MTZ 255Dar
JF-Expert Member
- Sep 25, 2018
- 1,149
- 3,963
Sio kweli. Makaa ya Mawe ni Gharama nafuu Sana kuliko Fossil Fuels zote. Tatizo la Makaa ya Mawe ni Chanzo kikubwa Cha uchaguzi wa hewa Duniani kuliko vyote. Kilichoifanya Ulaya hasa Ujerumani kutegemea gas ya Urusi ni kwasababu ya Siasa zao za Ndani. Kuanzia Mwaka 1998,Ugerumani ilikuwa na Vinu vya Nyuklia 78 na 60 vya Makaa ya Mawe,Lakini mpaka kufikia mwaka 2010,Zaidi ya Vinu Vya Nyuklia 75 na 60 vya Makaa ya Mawe vilifungwa kwamba vinachafua mazingira. Na hiyo ni kutokana na Vya vya Mazingira Kama chama Cha Kijani Kuingia kwenye Serikali ya Shirikisho.Makaa Ya mawe ni inferior kwa gesi, LA sivyo watu wasingetumia gharama kubwa kuagizishia Gesi nje ya Nchi
Kwahiyo Mimi naamini kabisa Nchi Kama Ujerumani iliyokuwa na Vinu vya Nyuklia 78 na 60 vya Makaa ya Mawe inauwezo wa kuachana na Gas ya Urusi ndani ya MIEZI 6 ikiamua kwasha Vinu vyake vyote vya zamani. Tatizo Kuna vyama vya kisiasa kwenye Serikali ya Shirikisho ambavyo vinapinga Matumizi ya Nishati ya Nyuklia na Makaa ya Mawe,kwahiyo Kisiasa haitawezekana kwa Ujerumani.
Mbadala wa Mafuta ya Urusi ndio Shida mpaka Sasa.