Uislamu ni tofauti na wengi tunavyouchukulia: Haya ni mambo ambayo watu walielewa tofauti kuhusu uislamu

1.Huko kusema Mungu hayuko,ndio kuwako kwake.
2.Hakuna contradiction yoyote ni wewe elimu yako ndogo.Lazima usome,uislamu unasomwa,na kujifunza,ndio utaulewa.Ni sawa na wewe kumuona Doctor akimpasua mgonjwa,kwa vile hukusomea udaktari, utaona Doctor,anazidi kumuongezea maradhi mgonjwa;kumbe ndio matibabu wenyewe.Kasome acha ujanja janja,waliosoma wanakucheka,hawakuambii.
 
Kama kusema Mungu hayupo, ndiyo kuwako kwake, basi kusema kwako Mungu yupo ndiyo kutokuwapo kwake, kwa kutumia sheria hiyo hiyo ya ku invert maana.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, kusingekuwa na mtu mwenye elimu ndogo ya kumuelewa.

Wote tungepeea elimu yote ya kumuelewa.

Hivyo, hoja yako ya kwamba kuna watu wana elimu ndogo ya kumuelewa Mungu, inathibitisha Mungu hayupo.

Wewe unaona unatoa hoja ya kutetea uwapo wa Mungu, lakini, kiuhalisia na kikweli unatoa hoja ya kukanusha uwepo wa Mungu.
 
Hizo nguvu nyingi,unazozitumia kusema Mungu hayupo,ndio kuweko kwa Mungu.Kisichokuwepo,hakitumiwi nguvu nyingi ya kujulishwa kuwa hakipo.
 
Hizo nguvu nyingi,unazozitumia kusema Mungu hayupo,ndio kuweko kwa Mungu.Kisichokuwepo,hakitumiwi nguvu nyingi ya kujulishwa kuwa hakipo.
Kwa kanuni hiyo hiyo.

Na wewe hiyo nguvu nyingi unayotumia kusema Mungu yupo, ndiyo kutokuwepo kwa Mungu.

Kilichopo hakitumiwi nguvu nyingi kujulishwa kuwa kipo.

Kusema Mungu yupo au Mungu hayupo hakufanyi awepo au asiwepo.

Kama vile kusema wewe ni bilionea au si bilionea hakukufanyi wewe uwe au usiwe bilionea.

Kuna ukweli ambao hautegemei watu wanasema nini.

Na ukweli huo ni kwamba, Mungu hayupo.

Hili tunaweza kulithibitisha kimantiki.
 
Kuwepo kwa Mungu hakutumiki nguvu nyingi.Ingekuwa hayupo kanunizake zisingekupo
1.Watoto wote wachanga wanzaliwa wanalia,awe wa tajiri,wa maskini,wa mfalme,kiongozi,awe mzungu,awe mweupe,awe mweusi sana,awe mweusi,awe maji ya kunde.Ingekuwa hakuna Mwenye kuyafanya hayo,wanasayansi wangetengeneza dawa;watoto wa kitajiri wakizaliwa wanacheka
2.Kifo,tajiri anakufa,maskini anakufa,mweupe anakufa mweusi ana kufa.Hakuna mwanasayansi anayeweza kubadilisha kifo.
3.Kwenda choo,kikubwa na kidogo,maskini anakwenda tajiri anakwenda,mweusi anakwenda mweupe anakwenda,hakuna mwanasayansi mwenye kubadilisha,tajiri asiende choo,na pia choo chake kikubwa kinukie vizuri.
 
Unashindwa kuelewa,ubilionea ni sifa sio uwezo wa utendaji.Aliye bilionea anaweza kuwa fukara,na aliyefukara akawa bilionea.
 
Nakuambia thibitisha Mungu yupo, unaanza kuongelea kanuni zake, unajuaje hizo unazoziita kanuni zake ni kanuni zake kweli, na kuwa hiyo habari nzima ya kanuni zake si hadithi ya uongo tu mnayohadithiana?

1. Watoto kulia ni uthibitisho kwamba wanalia, si uthibitisho kwamba Mungu yupo. Hujathibitisha Mungu yupo, umethibitisha una amini Mungu yupo, mawili hayo ni tofauti.

2.Watu kufa si uthibitisho kwamba Mungu yupo. Kwanza, kifo kinathibitisha Mungu hayupo. Kifo kinatenganisha watu wanaopendana, kwa huzuni na uchungu mkubwa. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, kifo kisingekuwepo.Mungu huyo si mkatili hivyo kuruhusu kifo kiwepo na kitenganishe viumbe wake kwa huzuni na uchungu mkubwa. Hii hoja ya kifo inathibitisha Mungu hayupo, haithibitishi Mungu yupo.

3. Kwenda choo kifizikia ni ku produce waste products. Mashine ku produce waste products maana yake ni inefficiency, maana yake mashine haina 100% efficiency. Maana yake mwili wa mtu hauna 100% efficiency. Maana yake mwili huu haujaumbwa na Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.Ungekuwa umeumbwa na Mungu huyo, asingeruhusu usiwe na 100% efficiency.

Hoja zako mwenyewe zinaonesha Mungu hayupo zaidi ya zinavyoonesha Mungu yupo.
 
Unashindwa kuelewa,ubilionea ni sifa sio uwezo wa utendaji.Aliye bilionea anaweza kuwa fukara,na aliyefukara akawa bilionea.
Nikisema una mikono nane, wakati huna mikono nane, mimi kusema hivyo kutakufanya uwe na mikono nane?
 
amekusudia kukuua hivyo kupigana vita/kuua kunakuwa ni kwa sababu ya kujihami, kujitetea au kupambania kuondosha fitina iliyokithiri ili haki itendeke kwa wanajamii.
Vipi, Boko haramu wanampiga nani wanayehofia atawapiga?
 
Vipi, Boko haramu wanampiga nani wanayehofia atawapiga?
Inaonekana hujasoma bandiko lote bali ukaishia kipande ulichoniquote. Mbona swali unalouliza majibu yake yapo paragraph inayofuata hapo hapo mbele ya kipande ulichoniquote
 
Tofautisha hadithi na Qur'an,mimi nakuletea aya za Biblia sio hadithi.
Lete aya ya Qur'an.Hadithi ni maneno ya watu,yapo ya ukweli na yapo ya uongoView attachment 2706257View attachment 2706258
Hata Quran ni Hadith Tamu Tamu!
[emoji116][emoji116]
اللَّهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ هُدَى اللَّهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ

[ AZZUMAR - 23 ]
Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa.
 
Huwezi kutenganisha uislam na UGAIDI,kuua,chinja chinja nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…