Duuuh, huu upenzi ni wa kiwango cha SGR.
Miaka mitano ya kwanza, raisi yeyote anatembelea mipango iliyopo, mitano inayofuata anakuwa bize kujilimbikizia mali, hapo sasa anaweza chora ramani ya miaka 5(ya mwenzake) ijayo.
Kabla hamjaanza hizi tambo, tuambieni mipango iliyokuwepo kuanzia awamu ya kwanza, ipi ilikamilika na ilikamilika awamu ipi? Ipi bado na ipi ndo inaendelezwa sasa; mfano, daraja la Mkapa, ni mpango wa awamu ya kwanza, awamu ya 3 wakaanzisha mchakato uliokamilika awamu ya nne.
Uwanja wa mpira ni mpango wa awamu ya tatu, ukakamilika awamu nne, mpango wa kusambaza umeme nchi zima ni wa awamu ya pili kwa gharama ya Tshs 1.2trillion, Tanesco wakanyimwa, wakapewa IPTL, guess nani alileta IPTL! Mpaka leo mradi huo haujakamilika, umeridhiwa na REA kwa kuwakamua wananchi sasa.
Maji ya Nile, mpango wa awamu ya 3, Lowasa akawashinda waarabu na mradi ukafanyika kipindi hicho.
Sasa, tujue basi ili anayestahili asifiwe na tusisahau kuweka na madudu yao, tupime ili tupate mizania sawa na ya haki.