Ujasiri wa JWTZ katika kulinda! Apambana na Chatu

Ujasiri wa JWTZ katika kulinda! Apambana na Chatu

Hii ishu ya kuua nyara ilibarikiwa na viongozi wa juu.Mnakumbuka yule polisi aliua nyoka,akapewa hela?
 
Halikuwa tukio la kujisifu ila kwa vile amefanya mtu ambaye kazi yake ina asili ya kukutana na vikwazo vikubwa kama hivyo ni pongezi kwake kwa kuweza kuhakikisha adui anaanguka ila kiuhalisia alifaa aachane na chatu huyo aendelee na maisha yake.
Chatu hana msdhara yoyote,alitakiwa aachwe aendelee na maisha yake
 
Wote mliochangia negative mnaguswa na mafuta ya mwamposa...........ulitaka binadamu mwenzanko afe au?? Unajua gharama ya binadamu mpaka afikie rika Hilo?? Unajua kama ana familia au wazazi je ?? Bora kufa chatu roho yake amebaki nayo kwa ujenzi WA familia yake na taifa pia
 
Bado tunahitaji elimu sana kutunza wanyama wetu
America Mamba wanaingia mpaka swimming pools za watu ila wanapiga Simu kwenye mamlaka husika na wanakuja kuwaondoa
Hapo kuna wanyama wao na hata watoto wadogo
Na bunduki wanazo kila nyumba ila hawathubutu kuwauwa

Ni kosa la jinai kuuwa hawa wanyama
Kama hakuwa na madhara na ni porini ilikuwa amuache tu aendelee na mishe zake

Nimekutana na Chatu kama mara tatu kwa sehemu tofauti ila huwa nawaangalia mpaka wanakatisha bila kuwaza kuwauwa
Sio kuwajibishwa bali elimu inatakiwa sana
Kama wako vitani ni sawa hapo wamepata mboga ya uhakika
Ila sio haki yake kuuwa
 
Hehehe!! Elimu inapaswa kutolewa kwa askari wa JWTZ kwamba wanyama ni raslimali ya taifa na ukimkuta maporini usimuue, inapaswa uwaite wahusika waje wamkamate kwa kutumia mafunzo yao.
Kama angemkuta maeneo ya raia, hapo angekua na haki ya kumuua.
 
We wanakugusa masaburi! Jamaa anafanya ulinzi kwenye ranch za nguruwe ghafla akakutana na chatu na yeye yupo lindo! Sasa afanyeje amuachie akameze nguruwe ama ulitakaje
Apigie simu TAWA (Tanzania Wildlife Management Authority) Waje wamchukue chatu huyo, hivyo ndo sisi tumeelezwa kufanya, ukiona nyoka mkubwa usimuue, pigia simu kwa KWS au snake park waje wamchukue.
 
Mimi mwenyewe niliona video jana nikajisemea moyoni kwamba watanzania bado tuna safari ndefu sana. Huyo jamaa katika utumishi wake wote kaona hicho ndo kitendo kikubwa cha kujisifia bila kutambua alifanya uharifu na alipaswa apelekwe mahakamani,sheria za kulinda wanyama zipo. Cha kushangaza pia mamlaka ya usimamizi wa wanayamapori hakuna hatua watachukua. Vile vile yule chatu inaonekana alikuwa kwenye mawindo ya wanyama anaowamudu kuwameza, chatu ni mnyama mwenye akili sana, hawezi kuwinda windo linalomzidi au litakalomshinda kulimeza.
kwa ukubwa wa yule chatu anaweza kabisa kummeza mtu mwenye umbo kama la JB au Asha boko yule chatu ni mkubwa saana

pia askari kafanya kazi yake yeye jukumu lake lilikuwa ni kulinda mifugo ya jeshi(nguruwe) chatu alikuwa pale kuvizia nguruwe
 
Wapo

wengi zaidi ya huyo! Nyoka ana maeneo yake akiingilia hifadhi ya jeshi sio kwake mle
Lakini ukumbuke pia sisi binadamu ndo tunamaliza misitu kiasi cha kua wanyama hawana mahali salama pa kuishi tena ambapo watatoshelezeka na chakula...
 
Back
Top Bottom