MSEZA MKULU njoo utie neno huku mkuu!
Mkuu nakushukuru sana kwa bandiko hili lenye uzito mkubwa.
Ujasusi chanya Kwa taifa unaweza kulisaidia kufanikiwa katika nyanja zote za kimaisha.
Kitabu cha art of War Cha General anayesadikika kuwa wa kichina Sun TZU kinaeleza kwa undani kuwa ushindi wowote ambao ni bora ni ule unaopatikana bila jasho na kwa mbinu. Hizi mbinu ndio zinaingia katika kipengele cha ujasusi chanya, Yaani kukusanya taarifa sahihi na kuzitumia kwa wakati katika kuleta tija kwa taifa. Nakumbuka unajua hata wewe enzi za wakina Lincoln hata US ujasusi ulikuwa umejikita kwenye mambo ya kiuchumi zaidi na Secret services zilikua chini ya Treasury haya yote yalitokea katka kujitanua kimataifa.
Ukisoma kitabu cha HESABU 13. Ujasusi ulitumika kugundua wanchotazamia kukigombania waisrael (Nchi ya KAanani) kuna faida au la. Japo kati ya majasusi 10 wanane walikuwa na mwelekeo hasi na kutoa taarifa za kifitini na za kukatisha tamaa kwa exageration. Kama RUSSIA walivyokabidhi PUTIN Israel walimkabidhi hiyo kazi YOSHUA (JASUSI) mwana wa NUNI kuivusha nchi kwenda kwenye mafanikio ya KIUCHUMI,KIJESHI,KIMBINU na KISIASA. Kama Haitoshi ni Majasusi watatu waliotumwa Yeriko na kuleta habari kuwa Pamoja na Uimara wa Yeriko wanawaogopa Israel kuliko kawaida (Huu ukawa mtaji wa ushindi wa YOSHUA kwa jeshi dogo).
Naamini PUTIN anapokuwa Rais wa RUSSIA anaingia sio kama Obama au Trump bali yeye yuko informed kuliko hata nadhani rais mchaguliwa wa US kuhusu dunia. Anaingia akiwa na Information za kiintelligensia nyingi kuhusu dunia ulaya na Us kuliko mtu yoyote. Taarifa kama hzi zinamsaidia Kiongozi mkuu kufanya informed decision na kutokudanganywa kirahisi. Angekuwa mtu wa kukurupuka Ishu ya Balozi kupigwa risasi ingezua WW3.
Naungana na wewe mkuu, Kiongozi mkuu akiwa anaamini na Uzoefu wa intrllijensia chanya na ameshiriki katika misukosuko hiyo anakuwa na EDGE zaidi ya yule anayesubiri kuambiwa kila kitu japo sio sawa wakati wote. Kwa ufupi anakuwa na macho ya ziada na hii inakuwa na faida zaidi kama akiwa na Uzalendo na Leadership qualities za kulivusha taifa.
Maelezo yako yale marefu mkuu yanatoa changamoto kufukua zaidi magombo ya dunia.
Kuna wengine wanazungumzia Power balance inatengenezwa na vyama vya siri(Secret Societies) kwa mipango yao. Mada nzuri mkuu