Ujasusi na uongozi: Mafanikio ya rais Putin katika kuirejesha tena Urusi

Kwenye technology ya kijeshi yupo vizuri labda heavy industries.Mkuu ebu angalia National interest ya think tank ya wamerekani wanavyo sifia Russia na wanafanya comparison na wao itakuwa mbongo kama wewe unasema usichokijua!
 
makonda give me a break! jamaa kasoma muccobs sidhan tiss wanachukua watu kwenye taasis za watu wenye uwezo mdogo kitaaluma kama muccobs
 
Nimekusoma mkuu
 
Kuweka kumbukumbu vizuri..makonda siyo TISS
 
Hivi hujaacha tu kuvua via mambo, type ushahidi wa hayo uliyoandika.,
 
sawa mkuu

Kuweka kumbukumbu vizuri..makonda siyo TISS


makonda give me a break! jamaa kasoma muccobs sidhan tiss wanachukua watu kwenye taasis za watu wenye uwezo mdogo kitaaluma kama muccobs

Hamjui mnaloliongea, Hivi kwa mawazo yenu Makonda kaibuka tuu from no where mpaka kupewa ukuu wa wilaya, tena kinondoni, and now Ukuu wa mkoa. Hivi unajua what it takes mtu kuwa kiongozi wa ulinzi na usalama wa mkoa.?
 
Safi sana Malcom Lumumba kwa uchambuzi yakinifu.

hakika "The Peoples' Friendship University of Russia" watakuwa proud of you.
 

Pamoja sana mkuu!
 
MSEZA MKULU njoo utie neno huku mkuu!
Mkuu nakushukuru sana kwa bandiko hili lenye uzito mkubwa.
Ujasusi chanya Kwa taifa unaweza kulisaidia kufanikiwa katika nyanja zote za kimaisha.
Kitabu cha art of War Cha General anayesadikika kuwa wa kichina Sun TZU kinaeleza kwa undani kuwa ushindi wowote ambao ni bora ni ule unaopatikana bila jasho na kwa mbinu. Hizi mbinu ndio zinaingia katika kipengele cha ujasusi chanya, Yaani kukusanya taarifa sahihi na kuzitumia kwa wakati katika kuleta tija kwa taifa. Nakumbuka unajua hata wewe enzi za wakina Lincoln hata US ujasusi ulikuwa umejikita kwenye mambo ya kiuchumi zaidi na Secret services zilikua chini ya Treasury haya yote yalitokea katka kujitanua kimataifa.

Ukisoma kitabu cha HESABU 13. Ujasusi ulitumika kugundua wanchotazamia kukigombania waisrael (Nchi ya KAanani) kuna faida au la. Japo kati ya majasusi 10 wanane walikuwa na mwelekeo hasi na kutoa taarifa za kifitini na za kukatisha tamaa kwa exageration. Kama RUSSIA walivyokabidhi PUTIN Israel walimkabidhi hiyo kazi YOSHUA (JASUSI) mwana wa NUNI kuivusha nchi kwenda kwenye mafanikio ya KIUCHUMI,KIJESHI,KIMBINU na KISIASA. Kama Haitoshi ni Majasusi watatu waliotumwa Yeriko na kuleta habari kuwa Pamoja na Uimara wa Yeriko wanawaogopa Israel kuliko kawaida (Huu ukawa mtaji wa ushindi wa YOSHUA kwa jeshi dogo).

Naamini PUTIN anapokuwa Rais wa RUSSIA anaingia sio kama Obama au Trump bali yeye yuko informed kuliko hata nadhani rais mchaguliwa wa US kuhusu dunia. Anaingia akiwa na Information za kiintelligensia nyingi kuhusu dunia ulaya na Us kuliko mtu yoyote. Taarifa kama hzi zinamsaidia Kiongozi mkuu kufanya informed decision na kutokudanganywa kirahisi. Angekuwa mtu wa kukurupuka Ishu ya Balozi kupigwa risasi ingezua WW3.

Naungana na wewe mkuu, Kiongozi mkuu akiwa anaamini na Uzoefu wa intrllijensia chanya na ameshiriki katika misukosuko hiyo anakuwa na EDGE zaidi ya yule anayesubiri kuambiwa kila kitu japo sio sawa wakati wote. Kwa ufupi anakuwa na macho ya ziada na hii inakuwa na faida zaidi kama akiwa na Uzalendo na Leadership qualities za kulivusha taifa.

Maelezo yako yale marefu mkuu yanatoa changamoto kufukua zaidi magombo ya dunia.
Kuna wengine wanazungumzia Power balance inatengenezwa na vyama vya siri(Secret Societies) kwa mipango yao. Mada nzuri mkuu
 
Urusi amepeleka jeshi lake siria tu anahangaika, mwenzake marekani yupo na amsha amsha karibu nchi sita lkn mambo hayayumbi

Meli ya kubeba ndege za kivita kujaza mafuta ilikuwa shughuli, syria wa mesha anza kuwithdraw majeshi yao. Huyo jasusi anayesifiwa hapa ndio anastuka sasa kuwa syria alivishwa mkenge. Unawekewa vikwazo vya kiuchumi kuna nini cha kujivunia hapo katika ubabe wa dunia hii? Brics imefia wapi?


Na washawasha!
 
Mkuu usitumie sana nguvu karne hii ya 21 bali tumia AKILI, kama mrusi kaweza ingiilia mifumo ya usa mara kibao basi anafahamu nini aliwazalo mmarekani na hapo ni ku deal na line of weakness tuu.
Nadhani wamarekani wamejua hilo la kuingilia uchaguzi tu,sijui kama wanajua kama wameingilia kuhusu mambo yao ya silaha,teknolojia na mengineyo,wako na snowden pale,mchawi wa haya mambo
 
Nikichukua mawazo yako,nikalinganisha na huyu wa kwetu,kwa kweli kuna haja ya kuwa na mtu wa kufanya well informed decisions
 
Hivi Russia wana aircraft carrier ngapi vile?
 
Utasikia: tunataka tuwe na uchumi imara kuizidi marekani, ndio maana hatuwataki wanasiasa. Hahaha
 
Mnamkumbuka Huyu?
 

Attachments

  • 800px-Mikhail_Gorbachev_-_May_2010.jpg
    53.6 KB · Views: 127
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…