Ujenzi wa Reli ya SGR uishie Tabora

Hakuna itaishia ilipopangwa.
 
Jielimishe kwanza kuhusu usafiri wa reli duniani
 
Hakuna boda iliyobusy Tanzania hii kuliko boda ya Tunduma kubali kataa lakini huo ndo ukweli
 
Bora umesema ww wengi hawajui kitu.
 
Kuipeleka mwanza ni very potential mkuu kuliko kuipeleka uelekeo wa kusini. Kusini huku hatuna ushindani sana. Zambia, Malawi na DRC kusini bado zinategemea sana Dar pot. Option ya kwenda Mozambiqu si rafiki kwa sababu ya miundombinu na security. Kuipeleka mwanza ni kutaka kuwin influence ya Kenya kwa mataifa ya Rwanda, Uganda Burundi South Sudan na Eastern DRC . Uganda ina watu 45m, Rwanda 13m na Burundi 12m acha South Sudan na Eastern DRC. Wakati malawi ina watu 19m na Zambia ina watu 18m.
JPM alikuwa anaona mbali sana.
 

Dar to KapiriMposhi tayari tuna TZR. Hivyo ni usimamizi tu.
 
Nimekuelewa kwa mbali kidogo lakini iko hivi hii Sgr haikupaswa kuelekea mwanza kabla ya Kigoma kwa sababu wanaopitisha mizigo mingi bandari ya dar ni DRC, hivyo ilitakiwa hii reli ielekee Kigoma ili mizigo ya Zambia na DRC ikifika kigoma ipakiwe kwenye meli kubwa kupitia ziwa Tanganyika kuelekea DRC na Zambia.
 
mbona unahemkwa hivyo?
 
Zambia kuna SGR ya reli ya uhuru kama hujui kaipande uone sema shirika halifanyi vizuri kutokana na uwepo wa boss anatoka Zambia kwakuwa wao wanahisa kubwa
 
Kigoma mizigo ipi inaenda DRC, Tunatakiwa kujenga meli ziwa Tanganyika ili Mizigo iende Moba, Kalemie iweze kufika Lubumbashi kwa wakati mfupi barabara ipo Kutoka Dar-Tunduma-Sumbawanga hadi bandari ya Kasanga
 
Cobalt inachenjuliwa na kubebwa kwenye ndege kama dhahabu au silver Kwahiyo usitegemee kuona makontena ya cobalt
 
Bandari kuu ikiwekwa pale Tabora hizi hii reli ya Kati itafanyakazi kwa ufanis KUCHUKUA MIZIGO KWENDA Mwanza na kigoma na burundii
 
Hivi Hizi chuki na watu wa Kanda zinawanufaisha nn enyi nyie kizazi cha Nyoka, mnahisi kabisa Chadema Kuna siku itashika dola anyway labda Corona iue watanzania wote abaki Mbowe na genge lake.
Kanda ya ziwa walionyesha uprimitive fulani. Hata akina dudubaya (conc conc conc master) walitamba katika awamu ile,
 
Bora umesema ww wengi hawajui kitu.
Nimeona watu hawaelewi kitu chochote juu ya Congo. Kwanza inabidi watu wajue congo ni nchi kubwa sana. Reli yetu tumefanya makosa kupeleka matrillioni ya hela kujenga reli maeneo yasiyo na mzigo tutakula hasara. Mizigo ipo Zambia na Katanga/kolwezi kwenye migodi.
 
Cobalt inachenjuliwa na kubebwa kwenye ndege kama dhahabu au silver Kwahiyo usitegemee kuona makontena ya cobalt
Kwasasa cobalt bado inasafirishwa na malori kwenda afrika ya kusini kupitia bandari ya Durban. Mzigo wa Cobalt na Copper ni mwingi kiasi kwamba bandarini Dar hawawezi kuhandle.

Na mzigo wa Copper na Cobalt upo mwingi na wa kutosha. Kuanzia copper belt ya Zambia kufika Katanga mpaka Kolwezi mpaka kufika kwenye migodi ya cobalt. Sasa hii reli yetu wamefanya makosa makubwa. Wanapeleka reli kigoma ujue upande wa pili ni uvira na hakuna mzigo na ni mbali sana toka Katanga kwa hiyo mzigo wa cobalt tutaukosa. Na sgr watapeleka karema- katavi ambapo upande wa pili ni Kalemie ambapo hakuna mzigo na ni mbali toka migodi ya Cobalt ya Katanga na kolwezi kama 1000km. Na hapo hujapiga hesabu ya kununua meli kubwa ya mizigo ziwa Tanganyika, na pia Congo inabidi wajenge bandari kubwa upande wao wa Kalemie. Yaani kiufupi mradi wa sgr ukikamilika hautapata mzigo mkubwa wa kurudisha hela na madeni na riba. Nenda kafatilie uzalishaji wa Copper na Cobalt na maeneo ambayo migodi ipo huko zambia(Copper belt) na congo (katanga, Lubumbashi, kolwezi) halafu fatilia geography ya congo. Kisha linganisha na sgr ya inayojengwa ndio utaelewa jinsi sgr inavyopotea
 
Bandari kuu ikiwekwa pale Tabora hizi hii reli ya Kati itafanyakazi kwa ufanis KUCHUKUA MIZIGO KWENDA Mwanza na kigoma na burundii

..nadhani point ya mtoa mada ni kuwa na bandari kavu eneo ambalo litafaa kwa nchi za DRC, Burundi, Rwanda, na Uganda, kufuata mizigo yao. Mtoa mada ametaja Tabora kama mfano tu.
 
Nenda kaangalie ramani ya Congo, Zambia na Tanzania. Halafu angalia umbali kati ya Katanga, Kolwezi kuja Dar kupitia Kapirimoshi zambia. Halafu angalia njia na umbali toka Katanga kuja uvira kisha kigoma kisha Dar. Angalia route ipi ni fupi. Kumbuka hii ni biashara na mzigo ukipita route fupi ndio gharama ya usafiri inapungua. Na mzigo mwingi upo Zambia kwenye copper belt na Cobalt ya congo kwenye migodi iliyopo Katanga mpaka Kolwezi. Hebu kaangalie ramani ndio utaelewa makosa ya sgr
 
Jpm kapotea.


Hii ni biashara, kwenye biashara ya usafiri tunaangalia mizigo inayosafirishwa. Na tunaangalia potential ya kuwepo uhakika wa mizigo ya kusafirisha. Kwa takwimu za bandarini. Mizigo mingi inatoka Migodi ya Zambia na Congo na ndio inapita Bandarini. Sasa ilitakiwa sgr ijengwe kuifuata migodi ya Zambia na Congo. Hicho kilichofanywa kupeleka reli kanda ya ziwa na kigoma ni kupoteza hela na hakuna mizigo ya kurudisha hela na madeni na riba.


Sasa hivi mizigo ya migodini inapitia Durban afrika ya kusini.
 

..ingesaidia kama ungeeleza reli ilitakiwa ipite wapi.

..tueleze reli ianzie wapi, ipite wapi, na iishie wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…