Ujasusi na uongozi: Mafanikio ya rais Putin katika kuirejesha tena Urusi

Ujasusi na uongozi: Mafanikio ya rais Putin katika kuirejesha tena Urusi

Putin na Urusi wamefanikiwa sana kwenye kurudi kwenye siasa za dunia ila kwenye uchumi na technology bado sana. Putin kwa kuwadhibiti wapinzani wake na media amefanikiwa kuilisha dunia propaganda kuwa kila kitu kiko sawa kinyume na ukweli wenyewe.

Hata kijeshi nguvu za Urusi hazipo kwenye sophisticate military welfare bado anaamini katika jeshi lenye watu wengi wenye ujuzi duni. Mataifa mengi yaliyoendelea wanawekeza pesa nyingi kwenye R & D ya silaha na teknolojia za kivita za hali ya juu, hii ni pamoja na kuendesha vita kwa staili nyinginezo zikiwamo za kucontrol mind za wengine na silaha nyingine za kuathiri mienendo ya kibinadamu.

Kiuchumi hatuhitaji kuzungumza sana Urusi ana hali mbaya kupita maelezo. Unavyoona duniani watu wanarace kupigania rasilimali Afrika na kwingineko halafu yeye katulia si kwamba ameridhika na pesa, hana pesa ya kuwekeza huku.

Move mbovu aliyofanya ni kuweaken private sector nje ya Gazprom uwezo wa kufanya uwekezaji wa maana nje ya Urusi hana.
Kwenye technology ya kijeshi yupo vizuri labda heavy industries.Mkuu ebu angalia National interest ya think tank ya wamerekani wanavyo sifia Russia na wanafanya comparison na wao itakuwa mbongo kama wewe unasema usichokijua!
 
Ni kweli kabisa ujasusi ni muhimu katika uongozi.lkn ndugu yangu nikwambie tu hawa wengi unaowaona kuwa ni viongozi wengi wanatokea tiss mfano h.polepole ni mtu wa tiss totally p.makonda kadhalika.shida ni vipaumbele vyao wanawaza watawale ili watajirike lkn si kwa manufaa ya nchi.yapo mengi kwa leo inatosha.
makonda give me a break! jamaa kasoma muccobs sidhan tiss wanachukua watu kwenye taasis za watu wenye uwezo mdogo kitaaluma kama muccobs
 
Mkuu herikipaji ,
Mosi, Umesoma vitabu vya UFUNUO WA YOHANA, NABII ISAYA, NABII DANIELI na NABII EZEKIELI?
Majibu yako haya yote utayapata humo ndani ni kwanini Urusi imeinuka kutoka mavumbini hadi kufika hapa leo.
Unaweza kudharau haya ninayosema lakini huu ndiyo ukweli na wala haukimbiliki; wachambuzi wa masuala ya ulinzi hawawezi kukubali hadharani lakini usiku kucha wanashinda wakisoma Utabiri wa NOSTRADAMUS, MAYANS na BIBLIA.

Pili, Sidhani kama Ujasusi wa Vladmir Putin ndiyo umeifanya Urusi kufika hapo ilipofika leo.
Urusi tokea mwaka 1982-1984 ilishawahi kutawaliwa na Yuri Andropov ambaye alikuwa bosi wa K.G.B kwa miaka 15 lakini bado hali ya nchi ilikuwa mbaya sana hasa kwenye Uchumi.
Mathalani, George Bush alishawahi kuwa Jasusi mkubwa (MKURUGENZI MKUU) katika idara ya C.I.A lakini alitawala kwa miaka 4 na utawala wake una historia ya kuwa na sera mbovu sana nchini humo.

Deng Xiaoping hana historia yoyote ya Ujasusi lakini utawala wake tokea mwaka 1978-1989 ndiyo umeifanya nchi ya Uchina kuwa na:
-Mfumo Imara wa Soko la kimataifa,
-Mfumo Imara wa kiuchumi,
-Mfumo Imara wa Siasa ya Chama Kimoja,
-Mfumo Imara na mitaala bora kabisa ya Elimu na
-Mifumo Imara ya Kiulinzi na Usalama (Kuanzia Ujasusi, Ulinzi wa mipaka, Ulinzi wa tamaduni na Udhibiti mzuri wa mali za Ummah)

Japo Majasusi wengi wana nafasi kubwa ya kuwa viongozi wazuri kwenye nchi endapo tu akiwa na kipawa na vinasaba vya Uongozi thabiti.

Tatu, Uongozi wa Vladmir Putin umekuwa na mafanikio makubwa sana na wenye urahisi kwasababu ya mifumo iliyojengwa na watawala wa Urusi kabla yake. Kwenye suala zima la Sayansi na Teknolojia Putin amekuta Urusi imeendelea sana, yeye kazi yake ilikuwa ni kusimamia na kuendeleza kwa uthabiti. Makampuni karibia yote makubwa ya Urusi Vladmir Putin ameyakuta yameshaanzishwa, mfano mzuri:

- Gazprom (Kampuni kubwa la mafuta Urusi) limeanzishwa mwaka 1989 kwenye utawala wa Mikhail Gorbachev.
- Rosneft (Kampuni la mafuta) limeanzishwa mwaka 1993 kwenye utawala wa Boris Yeltsin.
- Ularvagonzavod UVZ (Kampuni la mashine na silaha) limeanzishwa mwaka 1936 na Joseph Stalin.
- Tupolev TU (Kampuni la ndege) limeanzishwa mwaka 1922 kipindi cha Utawala ya Vladmir Lenin.
- JSC Kalashnikov Concern (Kampuni la silaha) limeanzishwa mwaka 1807 na mfalme Alexander.

Ukimsoma mwandishi maarufu duniani Milan Kundera kwenye Riwaya lake la IGNORANCE anasema kwamba Urusi ni tofauti sana na mataifa ya kifashisti kwasababu mafanikio yake yameunganishwa na tamaduni yao, dini zao na historia yao. Hivyo tofauti na Ujerumani, Italia au Japan ambapo Ufashisti ulikufa mara tu baada ya viongozi kama Adolf Hitler, Benitho Mussolini na Hedaki Tojo kufariki.

Mfano mwingine hai kabisa ni nchi ya Marekani, ambapo Maraisi wengi wamefanikiwa kutokana na mifumo ambayo ilijengwa hata kabla wao hawajazaliwa au kuwepo Madarakani. Mfano Ronald Reagan ndiye raisi aliyefanikiwa sana kwenye historia ya Marekani tangu Vita ya Pili ya dunia kuisha mwaka 1945. Lakini vitu vyote vizuri alivikuta vimeshajengwa muda mrefu sana na yeye kazi yake ikawa ni kusimamia kwa kupitia sera yake ya REAGANOMICS, mfano mzuri tu:

  1. C.I.A ilikuwa na nguvu sana kipindi cha Ronald Reagan lakini ilianzishwa mwaka 1947 na raisi Harry S Truman.
  2. Mifumo bora kabisa ya Kiutawala hapa duniani (Demokrasia, Utawala wa Katiba na sheria, Uhuru wa mahakama na mgawanyo wa madaraka) alivikuta vimeanzishwa na wakina George Washington, Thomas Jefferson, James Monroe, John Adams na Benjamin Franklin kuanzia mwaka 1776 wanapata uhuru hadi mwaka 1787 wanaandika katiba.
  3. Nguvu kubwa ya kijeshi (Military Industrial Complex) imeanza kipindi cha utawala wa Franklin Delano Roosevelt 1933-1945 na kuendelea na Harry S Truman mpaka leo.
  4. Mifumo na Mitaala bora kabisa ya Elimu ameikuta (Vyuo kama Harvard, Yale na Stanford vilikuwepo) alichofanya ni kuborosha tu. Mwaka 1985 Marekani na Japan waliiga mtaala wa Elimu wa nchi ya Urusi ya Kisovieti na kuuboresha kuweza kukidhi mahitaji ya nchi zao.

Nne, Uzembe wa mataifa ya Magharibi yenyewe ndiyo yameifanya Urusi kurudi kwa nguvu. Wakati Urusi inakaribia kuanguka miaka ya themanini mwishoni na tisini mwanzoni kulikuwa na makubaliano baina ya Serikali ya Mikhaili Gorbachev na George Bush kwamba Urusi ingesitisha vita na kuzipa Uhuru nchi kama Poland, Latvia, Estonia na zinginezo ambazo zingependa kujitoa kwenye Jamhuri ya Kisovyeti. Lakini haya yangefanyika tu endapo umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi N.A.T.O hautajitanua tu hata kwa Inchi moja wala Sentimeta moja kuelekea Ulaya Mashariki kwenye nchi ambazo bado zina maslahi ya Urusi. Kwa bahati zaidi Mikhaili Gorbachev alikuwa akihudhuria kwenye vikao vya G7 mnamo siku za mwisho za Jamhuri ya Kisovieti na alikuwa akiomba mkopo kwa mataifa hayo ili kunusuru uchumi wa Urusi, lakini tofauti na Ufaransa hakuna taifa lililokubali kumpa mkopo wakati tayari alikuwa ameshakubali kufanya matakwa yao ya kuinganisha Ujerumani kwa Kuvunja Ukuta wa Berlin.

Utawala wa William Jefferson Clinton ulikiuka masharti na kuamua kufanya ubabe kwa kuanza kuitanua N.A.T.O kwa kasi kuielekea nchi ya Urusi ambayo ilikuwa imeshakubali kuweka silaha chini na kutafuta amani. Unakumbuka walivyoanza kuilipua YUGOSLAVIA ambayo kwenye Historia Warusi wanachukulia SLAVS kama ndugu zao wa damu; na kama wewe ni msomaji mzuri utakumbuka kwamba chanzo cha VITA YA KWANZA ya dunia ni pale ambapo URUSI hakukubali kuona UJERUMANI na AUSTRIA-HUNGARY wanaipa masharti nchi ya SERBIA. Mwaka 1914 AUSTRIA ilivyoitangazia vita SERBIA kwa kushindwa kuwapelekea wauaji wa Arch-Duke Ferdinand basi URUSI chini ya Mfalme Nicholas Ramanov waliitangazia vita Austria na yakatoe yalitokea mpaka mwaka 1917.

Lakini William Jefferson Clinton na Madeline Albright waliipuuza hii historia na kuanza kuvunja makubaliono waliyowahi kufanya na Gorbachev. Mwaka 1999 nchi za Czech, Poland na Hungary zikajiunga na N.A.T.O na watu wengi walililamika sana akiwemo Gorbachev na Boris Yeltsin lakini U.S.A wakawapuuza. Warusi walichukulia hili kama Usaliti hasahasa pale ambapo N.A.T.O miaka ya 1990's ikiongozwa na Marekani iliamua kufanya uvamizi dhidi ya Jamhuri za YUGOSLAVIA na kuanza kulipua KOSOVO ambayo ni sehemu yenye maslahi makubwa na Urusi pia ndiyo sehemu iliyomfanya Mrusi aingie kwenye Vita ya Kwanza ya dunia mwaka 1914. Hili jambo hado kijarida cha National Interest wanalaani kwa kusema kwamba haya yalikuwa ni makosa ya kiufundi kwa Utawala wa William, unaweza kujisomea mwenyewe hapa How Bill Clinton Made America More Ambitious—and Dangerous

George Bush Mdogo naye akandelea kufanya ujinga, kaitoa Marekani kwenye mkataba wa ABM (Anti-Ballistic Missile Treaty 1972) na kuamua kutengeneza makombora ya masafa Marefu. Walipoulizwa na Urusi kuhusu hili wakasema na nyinyi tengenezeni kama mnaweza sisi hatuna tatizo. Mwaka 2000 PENTAGON ilipeleka ripoti ya Uchambuzi wa Ulinzi kwa raisi George Bush kwamba serikali ya Urusi hasa jeshi lake lipo hoi, Nchi imechoka na rushwa, utawala mbovu, vita ya Chechenya na Ugaidi. Kama ikiendelea hivyo basi kufika mwaka 2004 Jeshi la Urusi na nchi inaweza isiwepo kabisa hapa duniani kwasababu itakuwa imeshasambaratika zaidi. Serikali ya Marekani wakiongozwa na Media zao wakayaamini haya na kuanza kujifanyia wanayotaka. Nyuma ya pazia Warusi wakaanza kujipanga na kuungana hasa hasa baada ya kujua kwamba Marekani anataka kuwafutilia mbali ya uso wa dunia.

George Bush baada ya kuona Urusi imeanza kuwa na nguvu, Vita za Afghanistani na Iraq zimeenda vibaya na wakati huo huo Uchina anachuana naye sana kibiashara akachanganyikiwa hadi mwaka 2004 bila hata kufikiria madhara yake, akaamua kuziingiza nchi saba zilizojirani na Urusi kwenye Umoja wa kujihami wa NATO. Marekani akavuta mipaka zaidi baada ya kusoge karibu kabisa na Urusi kupitia Georgia mwaka 2008 na tunakumbuka wote nini ambacho Vladmir Putin alimfanya Mikhail Sakhasvilli ambaye alikuwa raisi wa Georgia.

Mjaluo wetu Barack Obama huyo naye kaingia kichwa kichwa huko UKRAINE na SYRIA sehemu zenye maslahi makubwa ya Urusi. Kumbe hakujua kwamba anazidi kuwafanya Warusi wapate sababu ya kujijenga kijeshi mpaka leo hii Marekani inapigwa mikwara na Kremlin ova siyo taifa kubwa hapa duniani. Juzi Henry Kissinger kasema kama Marekani itataka kumshinda Uchina basi ni lazima iunde urafiki na Urusi, na hii ndiyo njia pekee (Hakuna njia mbadala). Hii inamaanisha hata Ujuio na sera za Donald Trump ni mipango ya wakubwa hapa duniani, maana ukiona mtu kama Henry Kissinger anasema Trump anaweza kuijenga Marekani basi Ujue la mgambo limelia.
Hivyo Vladmir Putin kufika hapa alipo pia Ujinga wa mataifa ya Ulaya umechangia kwa kiasi kukubwa Warusi wamuunge mkono Putin na kuona kama ni mwokozi wao kwa wakati kama huu.

Tano, Marekani anazidi kumfanya Vladmir Putin na Urusi wawe na nguvu ya zaidi ya hapa walipo kwasababu hana jinsi nyingine ya kumshinda Mchina isipokuwa kupitia ushawishi wa URUSI tu. Hili amelisema juzi Henry Kissinger ambapo alikiri kwamba ili Marekani iweze kufanikiwa kumthibiti Mchina mwenye nguvu kubwa ya kiuchumi hana jinsi zaidi ya kutumia ushawishi wa nchi ya Urusi. Alisema Donald Trump ni kiongozi ambaye dunia haijawahi kumuona na hivyo basi akijenga mahusiano mazuri na Moscow basi Uchina itapata shida sana kukua kijeshi.

Hii sera kwenye Sayansi ya Siasa inaitwa Divide et Impera ambapo taifa moja linawagawa mataifa mawili au zaidi na kusababisha chuki baina yao ili liwatawale vizuri. Imetumika sana hii sera hapa duniani hasa hasa kwetu Afrika kipindi cha Ukoloni au Ujerumani aliitumia hii sera sana kipindi cha Chancellor Otto Von Bismarck ambapo mataifa mengi yalipandikiziwa chuki ili yatawaliwe kirahisi na nchi ya Prussia ambayo ilikuja kuwa Ujerumani. Kibaya zaidi hii sera Henry Kissinger mwenyewe aliitumia kuwafarakanisha Warusi na Wachina kipindi cha Vita Baridi na bila Warusi kufikiria wakaingia mkenge na mwishowe sera ikazaa matunda mazuri sana. Mwaka 1960's Urusi alianza kuzozana na Uchina na hatimaye mwaka 1969 serikali ya Leonid Brezhnev ailifikiri hadi kutumia silaha za nyuklia dhidi ya Uchina, ambapo waliwauliza Wamarekani ambao walikuwa hawampendi Mchina kwamba tukimpiga Uchina ninyi msiingilie. Wamarekani wakakataa na kuamua kutumia mwanya kumvuta Uchina Upande wake ili kumzorotesha Urusi na Mwishowe kikatokea kitu kinachoitwa SINO-SOVIET SPLIT.

Mwaka 1972 raisi Richard Nixon akaenda hadi Uchina kutembelea Great Wall ambapo alifanya kikao na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Zhou Enlai pamoja na baadae raisi wa nchi hiyo Mao Zedong. Walikubaliana kuanza mikataba ya kibiashara na kufungua masoko yote hii kumkomoa Urusi. Ikumbukwe kipindi hiki sera maarufu ya Uchina moja ( ONE CHINA POLICY) ndiyo ilizaliwa. Ili kumkomoa Urusi serikali ya Marekani ikaamua kutambua kwamba Taiwan ni jimbo halali la Uchina japo linajitawala lenyewe. Ukikumbuka vizuri mwaka huo huo Uchina ilikuwa haina kiti katika baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa mataifa na hivyo Taiwan ndiyo ilikalia hicho kiti pamoja na kupewa kura ya VETO: Lakini mwaka huo kwa mara ya kwanza serikali ya Marekani ikaitambua serikali ya Kikomunisti ya Uchina kama Serikali halali ya nchi hiyo. Ghafla mwaka huo huo Uchina ikarudishwa kwenye Baraza la Ulinzi la Umoja wa Mataifa na kupewa kura ya VETO huku Taiwan ikitolewa. Marekani kamfungulia Masoko Uchina na kuanza kuwasomesha Wachina bure huku Wachina wakianza kukua kwa haraka sana kiuchumi.

Matokea ya hii sera Uchina akaanza kupingana na Urusi sehemu nyingi hapa duniani hadi kupelekea ushawishi wa Urusi kupungua kwa kasi hasa barani Afrika kuanzia miaka ya 1970. Mfano mzuri Uchina alimuunga mkono Muingereza nchini Angola dhidi ya taifa la Urusi na Cuba, kwenye kuvamia Afghanistani Wachina walikuwa upande wa Marekani kinyume kabisa na Urusi tofauti na ilivyokuwa kwenye vita ya Vietnam hivyo kupelekea Urusi kushindwa kujitanua kwa kasi. Mwisho wa haya ni kwamba Urusi ilididimia hadi kufika mwaka 1991 huku Uchina likikua kwa haraka sana. Sasa Marekani amekuwa mkubw na Ukomunisti na Jamhuri ya Kisovieti hazipo, adui mkubwa kwa Uchumi wa Marekani ni Uchina, hivyo basi kipindi hiki Henry Kissinger na wataalamu wengine wanapendekeza kwamba Watumia sera hiyo hiyo ya Divide et Impera na kutengeneza THE SECOND SINO-SOVIET SPLIT. Matokeo yake ni kwamba Urusi na lazima itakuwa na nguvu sana kwasababu Marekani hatampinga sana kwasababu Muungano wa Uchina na Urusi kutoke mwaka 2014-2016 umeleta madhara makubwa kwa Marekani hivyo ni bora hawa wasiwe wote. Donald Trump anawachuki sana Wachina na Kuwakumbatia Warusi, yote hii ni mikakati kwasababu naamini Wamarekani huwa wanafanya sana hesabu ya hatua zao hata kama ni za hovyo.

Putin na Urusi watazidi kuwa na nguvu sana kama sera za Trump na Kissinger zitaanza kutumika kuwagawanya hawa marafiki wawili. Japo sijajua sana kama Uchina wataachana na Urusi au lah, au kama Marekani anaweza kumshinda Mchina kwa hatua alipofika sasa. Lakini yote tisa Urusi akicheza karata yake vizuri anaweza kuwa anakula kotekote Washington na Beijing, hana cha kupoteza kabisa kwasababu mataifa yote haya (Marekani na Uchina) wanahitaji Ushawishi wa Moscow kumshinda mwenzake.

Mwaka 2017-2020 tutaona mengi sana ya Vladmir Putin.......
Huu ni mtazamo tu Mkuu..............

CC: Red Giant, Consigliere , Bukyanagandi , MSEZA MKULU , Dotworld , mchambawima1 , maalimu shewedy , kui , Chief , SirChief , mshana jr , Infantry Soldier , Richard , mngony , py thon , Apollo , Koba , big gift , Bavaria , Daudi Mchambuzi , Mabs , cognition, asigwa
Nimekusoma mkuu
 
Ni kweli kabisa ujasusi ni muhimu katika uongozi.lkn ndugu yangu nikwambie tu hawa wengi unaowaona kuwa ni viongozi wengi wanatokea tiss mfano h.polepole ni mtu wa tiss totally p.makonda kadhalika.shida ni vipaumbele vyao wanawaza watawale ili watajirike lkn si kwa manufaa ya nchi.yapo mengi kwa leo inatosha.
Kuweka kumbukumbu vizuri..makonda siyo TISS
 
Ni kweli kabisa ujasusi ni muhimu katika uongozi.lkn ndugu yangu nikwambie tu hawa wengi unaowaona kuwa ni viongozi wengi wanatokea tiss mfano h.polepole ni mtu wa tiss totally p.makonda kadhalika.shida ni vipaumbele vyao wanawaza watawale ili watajirike lkn si kwa manufaa ya nchi.yapo mengi kwa leo inatosha.
Hivi hujaacha tu kuvua via mambo, type ushahidi wa hayo uliyoandika.,
 
sawa mkuu

Kuweka kumbukumbu vizuri..makonda siyo TISS


makonda give me a break! jamaa kasoma muccobs sidhan tiss wanachukua watu kwenye taasis za watu wenye uwezo mdogo kitaaluma kama muccobs

Hamjui mnaloliongea, Hivi kwa mawazo yenu Makonda kaibuka tuu from no where mpaka kupewa ukuu wa wilaya, tena kinondoni, and now Ukuu wa mkoa. Hivi unajua what it takes mtu kuwa kiongozi wa ulinzi na usalama wa mkoa.?
 
Safi sana Malcom Lumumba kwa uchambuzi yakinifu.

hakika "The Peoples' Friendship University of Russia" watakuwa proud of you.
 
View attachment 456662
Rais Putin wa Urusi

Umetoa elimu kubwa na nzuri MALCOM LUMUMBA na hakika yapo mengi ya kujifunza kwenye uchambuzi wako huu.


Tuzidi kuangalia sera mpya za Trump zitaleta impact ipi kwenye hizi geopolitics duniani maana mie huwa namuona Trump kama mtu asiyekuwa na misimamo vile yani anabadilika badilika sana.

Nitazidi kuvisoma hivyo vitabu vya biblia nitafakari zaidi mkuu.

Pamoja sana mkuu!
 
MSEZA MKULU njoo utie neno huku mkuu!
Mkuu nakushukuru sana kwa bandiko hili lenye uzito mkubwa.
Ujasusi chanya Kwa taifa unaweza kulisaidia kufanikiwa katika nyanja zote za kimaisha.
Kitabu cha art of War Cha General anayesadikika kuwa wa kichina Sun TZU kinaeleza kwa undani kuwa ushindi wowote ambao ni bora ni ule unaopatikana bila jasho na kwa mbinu. Hizi mbinu ndio zinaingia katika kipengele cha ujasusi chanya, Yaani kukusanya taarifa sahihi na kuzitumia kwa wakati katika kuleta tija kwa taifa. Nakumbuka unajua hata wewe enzi za wakina Lincoln hata US ujasusi ulikuwa umejikita kwenye mambo ya kiuchumi zaidi na Secret services zilikua chini ya Treasury haya yote yalitokea katka kujitanua kimataifa.

Ukisoma kitabu cha HESABU 13. Ujasusi ulitumika kugundua wanchotazamia kukigombania waisrael (Nchi ya KAanani) kuna faida au la. Japo kati ya majasusi 10 wanane walikuwa na mwelekeo hasi na kutoa taarifa za kifitini na za kukatisha tamaa kwa exageration. Kama RUSSIA walivyokabidhi PUTIN Israel walimkabidhi hiyo kazi YOSHUA (JASUSI) mwana wa NUNI kuivusha nchi kwenda kwenye mafanikio ya KIUCHUMI,KIJESHI,KIMBINU na KISIASA. Kama Haitoshi ni Majasusi watatu waliotumwa Yeriko na kuleta habari kuwa Pamoja na Uimara wa Yeriko wanawaogopa Israel kuliko kawaida (Huu ukawa mtaji wa ushindi wa YOSHUA kwa jeshi dogo).

Naamini PUTIN anapokuwa Rais wa RUSSIA anaingia sio kama Obama au Trump bali yeye yuko informed kuliko hata nadhani rais mchaguliwa wa US kuhusu dunia. Anaingia akiwa na Information za kiintelligensia nyingi kuhusu dunia ulaya na Us kuliko mtu yoyote. Taarifa kama hzi zinamsaidia Kiongozi mkuu kufanya informed decision na kutokudanganywa kirahisi. Angekuwa mtu wa kukurupuka Ishu ya Balozi kupigwa risasi ingezua WW3.

Naungana na wewe mkuu, Kiongozi mkuu akiwa anaamini na Uzoefu wa intrllijensia chanya na ameshiriki katika misukosuko hiyo anakuwa na EDGE zaidi ya yule anayesubiri kuambiwa kila kitu japo sio sawa wakati wote. Kwa ufupi anakuwa na macho ya ziada na hii inakuwa na faida zaidi kama akiwa na Uzalendo na Leadership qualities za kulivusha taifa.

Maelezo yako yale marefu mkuu yanatoa changamoto kufukua zaidi magombo ya dunia.
Kuna wengine wanazungumzia Power balance inatengenezwa na vyama vya siri(Secret Societies) kwa mipango yao. Mada nzuri mkuu
 
Urusi amepeleka jeshi lake siria tu anahangaika, mwenzake marekani yupo na amsha amsha karibu nchi sita lkn mambo hayayumbi

Meli ya kubeba ndege za kivita kujaza mafuta ilikuwa shughuli, syria wa mesha anza kuwithdraw majeshi yao. Huyo jasusi anayesifiwa hapa ndio anastuka sasa kuwa syria alivishwa mkenge. Unawekewa vikwazo vya kiuchumi kuna nini cha kujivunia hapo katika ubabe wa dunia hii? Brics imefia wapi?


Na washawasha!
 
Mkuu usitumie sana nguvu karne hii ya 21 bali tumia AKILI, kama mrusi kaweza ingiilia mifumo ya usa mara kibao basi anafahamu nini aliwazalo mmarekani na hapo ni ku deal na line of weakness tuu.
Nadhani wamarekani wamejua hilo la kuingilia uchaguzi tu,sijui kama wanajua kama wameingilia kuhusu mambo yao ya silaha,teknolojia na mengineyo,wako na snowden pale,mchawi wa haya mambo
 
Mkuu nakushukuru sana kwa bandiko hili lenye uzito mkubwa.
Ujasusi chanya Kwa taifa unaweza kulisaidia kufanikiwa katika nyanja zote za kimaisha.
Kitabu cha art of War Cha General anayesadikika kuwa wa kichina Sun TZU kinaeleza kwa undani kuwa ushindi wowote ambao ni bora ni ule unaopatikana bila jasho na kwa mbinu. Hizi mbinu ndio zinaingia katika kipengele cha ujasusi chanya, Yaani kukusanya taarifa sahihi na kuzitumia kwa wakati katika kuleta tija kwa taifa. Nakumbuka unajua hata wewe enzi za wakina Lincoln hata US ujasusi ulikuwa umejikita kwenye mambo ya kiuchumi zaidi na Secret services zilikua chini ya Treasury haya yote yalitokea katka kujitanua kimataifa.

Ukisoma kitabu cha HESABU 13. Ujasusi ulitumika kugundua wanchotazamia kukigombania waisrael (Nchi ya KAanani) kuna faida au la. Japo kati ya majasusi 10 wanane walikuwa na mwelekeo hasi na kutoa taarifa za kifitini na za kukatisha tamaa kwa exageration. Kama RUSSIA walivyokabidhi PUTIN Israel walimkabidhi hiyo kazi YOSHUA (JASUSI) mwana wa NUNI kuivusha nchi kwenda kwenye mafanikio ya KIUCHUMI,KIJESHI,KIMBINU na KISIASA. Kama Haitoshi ni Majasusi watatu waliotumwa Yeriko na kuleta habari kuwa Pamoja na Uimara wa Yeriko wanawaogopa Israel kuliko kawaida (Huu ukawa mtaji wa ushindi wa YOSHUA kwa jeshi dogo).

Naamini PUTIN anapokuwa Rais wa RUSSIA anaingia sio kama Obama au Trump bali yeye yuko informed kuliko hata nadhani rais mchaguliwa wa US kuhusu dunia. Anaingia akiwa na Information za kiintelligensia nyingi kuhusu dunia ulaya na Us kuliko mtu yoyote. Taarifa kama hzi zinamsaidia Kiongozi mkuu kufanya informed decision na kutokudanganywa kirahisi. Angekuwa mtu wa kukurupuka Ishu ya Balozi kupigwa risasi ingezua WW3.

Naungana na wewe mkuu, Kiongozi mkuu akiwa anaamini na Uzoefu wa intrllijensia chanya na ameshiriki katika misukosuko hiyo anakuwa na EDGE zaidi ya yule anayesubiri kuambiwa kila kitu japo sio sawa wakati wote. Kwa ufupi anakuwa na macho ya ziada na hii inakuwa na faida zaidi kama akiwa na Uzalendo na Leadership qualities za kulivusha taifa.

Maelezo yako yale marefu mkuu yanatoa changamoto kufukua zaidi magombo ya dunia.
Kuna wengine wanazungumzia Power balance inatengenezwa na vyama vya siri(Secret Societies) kwa mipango yao. Mada nzuri mkuu
Nikichukua mawazo yako,nikalinganisha na huyu wa kwetu,kwa kweli kuna haja ya kuwa na mtu wa kufanya well informed decisions
 
Mkuu kwenye uchumi ni upo sawa hali ya Urusi sio nzuri sana kiuchumi lakini kwenye military tech hapa natofautiana nawewe.
Alichokifanya Putin na ndiyo kipaumbele chake ni millitary modernization hapa wamelifanya jeshi lao kuwa imara lenye uwezo mkubwa kuanzia majini, nchi kavu na angani.
wamefanya upgrade ya silaha zao submarines, heavy bomber&fighter jets, tanks, air defence systems.

Kama wangekuwa weak hata wasingeweza kurusha missiles kutoka umbali zaidi ya 2500 kms pale Caspian sea ile si kila nchi inaweza tena kwa kutumia light little warships.

Na lile tukio lina maana gani?
Walitaka kutuma ujumbe kuwa sasa Warusi wanaeza kushambulia na kufika kila kona ya dunia kwa urahisi zaidi kutoka Urusi hawana haja ya kujenga millitary base nyingi na hili linapunguza gharama na kujilinda zaidi na zaidi.
Pia asilimia kubwa ya tech ya wachina wanategemea Urusi yani China bila Urusi itatetereka pia.

Wamewekeza sana kwenye millitary tech sababu wanaamini maadui wao wameapa kuivamia na kuiangusha Urusi pale tu watapokuwa na uwezo huo.
Maadui hao wanashindwa kuivamia sababu tu wanaona hawatoeza ila kama Urusi wangekuwa hawana sophisticated millitary tech tungekuwa tunazungumza mengine hapa.
Hivi Russia wana aircraft carrier ngapi vile?
 
Utasikia: tunataka tuwe na uchumi imara kuizidi marekani, ndio maana hatuwataki wanasiasa. Hahaha
 
Mnamkumbuka Huyu?
 

Attachments

  • 800px-Mikhail_Gorbachev_-_May_2010.jpg
    800px-Mikhail_Gorbachev_-_May_2010.jpg
    53.6 KB · Views: 127
Back
Top Bottom