Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Naona Mzee wa Kotapini inaingia kwa nguvu na kutoka kwa nguvu , kaja kuongeza nguvu .
 
Watanzania jamani hapa ndio tutie akili, haya mambo ya Chato kufanyika ziara hizi si dalili nzuri. Huyu kweli ataweza kuruhusu akili yake ikubali kuwa haya hayatakuwepo tena huko Chato akishindwa kwenye sanduku la kura?? Si atakomaa na kiti mpaka kufa kwake ili haya yaendelee! Chato sasa ndio Ikulu ya nchi.
Kwahiyo🤔?
 
Pole sana mkuu. Kwani unaamini kuwa Museveni kafunga Safari kutoka Kampala kwa ajili ya kuifanyia kampeni CCM.

Kipi kinamshinda? Kwani anatumia gharama gani wakati gharama zote zinabebwa na serikali yetu? Narudia tena maana naona unakwepa hapo. Siku ile Tanga walisaini mkataba kuwa ujenzi unaanza na kukamilika hii 2020, tena mbele ya wazungu wa Total. Iweje leo 2020 mradi haujaanza kisha wanasaini tena mradi kuanza, huku wazungu wa Total hawapo, zaidi ya wanaccm walioko kwenye kampeni mode? Jikite kwenye ufafanuzi huo.
 
Kwa hakika TUNDU LISSU ni jawabu la watanzania.

Baada ya kumchachafya sanaaa magufuli kwenye kampeni juu ya kuharibu mahusiano na majiran, kujenga kiwanja chato ambacho hakina faida

JAMAA WAMEHANGAIKA SANAA, NASIKIA M7 KAJA KWA MAKUBALIANO [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mmeamua kuja na hoja nyingine? Ile hoja yenu ya kwamba jamaa kakata upepo,anaumwa,imeishia🤔?
 
Kipi kinamshinda? Kwani anatumia gharama gani wakati gharama zote zinabebwa na serikali yetu? Narudia tena maana naona unakwepa hapo. Siku ile Tanga walisaini mkataba kuwa ujenzi unaanza na kukamilika hii 2020, tena mbele ya wazungu wa Total. Iweje leo 2020 mradi haujaanza kisha wanasaini tena mradi kuanza, huku wazungu wa Total hawapo, zaidi ya wanaccm walioko kwenye kampeni mode? Jikite kwenye ufafanuzi huo.
Zinaahirishwa ndoa sembuse muda wa kuanza kwa mradi!!.
 
Kwani Jiwe Leo hajaenda kutembea kanisani?
IMG_20200912_123312_1.jpg
 
Aibu nyingine Museveni kawa translator wa Magu..aibu hii
 
Yaani safari ya M7 Chato ni kujustify matumizi ya Uwanja Wa ndege wa Chato.
 
Mbona hao waganda wamevaa mabarakoa mengi, hawajui mwenye nyumba huwa hayapendi.
 
Hoja ya huyo uliyemquote iko nje ya uwezo wako, ww subiri hoja za nyomi ndio ziko ndani ya uwezo wako.
Hata wewe umeshindwa kulielewa swali langu,kwasababu liko nje ya uwezo wa ubongo wako, yeye angeliewa sio wewe nyumbu.Subiria hoja mserereko, userereke nazo kinyumbu-nyumbu, Ila iwe Makini, usije kufa kama wale wenzako 300 kule mto Mara.
 
Rais Magufuli anaitangaza hifadhi ya burigi -chato kwa aina yake

Miaka michache ijayo hii hifadhi itakuwa inaingiza fedha nyingi sana

Asante sana Rais Magufuli kwa kuona mbali
Kweli watalii wakiganda watakua wanamiminika apa Chato -Burigi iliyokua Kagera huko zamani
 
Wakati ule pale chongoleani Tanga mkawaweka wale wazungu wa Total kwenye jua, mlikuwa mnafanya utapeli wa nini? Huyo Museveni ni bonge la tapeli, aliwahi kuomba enzi za Mkapa RIP, apewe sehemu ya bandari ya Tanga ili apitishe mizigo ya Uganda. Mpaka Mkapa anaingia juzi kaburini hajawahi hata kuona tofali moja! Nilidhani kwakuwa hizi mbwembwe zilifanyika na mradi haukuanza, hakukuwa na haja tena ya kukusanya kundi lile lile la viongozi kula pesa za wananchi, wakati huu wa kampeni kurudia jambo lile, sana sana mnaonekana mnafanya kampeni za kitapeli, ndio maana kumejaa nguo za ccm kwenye huo utapeli. Ukitaka kujua hizo ni kampeni za kitapeli, wale wazungu wa Total mbona leo hawapo maana hela ni zao?
Una hoja ya msingi sana na swali lako linahitaji jibu watu waelewe kilichofanyika Leo tena ni nn tofauti na kile cha nyuma, tatizo unatumia maneno mengi sana kuelezea hoja.
 
Kumbe lile tukio la Tanga lilikua ni uongo...aaaah huyu aliepanga ili tukio ili kuvuta watu amejichanganya sana
 
Kipi kinamshinda? Kwani anatumia gharama gani wakati gharama zote zinabebwa na serikali yetu? Narudia tena maana naona unakwepa hapo. Siku ile Tanga walisaini mkataba kuwa ujenzi unaanza na kukamilika hii 2020, tena mbele ya wazungu wa Total. Iweje leo 2020 mradi haujaanza kisha wanasaini tena mradi kuanza, huku wazungu wa Total hawapo, zaidi ya wanaccm walioko kwenye kampeni mode? Jikite kwenye ufafanuzi huo.
Hili swali la muhimu. Lijibiwe kama lina jibu.
 
Zinaahirishwa ndoa sembuse muda wa kuanza kwa mradi!!.

Sina tatizo na kuahirishwa na ninakubaliana na hilo kabisa. Je kuna haja gani ya kukusanya kundi lile lile la viongozi, kuweka mkataba ambao ulikuwa umeahirishwa? Shaka yangu ni hii, wakati ule Tanga wazungu wa Total walikuwepo, na mradi haukwenda kama tulivyoaminishwa, ila leo igizo ni lile lile bila hao wazungu. Ninachoona hapo ni wanaccm ambao hawana hata kumi ya kutoa kwenye huo mradi, huku wazungu wenye pesa hawako kwenye hizo hii episode II. Naona ni kampeni zaidi.

Ninasema hivyo maana nina uzoefu na huyo Museveni. Aliwahi kupewa sehemu ya bandari ya Tanga aendeleze lakini hakufanya hivyo, hilo bomba alishakubali kulipitisha Kenya lakini kabidili porojo kalileta Tanzania! Kuna mengi ila leo sio mada, lakini huyo Museveni ni tapeli kama matapeli wengine, na ndio maana naona kwa sasa ni kampeni zaidi kuliko kinachoongelewa.
 
Back
Top Bottom