Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Hawa waisalmu wa morocco ni makafiri sana kwanini wanaandamana.

Says mmatumbi kutoka ofisi ya mtolo.
Sio Makafiri bali wanatemba uovu na dhambi ,sio kila dhambi na uovu inamfanya mtu awe kafiri.

Kusema mtu kafiri ni jambo kubwa linahitajia Elimu.
 
Moja kwa moja..

Sababu ya kuandika huu uzi ni kutokana na baadhi ya fikra za Wabongo wanona kutokana na mapungufu ya serikali bora tukiwashe na kukinikisha wengine wakienda mbali wanasema damu zikimwagika ndio tutaheshimiana. Nawaambia ndugu zangu Amani ni jambo muhimu sana bila kujali mambo gani yanaendelea waulizeni Hamas waliona bora kukiwasha kuliko unyonge sasa wamepata Faida na madhara gani , cheki Sudan mambo ya kupindua utawala yamepeleka uovu zaidi na hali mbaya mno , Libya nk mnoshadadia tukiwashe hamjui huku kwetu machafuko yatafika mbali kiasi gani na kusababisha madhara gani , kwa sisi ambao tumewahi kuishi sehemu kukiwa na mabomu na mitutu mara kwa mara tunaelewa Amani ni jambo zito kiasi gani.

Uislamu ni dini kamili ina sheria na miongozo yake inayojitosheleza katika kila jambo na tatizo lilipo Waislamu wengi tumekuwa wavivu wa kukaa chini kusoma dini yetu kwa uhakika na usahihi na hili swala ndio chanzo kikubwa cha matatizo kwa Umma wa Kiislamu kupelekea wengi kufuata mihemko , mkumbo na matamanio ndio maana Kuna kipindi baadhi ya Waislamu Osama walimuona kama Kidume na shujaa wa Kiislamu , wengine wakafuata mikumbo kuingia katika makundi potofu ya Jihadi na kuanzisha vuguvugu mbalimbali.

Na upande wa Wakristo wengi pia hawana ufahamu sahihi na Elimu ya uhakika kuhusu Uislamu ndio maana sio ajabu kukuta eti Mkiristo kukuambia Qur'an ina majini , Kufunga majini nk . Tatizo hili kuu la kukosa Elimu limepelekea wengi katika Wakristo au Waislamu ukiwaelekeza jambo Fulani la sawa kuhusu Uislamu wanaona kama ni jambo geni kwao na wanaweza kukupinga tu.

MIAKA YA VUGUVUGU ZA UASI KWA WAISLAMU

Kama mnakumbukumbu vizuri miaka kuanzia 2010 - 2013 hapa bongo kulitokea vuguvugu kubwa lililopamba moto kwa Waislamu wanaonewa na serikali katika nyanja mbalimbali na wengine wanaojiita Masheikh walikuwa Mstari wa mbele waliwahamaisha kuhamasisha maandamano, Fujo , uasi nk na ilileta madhara makubwa mpaka serikali ikaamua sasa kuvalia njuga ikakamata Masheikh na watu wengi Wenye hatia , wasio na hatia hata redio Moja maarufu ya Waislamu ilifungiwa kutokana na kuchochea chuki na uasi hatimaye hali ikapoa vuguvugu likapotea mpka sasa hali shwari.

MAANDIKO YANASEMAJE ?

Uasi (khurooj) hufafanuliwa kama kujaribu kunyang’anya mamlaka kutoka kwa mtawala, kumpinga hadharani, kujaribu kumwondoa madarakani kwa nguvu, kuwachochea watu dhidi yake (kupitia maandamano, mikutano ya hadhara, maandamano ya barabarani, migomo, n.k.), kupanga njama dhidi yake na kuinuka kumpinga kwa maandishi, kwa khutuba au kwa upanga.

Haya yote yanachukuliwa kuwa ni khurooj. Mtume (ﷺ) alikataza jambo hili katika hadithi zilizo wazi na zenye nguvu. Hadithi ambazo haziwezi kupingwa na matamanio, maoni binafsi au akili, wala kwa maamuzi yasiyo sahihi ya watu, bila kujali daraja yao mbele ya watu. Mtume (ﷺ) alizungumza kwa wahyi (ufunuo) kutoka kwa Allah, lakini waliokuja baada yake hawakuwa na wahyi. Kwa sababu hiyo, wakati ijmā’ (makubaliano ya pamoja ya wanazuoni) ilipothibitishwa, hakuna aliyepinga isipokuwa Khawārij, Shia, Mu’tazilah na matawi yao hadi wakati wetu huu.

Imepokewa na Muslim katika Sahih yake (1847) kutoka kwa Wā’il Ibn Hujr kuwa: Salamah Ibn Yazeed Al-Ju’fee alimuuliza Mtume wa Allah (ﷺ): “Ewe Mtume wa Allah, tufanye nini ikiwa tutakuwa na watawala juu yetu wanaotaka haki zao lakini wanatunyima haki zetu?” Akajibu: “Wasikilizeni na watiini [bila kujali]. Juu yao ni mzigo wao, na juu yenu ni mzigo wenu .”

MY TAKE :

Fikra za Kikhawarij (kutoka chini ya utii wa matawala ) ndio zimesababisha madhara ya Leo kuwepo Al Shabaab, Al Qaeda , Boko Haram nk wote hawa madai yao kwamba watawala hawaendesh kisawasawa wanaendesha mambo Kikafiri vurugu , kuingia msituni na kutoka dhidi yake.

Kubadilisha mtawala sio solutions ya matatizo yote ya kutawala , wakati wa kifo cha JPM baadhi ya watu mlishangilia na kumdhihaki vibaya mno na kuona matatizo yameisha na makundi yote yaliungana na kuimba mapambio ya "Mama anaupia mwingi " kuwaumiza wafuasi wa JPM sasa mmebadili gia angani.

Uzi huu unaendelea maana bado sijatoa solutions na Kuna mambo Muhimu bado sijayagusia

UPDATES :

1. Tuone kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu


Nabii Musa (Amani iwe juu yake ) alikuta Wana wa Israeli wakionewa chini ya utawala wa Kiongozi Dhalimu mkubwa Firauni lakini hakuwa kuhubili Wana wa Israeli wafanye njama ya kumtoa Firauni Madarakani au wafanye maandamano na Uasi bali yeye aliwaningania katika neno la Mungu .

Na hiyo ndio wito wa Manabii mara nyingi hawapendi kushindana na Serikali kwa kutaka kupanga njama za kuwapondua uasi , fujo nk wao wamefocuos kuwapa neno la haki kwa njia Bora . Mfano Yesu , Nuh , Shuayb, Yusuph na wengineo ( Amani iwe juu Yao wote
a)Kutoka kwenye maisha ya Kiigizo chema Mtume Muhammad (ﷺ)

Msingi mwingine dini ya Uislamu katika kila ibada kiigizo chetu ni Mtume Muhammad (ﷺ) lazima iangaliwe yeye alifanya vipi ili jambo liitwe dini kinyume na hapo ni uzushi , sasa angalia maisha yake kipindi Cha utume katika mji wa Makkah ambapo Uislamu ulipokuwa hauna nguvu. Je , Waislamu wangapi waliuwawa kwa dhuluma , kuteswa , kuporwa mali zao , dhihaka na madhila mengine makubwa ? Je alimarisha kisasi , maandamano, Fujo , njama , mapinduzi nk ?

Jawabu hapana, walifanya subra na wakamcha Allaah hatimaye wakafanya Hijra kuhamia Madina ili kuepuka dhuluma na manyaso na sio kutumia Maguvu kuminyana na watawala wakati hata nguvu zenyewe hauna na madhara yatakayo patikana kwa watu ni makubwa mno.

#LindaAmaniYaNchiYako

View attachment 3353969


Wazinzi tu
 
Nani kasema waarabu tu ndiyo wanaua ...jibu swali langu kwanza ...muhammad ni dhehebu gani ? Ni wahy kutoka kwa nani mmeupokea hadi kuanzisha madhehebu ?
Kwanza unajua maana ya madhehebu katika Uislamu ?

Usije ukaleta akili zako za Mabange na kubeti hapa wakati haujui mambo.
 
Shida unafikiria ndani ya fensi ya kiimani as if taifa linaendeshwa kwa misingi ya dini au ibada,huko ndio kupotoka kwenyewe.

Hapa unatetea nani sasa tukikuuliza,raia wenzako, waislam, chama,au viongozi ambao kila siku wanabambwa na maskendo ya wizi wa pesa za serikali na kuhujumu uchumi bila kuchukuliwa hatua yoyote?🤔

Kuna kitu kinaitwa logical reasoning. Unapoona watu wanapishana then jua kuna ambaye yupo sahihi na ambaye hayupo sahihi kulingana na situation iliyopo.

Huwezi kuongelea kwamba hili ni swala la waislam kihujumiwa au wakristo kuhijumiwa au kabila flani kuhujumiwa wakati bei za mafuta za kifisadi zinatuumiza sote, matumizi mabaya ya kodi zetu na mikopo kutoka nje inatuumiza sote kwa ujumla kama watanzania, bima ya afya sote hatuna sababu ya wizi wa pesa za michango ya bima tunapotoa kwa moyo m'moja, wastaafu kutolipwa mafao yao sote tunaumia, mfumo wa hovyo wa elimu na malipo duni kwa watumishi kama walimu na askari hajabagua dini wala kabila wote wanaumia, wewe hapo siajabu unaandika hapa ila unapita kwenyr barabara ya vumbi na gari yako kila siku inapata break down sababu ya barabara mbovu zisizotengenezwa sababu ya wizi wa pesa za miradi ya miundo mbinu.

Wewe unachotetea ni nini hasa?

Kwanini hivi baadhi ya watanzania huwa mnakuwa wazito kama kwenye vichwa m'mewekewa oil chafu badala ya ubongo?

Kwanini unashindwa kuja kuandika hoja za kitanzania unatuwekea mitazamo ya kidini na kiimani katika swala la kitaifa na la kisheria kabisa?

Kwahiyo wewe uzembe unaotokea Serikalini kwa makusudi kabisa ni unakufurahisha na unataka watanzania waendelee kuishi kizembe vizazi vyote si ndivyo?🤔

Hebu msiwe na ujinga muda mwingine.
 
IMG_20251010_132721.jpg
 
Je uislam unaruhusu kuongozwa na mwanamke? Je utawala ukiwa unaunga mkono ushoga, mauaji, utekaji, nk napo hakuna kupngana nao?
 
Je uislam unaruhusu kuongozwa na mwanamke? Je utawala ukiwa unaunga mkono ushoga, mauaji, utekaji, nk napo hakuna kupngana nao?
Hairuhusu .

Je , ikitokea Uislamu unatakaje tumpige ?

Haina mana hata ukimtoa Mwanamke bado utaongozwa na mfumo wa Kidemokrasia ambao ni ushetani upo kwa kufuata matamanio.

Ingekuwa ukimtoa Mwanamke tutaongozwa Kiislamu kidogo ingeMake sense .
 
Back
Top Bottom