Ujanja wa Rais Samia kutumia mpira kujizolea kura huku ripoti muhimu ya CAG iliyojaa wala rushwa ipo kapuni

Ujanja wa Rais Samia kutumia mpira kujizolea kura huku ripoti muhimu ya CAG iliyojaa wala rushwa ipo kapuni

Mhhh umasikini wa taifa ufichwe na medali ya dhahabu ya mtu mmoja?
Hii ya leo kali [emoji22]
Umaskini upo dunia nzima na sababu zake zinajulikana na zinazidi kuongezeka kila kukicha.

Heshima ya michezo inatafutwa na inachangia katika kukuza umaarufu wa taifa zima.

Usaini Bolt unajua kapeleka watalii wangapi kwao Jamaica?.

Sergei Bubka unajua alilitangaza kwa kiasi gani taifa lake la Ukraine miaka ile ya nyuma?.

Vipi kuhusu Senegal na timu zao za taifa zenye makombe makubwa barani afrika, hakuna ushawishi wowote wanaoupata mawakala wao huko Ulaya kupitia heshima ya timu zao za Taifa?.
 
Hizi report za CAG zinatoka kila mwaka, kuna awamu gani imeshawahi kuwa na report safi kabisa?.

Acheni nongwa za kipumbavu watanzania.

Michezo ndio inayafanya mataifa kama Ivory Coast yawe na amani baada ya vita za miaka na miaka.

Michezo kwa maana ya medali za dhahabu na wakimbiaji wa mita mia ndio inauficha umaskini wa jumla wa Jamaica.

Michezo ni heshima ya taifa. Ni nchi yenye kujaa washamba pekee isiyoelewa maana na faida za michezo.

Kuhusu mkataba wa bandari nakushauri tafuta mada nyingine za kuumiza kichwa chako, hilo jambo ndio limeshapita.

Michezo pia inatumika na Serikali ya ccm kuwapumbaza Watanzania!
 
Hakuna report ya CAG inayokuja bila ya kuwa na wala rushwa ndani yake. Sisi tunaoandika uzi kama huu hatujawahi kupata nafasi ya kuwa na mamlaka katika taasisi wala wizara yoyote ile.

Nina uhakika tukipata nafasi hiyo tunageuka kuwa wala rushwa namba moja kabisa. Ni ugonjwa wa kitaifa tunaugua, tangu awamu zilizotangulia wapigaji wapo kila mahali.

JPM alijua kuonyesha umma kwamba yupo vitani dhidi ya walarushwa lakini haikumaanisha kwamba katika awamu yake hakuwa na walarushwa, alijaza jamaa zake kwenye halmashauri zote nchini wakatengeneza ufalme wao na wakawa wanapiga pesa nyingi tu za umma.

Samia anaitendea haki michezo, atakuwa amekutana na washauri wazuri wa masuala haya kwani wameweza kumuonyesha muunganiko uliopo kati ya michezo na masuala ya kiuchumi.

Taifa la watu wazembe wasiopenda michezo ni taifa la watu mazezeta wenye akili zisizochangamka, ni taifa la watu wasengenyaji wenye kupenda udaku na mambo mepesi, ni taifa lenye watu wasio na ubunifu.
 
Michezo pia inatumika na Serikali ya ccm kuwapumbaza Watanzania!
Kupumbaza ni kwa mujibu wa maana zetu wenyewe. Anatimiza wajibu kila anapotoa milioni tano au kumi kwa timu inayoshinda mechi ya kimataifa. Akiamua kuichunia michezo ni sisi tutakaokuwa wa kwanza kulaumu kwamba serikali inatumia kifisadi pesa zetu huku ikiwa imeisahau michezo.

Huwa nongwa zinatujaa siku zote.
 
Frankly speaking Samia hajui chochote kuhusu mpira!
Wewe ndo hujui chochote! Kama uko timamu kabisa huwezi kuzarau profile ya mtu kama SAMIA kuwa hajui chochote kuhusu mpira!
Yani hajui hata kuwa kuna refa?
Nonesense.


FT:SIMBA 1-5 YANGA
 
Hali ilivyo huko mitandaoni
IMG_20231106_130504.jpg
IMG_20231106_130418.jpg
IMG_20231106_130440.jpg
 
Back
Top Bottom