Ujasiri wa JWTZ katika kulinda! Apambana na Chatu

Ujasiri wa JWTZ katika kulinda! Apambana na Chatu

Mimi sipingi kwamba ni hatari kwa nyoka huyo kua karibu na maeneo ya binadamu. (manake hata mtoto chini ya miaka 15 anawezwa kumezwa mzima mzima na chatu mkubwa kama huyo alieuliwa)

Kama ingekua nyoka huyo alimshambulia huyo askari na katika hali ya kupambana naye, askari akamuua, pia hio ninge support manake ile inaitwa self-defense ambayo inaruhusiwa, yani maisha yako au ya binadamu mwengine yalikua hatarini kwahivyo ulikua unatetea maisha yako ndo uka muua... Hata kwa binadamu hio inaruhusiwa, binadamu mwengine akikushambulia na silaha unaruhusiwa kummaliza na kutetea maisha yako yakiwa hatarini.

Lakini alichofanya huyu mwanajeshi si hivyo, Yeye alimuona nyoka kabla ashambuliwe kwahivyo hakua hatarini, alikua na mda wa kumchezea chezea nyoka kwa kumshika kwa mkia, kwenda kuchukua mkuki, mkuki ulipokua hautoshi akarudi tena na kuchukua panga ili aje ammalize, mda huu wote angeutumia kupigia simu, Tanzania Wildlife Management Authority (TAWA) waje wachukue kiumbe hichi ambacho hakina haitia yeyote....
mbona koboko wakimuona maporini wana nyuti?
 
Tunataka ushuhuda wa huyo comando kuua koboko, chatu hata awe na ukubwa wa anaconda bado haipendezi kujichukua ujiko kwasababu sote tunajua ni mzembe

Tunataka action ya koboko
Koboko unaweza kumuua kwa kumtumia honey Burger au nguchiro halafu wewe unajificha mbali unaangalia mpambano
 
Nilikua napitapita kule YouTube nilipokutana na hii vidio ilio nishtua sana, eti mwanajeshi kaua chatu kwa "mikono yake" miwili (Ingawaje hapo akijieleza anasema alitumia mkuki na pia panga).....

Kilichonishtua ni jinsi vile media ya jeshi ilirukia na kuingia kazini eti kutoa taarifa kana kwamba kitendo kilichofanyika ni cha kusifia au hata cha kuonyeshwa kwa mitandao, Tena kwenye hio video naona hata kamanda wa cheo cha juu ako hapo anaruhusu ahojiwe......

Chatu mkubwa kama vile hafai kuuliwa, unajua amechukua mda gani kua mkubwa kama vile? mnyama kama huyu ni kivutio kikubwa sana cha utalii, anaweza akaleta mapato makubwa sana akiwekwa kwa snake park.. Inakuaje mlinda amani kama huyu ndo anaongoza kwa kumaliza raslimali na kivutio kizuri kama hichi? Tena anachapishwa kwa video eti sifa........ Hizi s zile enzi za 1950's ambapo wanyamapori walikua wengi kuliko binadamu, hata wamasaai waliacha mila za kuua simba eti ndo waonyeshe ujasiri wa kubalehe kwasababu ya kulinda mazingira na kusupport sector ya utalii.

Huyu askari anafaa ashikwe na kushtakiwa, huu ni ushamba wa hali ya juu, kama kazi yake ya kulinda kambi imemboesha, mpelekeni msumbiji kule kabo-delgado akapambane na magaidi .
View attachment 1849529
Hivi Chatu ni hatari kiasi cha kujisifia kumuua?
 
Koboko unaweza kumuua kwa kumtumia honey Burger au nguchiro halafu wewe unajificha mbali unaangalia mpambano
sasa hapo unakua hujaua wewe japo uki force mbele ya camera point tatu unaweza ukapewa
 
Nilikua napitapita kule YouTube nilipokutana na hii vidio ilio nishtua sana, eti mwanajeshi kaua chatu kwa "mikono yake" miwili (Ingawaje hapo akijieleza anasema alitumia mkuki na pia panga).....

Kilichonishtua ni jinsi vile media ya jeshi ilirukia na kuingia kazini eti kutoa taarifa kana kwamba kitendo kilichofanyika ni cha kusifia au hata cha kuonyeshwa kwa mitandao, Tena kwenye hio video naona hata kamanda wa cheo cha juu ako hapo anaruhusu ahojiwe......

Chatu mkubwa kama vile hafai kuuliwa, unajua amechukua mda gani kua mkubwa kama vile? mnyama kama huyu ni kivutio kikubwa sana cha utalii, anaweza akaleta mapato makubwa sana akiwekwa kwa snake park.. Inakuaje mlinda amani kama huyu ndo anaongoza kwa kumaliza raslimali na kivutio kizuri kama hichi? Tena anachapishwa kwa video eti sifa........ Hizi s zile enzi za 1950's ambapo wanyamapori walikua wengi kuliko binadamu, hata wamasaai waliacha mila za kuua simba eti ndo waonyeshe ujasiri wa kubalehe kwasababu ya kulinda mazingira na kusupport sector ya utalii.

Huyu askari anafaa ashikwe na kushtakiwa, huu ni ushamba wa hali ya juu, kama kazi yake ya kulinda kambi imemboesha, mpelekeni msumbiji kule kabo-delgado akapambane na magaidi .
View attachment 1849529
Ruvu wanajihusisha na Ufugaji wa Kuku

Hivo Chatu wengi mara kwa mara, hujisogeza pale kutafuta mawindo.

Askari kaonyesha uthubutu, kwa tunaowajua Chatu, Huyu jamaa ni mwamba.

Vivutio tunavyo vingi Tanzania, vingi mnoooo vya kusaza.
 
We wanakugusa masaburi! Jamaa anafanya ulinzi kwenye ranch za nguruwe ghafla akakutana na chatu na yeye yupo lindo! Sasa afanyeje amuachie akameze nguruwe ama ulitakaje
Ahahah kumbe Mzee Baba unatukanaga..wanamguda masaburi [emoji16]
 
Hehehe!! Elimu inapaswa kutolewa kwa askari wa JWTZ kwamba wanyama ni raslimali ya taifa na ukimkuta maporini usimuue, inapaswa uwaite wahusika waje wamkamate kwa kutumia mafunzo yao.
Kama angemkuta maeneo ya raia, hapo angekua na haki ya kumuua.
Mkuu huyo aakaribalikuwa anafanya ulinzi kwenye ranch ya nguruwe,Kwa hiyo unaweza kuelewa huyo nyoka alikuja hapo kutafuta nn hapo

Ilikuwa hakuna jinsi Tu Bali kukabiliana nae na kumuua
 
Huyo chatu yeye angeenda mbugani kuwinda sio kuwinda vitoweo vya jeshi! Watu wanafuga nguruwe walishe jeshi huyu boya anajifanya anawinda bandani[emoji28][emoji28][emoji28]
Comments zako kwenye huu Uzi zinachekesha sn asee

Eti anajifanya kuwinda bandani badala akawinde porini

Chati anatafuta mseleleko[emoji1787]
 
Kwa hiyo huyo chatu angekamata kruta au mnyama pale zizini ni fresh maana ni kivutio.
Kumbuka huyo askari tayari huyo chatu kaingia 18 za askari ambae yuko kwenye kitengo chake cha kazi.
Laiti huyo chatu angechukua nguruwe huenda huyo askari kibarua kingeota nyasi.
Kijeshi ukiwa kitengo chako cha kazi kama ulinzi hata aje mkuu wa kambi unaruhusiwa kumshurutisha .

Sent using Jamii Forums mobile app
Chatu ni mnyama mwerevu sana, Hangeweza kushambulia hao nguruwe baada ya kujua kuna binadamu amemuona hapo karibu. (Labda kama huyo askari angempata chatu tayari ashamuua nguruwe na ako katika hali ya kummeza ndo hangeachilia chakula chake)
Chatu akishajua ameonekana na binadamu hua attention yote iko kwa binadamu maana anajua akisleki kidogo atauliwa. Infact, nyoka wote hua wako hivyo, wakishajua wameonekana na binadamu hua ni kukimbia au kujitetea maisha yake.
Mimi binafsi nimeshawahi kuona black mamba mkubwa sana karibia mita tatu, bahati nzuri alikua ashaniona na alikua anakwepa kwahivyo sikumfikia karibu kiasi cha kumtishia maisha yake kwa kumkanyaga bila kukusudia manake hapo angeniuma.... nilimfwata nyuma pole pole tu hadi akaingia kwa shimo flani, nikawapigia jamaa wa snake park inayopatikana karibu na kwetu wakaja waka ng'ang'ana hadi akatoka kwa shimo na wakamshika. Baada ya kama wiki moja jamaa huyo wa snake park akaja akanitafuta na kunipa Ksh.500, akaniambia huko snake park anakofanya kazi hua wanalipwa commision kulingana na ukali wa sumu au urefu wa nyoka watakaofanyikiwa kushika jangwani, akasema yeye alilipwa 3,400 kwa kumshika nyoka huyo kwahivyo hio 500 ni asante yake kwa kupiga simu.... Nikajua kumbe kuna faida kupiga simu!

Anyway, nilipomuuliza zaidi kuhusu huo ukali wa sumu akanieleza kua hapo snake park kazi yao ni ku extract sumu ya nyoka alafu wanaweka kwa package na kutuma South Africa, Ikifika huko sumu hio inadungwa kwa farasi ambao wanatengeneza anti-dote amabayo inatolewa kwa damu ya hao farasi kwenye maabara na wanasayansi wenye ujuzi huo alafu anti-dote hio ikirudi Kenya hua inauzwa gali sana kwahivyo hio industry ya kutengeneza tiba ya sumu za nyoka ni very exclusive na very profitable, kwahivyo nyoka wenye sumu kali si kivutio cha utalii tu bali ni industry ya kutengeneza tiba za kuumwa na nyoka lakini sisi Kenya na EAC kwa ujumla tunaichezea manake duniania kote kunaukosefu wa anti-dote za nyoka ilhali sisi tuko na nyoka wengi hatari kazi yetu kuua tu!
 
Comments zako kwenye huu Uzi zinachekesha sn asee

Eti anajifanya kuwinda bandani badala akawinde porini

Chati anatafuta mseleleko[emoji1787]
Chatu kazingua man, analeta janja janja ya nyani kujifanya ana survey karibu na banda 😅😅😅
 
Kweli kabisa hata mm nimeshangaa sana!!
ukimsikiliza jamaa alikuwa na nia ya kumuua chatu!!!??huu ni upunguani.....
angepiga simu mamlaka husika wanyama pori....
waje wachukue chatu wao.....
hawajui kwamba hiyo ni tuzo ya utalii!!??
Wanajeshi wanakula sana nyama pori. Hawawezi kuita mali asili
 
Mimi mwenyewe niliona video jana nikajisemea moyoni kwamba watanzania bado tuna safari ndefu sana. Huyo jamaa katika utumishi wake wote kaona hicho ndo kitendo kikubwa cha kujisifia bila kutambua alifanya uharifu na alipaswa apelekwe mahakamani,sheria za kulinda wanyama zipo. Cha kushangaza pia mamlaka ya usimamizi wa wanayamapori hakuna hatua watachukua. Vile vile yule chatu inaonekana alikuwa kwenye mawindo ya wanyama anaowamudu kuwameza, chatu ni mnyama mwenye akili sana, hawezi kuwinda windo linalomzidi au litakalomshinda kulimeza.
Chatu alikuwa mazingira ya kazi ya jamaa. Na vipi hao askari wa wanyama pori wangefika na kukuta chatu ametoweka ?. Hivi unadhani ni kazi rahisi askari wa wanyama pori kuingia kambi ya jeshi ?
 
Huyo Chatu alieuwawa na huyo mwanajeshi ni mnono kuliko huyo wa Nigeria alie meza ndama mzima! KWahivyo itabidi hao nguruwe wahesabiwe vizuri manake huyo chatu wa TZ alikua mkubwa hivyo kwa kula nini mda huu wote??

1626005605140.png

1626005647871.png

1626005717420.png

1626005737637.png

Back
Top Bottom