake na tunatakiwa kumsikiliza na kumtii (maadamu anayoamrisha sio haramu) hata kama atakuwa dhalimu na muovu na haifai kujitoa katika twaa yake.
Na Allah Ni Mjuzi zaidi.