Uislamu ni tofauti na wengi tunavyouchukulia: Haya ni mambo ambayo watu walielewa tofauti kuhusu uislamu

Uislamu ni tofauti na wengi tunavyouchukulia: Haya ni mambo ambayo watu walielewa tofauti kuhusu uislamu

Uislamu umejengwa jatika uongobjwamba Mungu mjuzibwa yite, mwenye uwezo wote na upendo wote, Allah, yupo.

Mungu huyo hayupo. Hili linaweza kuthibitishwa kimantiki.

Pia, kitabu cha Uislamu, Quran, kina contradictions nyingi sana.

Contradictions hizo zinaonesha kwamba, hiki si kitabu cha Mungu, ni kitabu cha watu tu waliokuwa wanapambana na hali zao kwa siasa zao.

Ndiyo maana unaona hapa unaambiwa ua, kule unaambiwa usiue. Kitabu hakina logical consistency.

Kama unabisha.

1. Thibitisha Mungu yupo.

2. Nikubalie niweke contradictions za kwenye Quran hapa tuzichambue uzitatue.
1.Huko kusema Mungu hayuko,ndio kuwako kwake.
2.Hakuna contradiction yoyote ni wewe elimu yako ndogo.Lazima usome,uislamu unasomwa,na kujifunza,ndio utaulewa.Ni sawa na wewe kumuona Doctor akimpasua mgonjwa,kwa vile hukusomea udaktari, utaona Doctor,anazidi kumuongezea maradhi mgonjwa;kumbe ndio matibabu wenyewe.Kasome acha ujanja janja,waliosoma wanakucheka,hawakuambii.
 
Kwaiyo unakubali shetani ni muislamu na alikuwa na nguvu.
Angaliq hapo,nakupa kwa aya sio hadithi,Yuda anambusu Yesu,Biblia Takatifu imetueleza
Matay 26:49
Screenshot_2023-08-02_144644.jpg
 
1.Huko kusema Mungu hayuko,ndio kuwako kwake.
2.Hakuna contradiction yoyote ni wewe elimu yako ndogo.Lazima usome,uislamu unasomwa,na kujifunza,ndio utaulewa.Ni sawa na wewe kumuona Doctor akimpasua mgonjwa,kwa vile hukusomea udaktari, utaona Doctor,anazidi kumuongezea maradhi mgonjwa;kumbe ndio matibabu wenyewe.Kasome acha ujanja janja,waliosoma wanakucheka,hawakuambii.
Kama kusema Mungu hayupo, ndiyo kuwako kwake, basi kusema kwako Mungu yupo ndiyo kutokuwapo kwake, kwa kutumia sheria hiyo hiyo ya ku invert maana.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, kusingekuwa na mtu mwenye elimu ndogo ya kumuelewa.

Wote tungepeea elimu yote ya kumuelewa.

Hivyo, hoja yako ya kwamba kuna watu wana elimu ndogo ya kumuelewa Mungu, inathibitisha Mungu hayupo.

Wewe unaona unatoa hoja ya kutetea uwapo wa Mungu, lakini, kiuhalisia na kikweli unatoa hoja ya kukanusha uwepo wa Mungu.
 
Hizo nguvu nyingi,unazozitumia kusema Mungu hayupo,ndio kuweko kwa Mungu.Kisichokuwepo,hakitumiwi nguvu nyingi ya kujulishwa kuwa hakipo.
 
Hizo nguvu nyingi,unazozitumia kusema Mungu hayupo,ndio kuweko kwa Mungu.Kisichokuwepo,hakitumiwi nguvu nyingi ya kujulishwa kuwa hakipo.
Kwa kanuni hiyo hiyo.

Na wewe hiyo nguvu nyingi unayotumia kusema Mungu yupo, ndiyo kutokuwepo kwa Mungu.

Kilichopo hakitumiwi nguvu nyingi kujulishwa kuwa kipo.

Kusema Mungu yupo au Mungu hayupo hakufanyi awepo au asiwepo.

Kama vile kusema wewe ni bilionea au si bilionea hakukufanyi wewe uwe au usiwe bilionea.

Kuna ukweli ambao hautegemei watu wanasema nini.

Na ukweli huo ni kwamba, Mungu hayupo.

Hili tunaweza kulithibitisha kimantiki.
 
Kuwepo kwa Mungu hakutumiki nguvu nyingi.Ingekuwa hayupo kanunizake zisingekupo
1.Watoto wote wachanga wanzaliwa wanalia,awe wa tajiri,wa maskini,wa mfalme,kiongozi,awe mzungu,awe mweupe,awe mweusi sana,awe mweusi,awe maji ya kunde.Ingekuwa hakuna Mwenye kuyafanya hayo,wanasayansi wangetengeneza dawa;watoto wa kitajiri wakizaliwa wanacheka
2.Kifo,tajiri anakufa,maskini anakufa,mweupe anakufa mweusi ana kufa.Hakuna mwanasayansi anayeweza kubadilisha kifo.
3.Kwenda choo,kikubwa na kidogo,maskini anakwenda tajiri anakwenda,mweusi anakwenda mweupe anakwenda,hakuna mwanasayansi mwenye kubadilisha,tajiri asiende choo,na pia choo chake kikubwa kinukie vizuri.
 
Unashindwa kuelewa,ubilionea ni sifa sio uwezo wa utendaji.Aliye bilionea anaweza kuwa fukara,na aliyefukara akawa bilionea.
 
Nakuambia thibitisha Mungu yupo, unaanza kuongelea kanuni zake, unajuaje hizo unazoziita kanuni zake ni kanuni zake kweli, na kuwa hiyo habari nzima ya kanuni zake si hadithi ya uongo tu mnayohadithiana?

1. Watoto kulia ni uthibitisho kwamba wanalia, si uthibitisho kwamba Mungu yupo. Hujathibitisha Mungu yupo, umethibitisha una amini Mungu yupo, mawili hayo ni tofauti.

2.Watu kufa si uthibitisho kwamba Mungu yupo. Kwanza, kifo kinathibitisha Mungu hayupo. Kifo kinatenganisha watu wanaopendana, kwa huzuni na uchungu mkubwa. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, kifo kisingekuwepo.Mungu huyo si mkatili hivyo kuruhusu kifo kiwepo na kitenganishe viumbe wake kwa huzuni na uchungu mkubwa. Hii hoja ya kifo inathibitisha Mungu hayupo, haithibitishi Mungu yupo.

3. Kwenda choo kifizikia ni ku produce waste products. Mashine ku produce waste products maana yake ni inefficiency, maana yake mashine haina 100% efficiency. Maana yake mwili wa mtu hauna 100% efficiency. Maana yake mwili huu haujaumbwa na Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.Ungekuwa umeumbwa na Mungu huyo, asingeruhusu usiwe na 100% efficiency.

Hoja zako mwenyewe zinaonesha Mungu hayupo zaidi ya zinavyoonesha Mungu yupo.
 
Unashindwa kuelewa,ubilionea ni sifa sio uwezo wa utendaji.Aliye bilionea anaweza kuwa fukara,na aliyefukara akawa bilionea.
Nikisema una mikono nane, wakati huna mikono nane, mimi kusema hivyo kutakufanya uwe na mikono nane?
 
amekusudia kukuua hivyo kupigana vita/kuua kunakuwa ni kwa sababu ya kujihami, kujitetea au kupambania kuondosha fitina iliyokithiri ili haki itendeke kwa wanajamii.
Vipi, Boko haramu wanampiga nani wanayehofia atawapiga?
 
Vipi, Boko haramu wanampiga nani wanayehofia atawapiga?
Inaonekana hujasoma bandiko lote bali ukaishia kipande ulichoniquote. Mbona swali unalouliza majibu yake yapo paragraph inayofuata hapo hapo mbele ya kipande ulichoniquote
 
Tofautisha hadithi na Qur'an,mimi nakuletea aya za Biblia sio hadithi.
Lete aya ya Qur'an.Hadithi ni maneno ya watu,yapo ya ukweli na yapo ya uongoView attachment 2706257View attachment 2706258
Hata Quran ni Hadith Tamu Tamu!
[emoji116][emoji116]
اللَّهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ هُدَى اللَّهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ

[ AZZUMAR - 23 ]
Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa.
 
Salaam alaykum...

Wengi wamekuwa wakipotosha watu kuhusu uislamu mpaka watu hao (wapotoshwaji) wamekuwa wakiona uislamu ni kitu kisichofaa katika jamii. Haijaisha hapo tu bali hata waliofuata huo uislamu wamepotoshwa baadhi ya mambo mpaka kufikia kuona dini yao ni chungu na ngumu kutekeleza

Tuongelee pande zote mbili yaani ugumu uliowekwa kwa mtu kuingia uislamu na ugumu uliowekwa kwa waislamu wenyewe

Tukianza na upotoshaji unaomkimbiza asiye muislamu

1. Ugaidi
Matendo yote ya ugaidi na yasiyoendana na ubinadamu mfano uhaini, uuaji bila hatia, ubakaji, ni miongoni mwa mambo yanayopingana vita sana na uislamu. Hoja wanazozisema wengi kuhusu uislamu kuwa ni ugaidi zinajibika kirahisi tu kwa mwenye kutaka kuelewa anaelewa. Aya za quran zote wanazocopy na kupaste wakisema zinasapoti kuua ukiangalia zinaongelea/zinaamrisha kuua baada ya kuwa adui amekusudia kukuua hivyo kupigana vita/kuua kunakuwa ni kwa sababu ya kujihami, kujitetea au kupambania kuondosha fitina iliyokithiri ili haki itendeke kwa wanajamii.

Tena hata kuua huko kuna masharti yake kadha wa kadha siyo kuua kwa mtu atakavyo. Mfano wale wanaoambiwa wanajitoa mhanga, wanaoteka mabinti na kuwanyanyasa (kama ni kweli) basi hiyo ni kwa matakwa yao wenyewe tu lakini uislamu unatetea kila mtu. Ushauri; hizo aya zote wanazosema humu watu na kuzipaste hebu ukiipata usiishie hapo tu bali soma kifungu chote (karaa) au sura kabisa halafu baada ya hapo utarudi. Kwa tafsiri ya ugaidi na maana zake hakuna aya wala hadithi hata moja utakayopata ikisapoti hiyo kitu!

2.Ubaguzi
Kuna mambo mengi ya kiibada ambayo muislamu akifanya kwa kuzingatia dini yake anaonekana kama anafanya ubaguzi kumbe siyo hata. Maswala kama ya ndoa muislamu haruhusiwi kufanya ibada hii ya kufunga ndoa na asiye muislamu, kuchinja muislamu haruhusiwi kula kilichochinjwa na asiyekuwa muislamu, muislamu haruhusiwi kushiriki ibada za wasiokuwa waislamu. Hayo yote siyo ubaguzi bali ni utaratibu wa dini kama ilivyo kwa dini zingine kuwa na mambo ambayo yanawahusu wao wenyewe tu na mengine yakawahusu watu wote na ndiyo maana hata kwa waislamu wakaruhusiwa kushirikiana na wasio waislamu kwa maswala yasiyokuwa ya ibada mahsusi mfano kula pamoja, kupiga stori, kufanya kazi, nk

3.Kuhusu Muhammed
Wapo waliomzushia mtume mambo mengi sana lakini majibu yote yametolewa kwenye quran sitaki nirudie rudie. Bali nitajikita kwenye uzushi mmoja tu kwamba Muhammed alikuwa anapenda sana ngono hasa na vitoto ndomaana alimwoa Aisha katoto. Watu wanaoelewa Historia vizuri wanacheka tu wakiona huu uzushi maana Muhammed amekuwa akiaminiwa tangu utoto mpaka ujana wake mpaka utu uzima wake hata kabla hajapewa utume watu wote walimpenda kwa ubora wa tabia aliyokuwa nayo haya huo uzinzi umetoka wapi. Pia huyu mtu ujana wake wala hakuufaidi ukitaka ukweli maana ana miaka 25 ndo akapata mke wake wa kwanza tena mwanamke akiwa na miaka 40! Mapungufu yote anayosingiziwa Mtume huyapati kwenye hadithi sahihi wala quran

4.Kuhusu Allah, Quran na shetani
Wengi wanaaminisha watu kwamba Allah ndiye shetani mara hivi mara vile. Jamani hebu tusome kwa uelewa vitu siyo kwa kumezeshwa. Kuna aya hapa wanapenda kuipaste kwamba eti shetani ndiye kateremsha kuran kumbe masikini ni shida ya kuelewa maandishi tu wala mola hakumaanisha kuwa ni shetani bali malaika jibril. Soma aya zote zinazotaja vitatu hivyo Allah, Quran na Iblis halafu utajionea mwenyewe

5.Kwamba ukiritadi unauawa. Hoja hii wanaipenda sana masikini lakini wanashindwa kusoma andiko lote lililoko pale. Kama ingekuwa ni kweli hicho wanachosema uislamu ndo ulivyo basi tungeona au hata kusikia huko watu wkiuawa kwa

Twende upotoshwaji kwa waislamu wenyewe

1.Ukiingiwa na najisi ya nguruwe usiswali siku 7 (wengine wakasema siku 40) eti baada ya hapo ndiyo unatwaharika. Ukishajitwaharisha vizuri kwa kufuata taratibu zote zinazokubalika basi wewe ni kazi kazi tu wala hakuna sheria hiyo ya kukaa bila kuswali

2.Janaba la zinaa linaisha kwa siku 40 eti ukizini na mwana wa watu hata kama utaoga usiingie msikitini siku 40 zipite ndipo utakuwa umetwaharika. Huu ni ujinga wa kiwango kikubwa sana, kalamu inasimama kwa mtoto mdogo, aliyepoteza fahamu/akili na aliyelala sasa sijui huyu wa siku 40 haswali anajinasulia wapi kwenye kuulizwa swala 200 atakazoziacha

3. Mama akijifungua anaogeshwa na shekhe. Hii ndo inauma sana aisee wazee wa zamani eti anaitwa akamuogeshe mmama wa watu yaani ni ushetani juu ya ushetani. Hadathi zote kama ilivyo najisi mtu anajitwaharisha mwenyewe tu sijui mashekhe wa zamani walikuwa na mpango gani na wadada wa watu

4. Mtu akichinja inabidi apewe shingo (ya mnyama aliyechinjwa). Hii mpaka sasa hivi huku nilipo bado wanayo yaani nyama ikiiva tu atatafutwa apewe shingo yake na kama mchinjaji akiifuata yeye mwenyewe akakuta imeliwa anadai hela. Hiyo kitu haipo wewe chinja uondoke ukipewa baadae ni swadaqa tu usipopewa isiwe deni wala mtoaji asifanye ni lazima akuchagulie shingo ndo akupe huo ni uzushi. Hela analipwa yule ambaye hiyo ni kazi yake mfano mchinjaji buchani, hotelini nk

5. Biashara inatakiwa kuuza faida isizidi robo yake (wengine nusu yake) yaani kama kitu umenunua sh.100 maana yake usiuze kwa bei ya itakayozidi 125 (robo) au 150 (nusu). Huu ni uongo mwingine wa mchana kweupe. kilichokatazwa kwenye biashara ni uongo na ulaghai tu lakini kama kitu umeamua kuuza laki na wewe ulinunua mia na mteja akakipenda akaridhia kununua bila kumchomekezea maneno ya kumpambisha na kumlaghai basi kitu hicho unaruhusiwa kumuuzia tu bila shida

6. Lailatul qadr ni nyota ing'aayo sana na ukipata bahati kuiona (ikikutokea hiyo nyota) basi unaomba chochote na hapaohapo unapata. Huu ni uongo ambao wengi bado wanao na tatizo ni darsa watu hawasomi madrasa wakaelewa. Usiku wa cheo, lailatul qadr ni usiku ndiyo lakini hauna alama yoyote kwamba mtu atasema ameupata bali tunahimizwa kufanya yaliyo mema zaidi ndani ya usiku huo (mfano kuswali, kusoma quran, kumsifu mola, kutoa sadaka nk) ili uwe umefanya jambo jema kwenye usiku bora kabisa. Haihusiani na nyota fulani wala jeneza wala kaburi wala...

7. Matendo mema ni kukusanya watu kufanya dua, kusoma maulidi, kuzuru na kusafishia makaburi, kuwafanyia dua ya kumbukumbu ya watu waliokufa, kusoma barzanji mara kwa mara, dhikri ya kidarueshi (ya kukohoa). Hapo kuna mambo mengi sana ambayo watu wamekuwa wakikomaa nayo huku wakiacha matendo mema kabisa kuliko yote ambayo ni kuswali, kusoma quran, kutoa zaka na sadaka, kufunga, kuelimisha watu, kukumbusha watu wadumu na matendo mema na kuzuia watu wasifanye maasi, kuwatii wazazi, nk

Mambo ni mengi sana ila yote kwa yote ni kwamba uislamu mola hatutakii magumu yenye uzito bali anatutakia yaliyo mepesi tu. huo ugumu na uzito wanaweka watu wenyewe! Ingia uislamu ujionee usisikilize propaganda za wasioutakia heri uislamu
Huwezi kutenganisha uislam na UGAIDI,kuua,chinja chinja nk
 
Back
Top Bottom