DOKEZO Ujenzi wa maeneo mengi ya Kariakoo hauzingatii usalama wa Watu na mali zao, hatua zichukuliwe tusisubiri majanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwa siku za hivi karibuni kama kati yetu kuna ambao wamebahatika kwenda kwenye eneo maarufu la kibiashara Kariakoo jijini Dar es Salaam mtaungana na mimi kwamba kuna ujenzi wa majengo mengi ya gorofa unaendelea kwa sasa.

Ujenzi huo unafanyika katika Mitaa mbalimbali ya Kariakoo ambapo kipindi hiki majengo zaidi ya 40 yanajengwa huku yakibomoleqa yanabomolewa yote moja kwa moja na kujengwa upya na mengine kukarabatiwa na kuboreshwa.

Lakini uchunguzi nilioufanya katika majengo mengi ambayo yanaboreshwa na kujengwa upya ni kwamba zoezi au michakato ya ujenzi huo inaendeshwa katika mazingira yanayohatarisha usalama wa raia na mali zao.

Katika maeneo niliofika na kushuhudia wamekuwa wakiendesha zoezi la kubomoa huku maeneo ya karibu wafanyabiashara wadogo wadogo na wapita njia wakikatiza maeneo hayo wengine kupanga kabisa bidhaa, ambapo maeneo mengi nyenzo za kuzuia athari zisiwafikie raia ni za kusuasua na pengine nyenzo hizo hazitumiki.
Baadhi ya watu wa karibu na kwenye maeneo ambapo ujenzi unaendelea niliopata fursa ya kuzungumza nao, wanadai kuwa licha ya ujenzi huo kuendelea lakini unawaweka katika mazingira ya wasiwasi muda mwingi.

"Kama unavyoona hali sio rafiki, sidhani kama kuna Mtu anapinga ujenzi lakini angalia wewe kama unaweza kukaa eneo hili bila hofu, lazima ukae na wasiwasi kwamba mbao au kipande cha tofari kinaweza kukuangukia, wanajenga lakini vile vifaa vya kuzuia vitu vyao visitufikie na kuleta athari hawana au kama wanavyo ni vya kubabaisha, tunalindwa na Mungu maana huna la kufanya huwezi kusema uhame utaenda wapi kwa uharaka?"anaeleza Mzee Juma mfanyabiashara eneo la Msimbazi Kariakoo

Wito wake ni upi? "Kwa kuwa uwezekano wa sisi kuondoka kwenye flemu zetu ambazo hakuna ujenzi unaoendelea haupo tunaomba hawa Watu wazingatie mazingira ya usalama wetu tofauti na hivyo utakuja kusikia majanga yanatokea na sijui nani atalaumiwa sisi raia au wao ambao unaona wanaendesha ujenzi bila kuzingatia mazingira"

Pia Mfanyabiashara mwingine (Mama Yanga) nae anaeleza kutofurahishwa na mazingira ya ujenzi usiozingatia usalama wa raia hususani wateja ambao ufika kwenye duka lake.

"Ukiangalia juu ya jengo hili unaona ujenzi unaendelea lakini tazama vizuri kama unaona kuna kitu cha kuzuia jambo lolote likitaka kudondoka lisiangukie huku, sijui sana masuala ya ujenzi lakini ninachoelewa ukiendesha ujenzi sehemu kama hizi lazima tahadhari ya juu iwepo, tunaweza kusema kuwa tuwe na imani na mafundi wanaojenga lakini wao sio malaika wanaweza kuteleza kwa bahati mbaya kitu kikadondokea huku na kuleta madhara makubwa" anasema Mama huyo

Mama huyo ambaye kwenye fremu anapofanyia biashara juu ya jengo hilo kuna ujenzi unaendelea anadai "Mimi vijana wangu walikuwa wanafungia mzigo hapo nje lakini kwa sasa ni ngumu huwezi kumwambia mteja au kijana afungie mzigo nje ya eneo la kibaraza wakati kila akiangalia juu anasikia na kuona mbao zinagongwa bila kitu cha kuzuia!. Tunaomba watambue kuwa wanaendesha ujenzi sehemu za watu wasione kama wapo kwenye kiwanja cha wazi"

Hata hivyo uchunguzi katika suala hili umebaini baadhi ya raia wamekuwa na hofu ya kukatiza kwenye baadhi ya maeneo ambapo ujenzi huo unaendelea na wengi wao wanadai kuwa hakuna usalama wa kutosha ambao unawapa amani hususani kwenye mitaa au njia zinazozunguka eneo ujenzi unapofanyika.

Sanjari hayo imeshuhudiwa wazi baadhi ya wamachinga wakiwa wamepanga bidhaa kwenye maeneo ya kando na ujenzi unapoendelea bila kuzingatia athari zinazoweza kutokea.

Lakini katika maeneo mengi ambapo ujenzi au zoezi la kubomoa linaendelea hakuna mabango ya yanayoowataka raia kuchukua tahadhari wala hakuna waangalizi wa kusisitiza wananchi kutosogelea maeneo hayo.

Kulingana na mazingira hayo ni muhimu sana mamlaka kuliona suala hilo kwa kuchukua hatua ya kuwasisitiza wanaosimamia ujenzi huo kwenye maeneo mbalimbali ya Kariakoo, kuwataka waogeze umakini za kwa kuzingatia matumizi ya vifaa vinavyoongeza usalama wakati ujenzi ukiendelea.

Tusingoje athari zitokee ndio tuanze kunyosheana vidole, tutambue Kariakoo ni sehemu ambayo ina mkusanyiko wa Watu wengi hivyo hata zoezi la ujenzi wowote unaofanyika eneo hilo linatakiwa kufanyika kwa umakini unaozingatia usalama wa raia na mali zao.

Pia soma:
~ OSHA mko wapi? Ubomoaji wa jengo la zamani la DDC Kariakoo unafanyika kiholela, ni hatari kwa usalama wa Watu
~ OSHA yazuia ubomoaji wa Jengo la Zamani la DDC Kariakoo kwa kutofuata utaratibu
Makao Makuu OSHA si wakp.hapo hapo Darisalamu jamani.
 
Unavaa suti na miwani nyeusi na majingambo kibao....mmeshindwa KUDITEKTI hili angalizo ambalo lipo wazi kabisa hata chekechea anaweza kuliona
 
Walipuuza hili andiko,yametokea
 
Hivi ni Kwanini Serikali isizuie kutoa vibali vya ujenzi maeneo ya katikati ya Jiji la Dar ili kupunguza msongamano ?

Kwanini wasitawanyishe majengo nje ya mji kama vile Tegeta , Bunju , Kigamboni, Kimara , mbezi, Mbagala n.k ??

Kwanini wanakosa uzalendo wa kuona mbele miaka 20-50 ijayo kiwa hali itazidi kuwa sio nzuri ??
 
juz kwenye uzi wa ppp nimesema jengo lao ndio pekee naona wanatumia scafold badala ya mirunda. nimependa wao wanatumia chuma kubebea ile floor.mim kwa roshen zaid ya 5 naona kama mirunda inanepq sometimes
 
Maghorofa wanayojenga wakinga,waswahili mengi ni magumashi

Ova
 
Kwa siku za hivi karibuni kama kati yetu kuna ambao wamebahatika kwenda kwenye eneo maarufu la kibiashara Kariakoo jijini Dar es Salaam mtaungana na mimi kwamba kuna ujenzi wa majengo mengi ya gorofa unaendelea kwa sasa.

Ujenzi huo unafanyika katika Mitaa mbalimbali ya Kariakoo ambapo kipindi hiki majengo zaidi ya 40 yanajengwa huku yakibomoleqa yanabomolewa yote moja kwa moja na kujengwa upya na mengine kukarabatiwa na kuboreshwa.

Lakini uchunguzi nilioufanya katika majengo mengi ambayo yanaboreshwa na kujengwa upya ni kwamba zoezi au michakato ya ujenzi huo inaendeshwa katika mazingira yanayohatarisha usalama wa raia na mali zao.

Katika maeneo niliofika na kushuhudia wamekuwa wakiendesha zoezi la kubomoa huku maeneo ya karibu wafanyabiashara wadogo wadogo na wapita njia wakikatiza maeneo hayo wengine kupanga kabisa bidhaa, ambapo maeneo mengi nyenzo za kuzuia athari zisiwafikie raia ni za kusuasua na pengine nyenzo hizo hazitumiki.
Baadhi ya watu wa karibu na kwenye maeneo ambapo ujenzi unaendelea niliopata fursa ya kuzungumza nao, wanadai kuwa licha ya ujenzi huo kuendelea lakini unawaweka katika mazingira ya wasiwasi muda mwingi.

"Kama unavyoona hali sio rafiki, sidhani kama kuna Mtu anapinga ujenzi lakini angalia wewe kama unaweza kukaa eneo hili bila hofu, lazima ukae na wasiwasi kwamba mbao au kipande cha tofari kinaweza kukuangukia, wanajenga lakini vile vifaa vya kuzuia vitu vyao visitufikie na kuleta athari hawana au kama wanavyo ni vya kubabaisha, tunalindwa na Mungu maana huna la kufanya huwezi kusema uhame utaenda wapi kwa uharaka?"anaeleza Mzee Juma mfanyabiashara eneo la Msimbazi Kariakoo

Wito wake ni upi? "Kwa kuwa uwezekano wa sisi kuondoka kwenye flemu zetu ambazo hakuna ujenzi unaoendelea haupo tunaomba hawa Watu wazingatie mazingira ya usalama wetu tofauti na hivyo utakuja kusikia majanga yanatokea na sijui nani atalaumiwa sisi raia au wao ambao unaona wanaendesha ujenzi bila kuzingatia mazingira"

Pia Mfanyabiashara mwingine (Mama Yanga) nae anaeleza kutofurahishwa na mazingira ya ujenzi usiozingatia usalama wa raia hususani wateja ambao ufika kwenye duka lake.

"Ukiangalia juu ya jengo hili unaona ujenzi unaendelea lakini tazama vizuri kama unaona kuna kitu cha kuzuia jambo lolote likitaka kudondoka lisiangukie huku, sijui sana masuala ya ujenzi lakini ninachoelewa ukiendesha ujenzi sehemu kama hizi lazima tahadhari ya juu iwepo, tunaweza kusema kuwa tuwe na imani na mafundi wanaojenga lakini wao sio malaika wanaweza kuteleza kwa bahati mbaya kitu kikadondokea huku na kuleta madhara makubwa" anasema Mama huyo

Mama huyo ambaye kwenye fremu anapofanyia biashara juu ya jengo hilo kuna ujenzi unaendelea anadai "Mimi vijana wangu walikuwa wanafungia mzigo hapo nje lakini kwa sasa ni ngumu huwezi kumwambia mteja au kijana afungie mzigo nje ya eneo la kibaraza wakati kila akiangalia juu anasikia na kuona mbao zinagongwa bila kitu cha kuzuia!. Tunaomba watambue kuwa wanaendesha ujenzi sehemu za watu wasione kama wapo kwenye kiwanja cha wazi"

Hata hivyo uchunguzi katika suala hili umebaini baadhi ya raia wamekuwa na hofu ya kukatiza kwenye baadhi ya maeneo ambapo ujenzi huo unaendelea na wengi wao wanadai kuwa hakuna usalama wa kutosha ambao unawapa amani hususani kwenye mitaa au njia zinazozunguka eneo ujenzi unapofanyika.

Sanjari hayo imeshuhudiwa wazi baadhi ya wamachinga wakiwa wamepanga bidhaa kwenye maeneo ya kando na ujenzi unapoendelea bila kuzingatia athari zinazoweza kutokea.

Lakini katika maeneo mengi ambapo ujenzi au zoezi la kubomoa linaendelea hakuna mabango ya yanayoowataka raia kuchukua tahadhari wala hakuna waangalizi wa kusisitiza wananchi kutosogelea maeneo hayo.

Kulingana na mazingira hayo ni muhimu sana mamlaka kuliona suala hilo kwa kuchukua hatua ya kuwasisitiza wanaosimamia ujenzi huo kwenye maeneo mbalimbali ya Kariakoo, kuwataka waogeze umakini za kwa kuzingatia matumizi ya vifaa vinavyoongeza usalama wakati ujenzi ukiendelea.

Tusingoje athari zitokee ndio tuanze kunyosheana vidole, tutambue Kariakoo ni sehemu ambayo ina mkusanyiko wa Watu wengi hivyo hata zoezi la ujenzi wowote unaofanyika eneo hilo linatakiwa kufanyika kwa umakini unaozingatia usalama wa raia na mali zao.

Pia soma:
~ OSHA mko wapi? Ubomoaji wa jengo la zamani la DDC Kariakoo unafanyika kiholela, ni hatari kwa usalama wa Watu
~ OSHA yazuia ubomoaji wa Jengo la Zamani la DDC Kariakoo kwa kutofuata utaratibu
Taifa la wasiokumbuka na nchi ya wasiojifunza...
 
Back
Top Bottom