Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Hiyo nyumba haipungui 200mil ni mwendelezo wa kudharirishana na kuoneana tu.....
 
Hawa ndio waliomba tena bilioni 1 kwa ajili ya uzio wa nyumba zote 7!!
Gharama ya kujenga hiyo nyumba milioni 143 na gharama ya uzio milioni 143!!

Hawa wameonja asali. Sasa wanataka mzinga!!
 
kwa nini uandikie mate wakati wino upo,
nyumba ipo, nyaraka za manunuzi zipo, wathamini wapo, sasa kwa nn tubishane? wakati kazi ndogo tu hiyo! ita valuer atoa tathimini ili kieleweke
 
Mnajitetea siyo??? Kwa Magu, mtazitema, Hana mtoto wa njomba Yule, Rudisheni pesa zetu

kwa nini uandikie mate wakati wino upo,
nyumba ipo, nyaraka za manunuzi zipo, wathamini wapo, sasa kwa nn tubishane? wakati kazi ndogo tu hiyo! its valuer atoa tathimini ili kieleweke
[/QUOT
 
Hii nyumba Ni kubwa mno,
Tena inatakiwa kua mil 150+ Kama ukiamua kuitendea haki upande wa material

HEBU TUPIGE HESABU SASA[emoji116]

1. MSINGI
(Kusafisha kiwanja, Kuchimba msingi,KIFUSI, tofali,cement, mchanga, maji,kumwaga jamvi,ufundi,mengineyo)
Almost 10mil imekata.

2. Kuinua kuta
(Tofali, mchanga, maji, ufundi,mengineyo)
Almost 15 mil imekata

3. Kumwaga beam nondo 4 nyumba nzima
(Nondo,kokoto,mbao, misumari, maji,mchanga,cement,ufundi, mengineyo)
Almost 10 mil imekata

4. Kupinga kenchi(KUPAUA)
(Mbao,misumari,binding wire, ufundi,fisha bodi ,mengineyo)
Almost 5mil imekata

5. Kupiga bati (kuezeka)
(Bati geji 28 au 26, misumari, gundi, ufundi, mengineyo)
Almost 15mil imekata

BOMA LIMEISHA, ALMOST 45Mil IMESHAKATA

Finishing[emoji116]

6. Hizo dirisha (alminium+ Gril+rangi+mengineyo) zilizotandazwa apo usichukulie poa.
Kwa haraka haraka Ziko sio chini ya 15 apo@500,000.
Mpaka zinavoonekana apo Almost 8mil imekata

7.Bado milango (frem+Top+vitasa+rangi+ufundi, mengineyo)
Kwa haraka haraka haipungui milango 10 ilo jengo. Each 400,000.
Mpaka inavoonekana apo Almost 5mil imekata

8.Hizo tiles bila shaka Ni first grade (TAASISI),
zimetandazwa sakafuni mpaka ukutani.
Mpaka zinavoonekana (tiles,grout,strips,skating,ufundi,mengineyo) apo Almost 15mil imekata

9.Hujaja gharama ya lipu, (mchanga, cement, ufundi,maji,mengineyo)
almost 10 mil nje ndani imekata

10.skimming ya nyumba nzima nje ndani kwa white cement(Rangi, white cement,ufundi, mengineyo)
Almost 7mil imekata

11. Kupiga BANDARINGI kwa ajili ya gypsum bodi.
(Mbao,misumari,ufundi,mengineyo)
Almost 7mil imekata

12. Kupiga GYPSUM BOARD
(Gypsum bodi,skruu, faiba tepu,ufundi,mengineyo)
Almost 7 mil imekata

13. Kupiga RANGI NYUMBA NZIMA nje ndani
(Rangi,ufundi,mengineyo)
Almost 5 mil imekata

14. MFUMO WA UMEME (wayaringi)
Hapo lazima nyaya SINGLE CORE first grade zimetembea za kutosha, TRONIC switch,socket,m/switch,breaker,cutout, earthrod,conduit,boxes, process za KUOMBA MITA TANESCO,ufundi n.k.
Apo almost 10mil imekata

15. MFUMO WA MAJI
Nazungumzia vyooni,jikoni,bafuni na kwingineko.
(MaSink, tanki, mabomba, ufundi, mengineyo)
Almost 5mil lazima ikate.

16. SHIMO LA CHOO
(Kuchimba,tofali,cement,mchanga,nondo,kokoto, ufundi,waya meshi, mengineyo)
Almost 2mil imekata

FINISHING tu MPAKA HAPO, jumla 81mil IMESHAKATA.

Sasa ukijumlisha
Kujenga boma 45mil + finishing 81mil= jumla 126mil.

Unaweza kuongezea na 10 mil ya kupiga FINAL TOUCHES ili kunogesha zaidi nyumba.

Kama urembo kwenye nguzo, vibaraza mbalimbali, bustani, taa za urembo, mfumo wa CCTV camera, bango, n.k

ALMOST 136MILLION inakamilisha Ilo jengo.


My take:
SIDHANI KAMA Kuna upigaji hapa.
Na Kama upo Basi ni kwa kiwango kidogo Sana.

Tena inaweza kua kwa kwa vitu vidogo vidogoKama kulipana posho, overtime,chakula Cha saiti,usafiri n.k.

Vinaweza kukava icho kiwango kinachopelea (yaani 7million) kufikia icho kiwango halisi walichotaja Cha 143million.

Shukran [emoji120]
Kupiga bati mil 15??? Mmh wajinga ni wengi sana, au inawezekana wewe ndio mkandarasi
Tufanye imekula bati 100 na bati moja ni 40,000(bei kubwa sana hii) , inakuwa ni mil 4 tu, kwa hiyo hiyo mil 11 ni matumizi ya mbao na misumari??
 
Namuona kaka yangu D. N umesimamishwa Kazi dah

Ova
 
Watanzania tuache kukurupuka. M 143 sio nyingi kabisa . japo nyumba zetu tunajenga kimaskini tunahamia hata kwa kuweka mashuka ila ukichukua diary upige hesabu unakuta M 70 imeisha hata aluminium dirisha hujaweka. Mm binafsi naushuhuda zilinunuliwa tiles za M 17 zikawekwa kwenye ghetto la kawaida tu.
Tiles za mil 17 ziwekwe kwenye gheto la kawaida?? Hebu chukulia tu mfano wa makadiriaji ya juu sana yaani tuseme box moja ni 80000, hapo unapata maboksi 212. Maboksi 212 unaweka kwenye gheto la kawaida??? Huu utani sasa
 
Hebu lete mchanganuo wako mkuu.

Yaani
Hiyo hiyo mifuko 200 ya simenti ndo hiyo hiyo

-Ujengee msingi.
-umwagie jamvi
-uinulie kuta mpaka juu
-ujengee SHIMO la choo na kufunika na mfuniko wa zege
-umwage linta
-upige lipu
-upige rough floor
-ubandikie tiles sakafuni na ukutani kuanzia chooni,vyumbani mpaka kuta za nje.

AISEE,
HEBU KUA SIRIASI BASI MKUU [emoji851]
Mifuko 200 ni mingi sana kwenye hii nyumba. Tumejenga manyoni kwa ramani sawa na hii
 
Tufanye tunakubaliana na wewe, embu jaribu kutupigia 'rafu' tuone.

Ninavyojua ni kwamba, nenda chini,fukua msingi urefu utakavyo, laza tofari upendavyo, weka 'resho' unayoitamani hata ya karai15 kwa mfuko, hiyo nyumba haiwezi kumeza tofari zaidi ya 6000÷20×20,000/=? na mifuko 200×20'000/= ya kujengea pamoja na ripu, tufanye na 100 kwa ajili ya tiles jumla mifuko 600.

Weka bati hizo za migongo mipana 200×33,000/=?
Mbao za size mbalimbali hazizidi 500×12,000/=?
Hapa hatujapigia nondo na vifaa vingine vya msingi kwenye finishing, lakini tupo kwenye ishirini na,30haijakatika.

Embu isongeshe kwenye mchanga, nondo, tiles rangi,misumari, alluminium na grill, milango, wiring, gipsum uone kama inavuka70?
Gharama za ujenzi tunazikuza sana kwa nakusudi ajili ya aslahi binafsi ama kutokujua hadi tunaingia uoga na kupelekea watu kusalia hadi kufia 'mapangoni'
Bati 200?? Kuna watu hamna kabisa ubongo kwenye vichwa vyenu
 
Kuna mtu anaweza kujenga nyumba kwa milioni 50, mwingine nyumba ya aina hiyo hiyo akajenga kwa milioni 100 kutegemeana na quality ya material na ubora wa finishing. Mambo ya ujenzi hayapo uniform kihivyo, kisa mtu kajenga kwa milioni 20 basi atataka kushawishi kila mtu kwamba gharama ya ujenzi wa nyumba haiwezi kuvuka mil.20.
 
Mifuko 200 ni mingi sana kwenye hii nyumba. Tumejenga manyoni kwa ramani sawa na hii
Utakua fundi tu wewe.
Kwanza niambie tofali za kulaza mfuko mmoja wa cement unajenga tofali ngapi?
 
Sasa kwanini nyumba za serikali ndio zinaongoza kwa ubovu?
Si kweli, ubovu umeanza siku hizi walipobadili mfumo wa usimamiaji.
Kabla ya magufuli nyumba za serikali zilikuwa na ubora na usimamizi thabiti.
Sababu usimamiaji ulisimamiqa tofauti na wajenzi.
 
Kuna mtu anaweza kujenga nyumba kwa milioni 50, mwingine nyumba ya aina hiyo hiyo akajenga kwa milioni 100 kutegemeana na quality ya material na ubora wa finishing. Mambo ya ujenzi hayapo uniform kihivyo, kisa mtu kajenga kwa milioni 20 basi atataka kushawishi kila mtu kwamba gharama ya ujenzi wa nyumba haiwezi kuvuka mil.20.
Big Yes
 
Si kweli, ubovu umeanza siku hizi walipobadili mfumo wa usimamiaji.
Kabla ya magufuli nyumba za serikali zilikuwa na ubora na usimamizi thabiti.
Sababu usimamiaji ulisimamiqa tofauti na wajenzi.
ndio maana mnashauriwa kuwa wasikikizaji zaidi.
 
Hivi kwanini wanasiasa wa bongo wanajitia kujua kila kitu hata vile ambavyo viko nje ya taaluma yao? Gharama za ujenzi ziko juu na mtu huwezi kutoa makadirio kwa kuangalia tu.
By the way, nani anajua gharama harisi za kununua madege ya atcl?
magufuli ni zaidi ya mwanasiasa mkuu,

amekaa wizara ya ujenzi miaka kadhaa,anajua upuuzi mwingi usioujua.
 
Back
Top Bottom