Ujerumani kuanza mgao wa mafuta

Ujerumani kuanza mgao wa mafuta

Ndo shida ya kuingilia ugomvi usiokuhusu.

Hivi ujerumani alkua na ugomvi gan na RUSSIA mpk nae ashiriki kumpiga SANCTIONS.

Angalia Sasa wajerumani wanaishi kwa tabu kwasababu ya viongzi wao kua vibaraka wa USA na kupelekeshwa ovyo.

Pongezi kwa TANZANIA kutokufungamana upande wowote, japo kias chake tunaathirika[emoji4][emoji106]
Sasa Tanzania ina raha gani kuishinda Ujerumani wakati ndizo "Shithole" countries zenyewe. Wewe hata hujui unachoongea ndio wale wale wa kwenye vijiwe vya tangawizi.
 
Russia hawezi kutumia nishati yoyote kuzi-blackmail nchi za magharibi ili akwepe impact ya vikwazo, hapo amechemka vibaya.

Hizo nchi zina njia mbadala zitakazotumia ili tu kuhakikisha kwamba hawanunui nishati ya Russia kwa Ruble hata kama njia hiyo itasababisha upungufu wa nishati kwa kiasi fulani lakini itakuwa ni swala la muda tu kabla hawajapata ufunguzi wa kudumu.

Lakini Russia lazima uchumi utaporomoka kwani hiyo njia anayotaka kutumia ya kulazimisha manunuzi kwa kutumia Ruble haina long term effect.
 
Wewe unadhani Ulaya hawakujua hili la Gas na mafuta kuwa litawapa shida kwa muda fulani but in long run watakuwa wamejiondoa kwenye utumwa wa Gas ya Russia? Kwanza hata leo wakiamua kupata mbadala wanao ambao ni Makaa ya Mawe halafu tuone hiyo Gas Urusi atamuuzia nani.
Watu wengi humu wamekariri kwamba ulaya wasiponunua mali yako umekwisha nawashauri waifuatilie dunia inavyozunguka US ilipositisha ununuz mafuta ghafi toka urusi India imeshakubali kuyachukua hayo mafuta na China ataichukua gas yote itakayokataliwa ulaya, maisha yanaenda kasi sana pamoja na kwamba hapo mwanzo watu walikataa kwamba ulaya hali imeanza kuwa ngumu lakini sasa hivi imedhihirika lakini bado pro US & co. wanakubali ila wanasema baadae Putin Aataumia sana tena wanasema in a long run ni vile wengi hawana taarifa za miaka ya nyuma juu ya Russia
 
Waambie ges haiozi
 
Ujerumani imetangaza rasmi kuanza kutoa gesi kwa watu wake kwa mgao, huku kukiwepo wasiwasi ya kuacha kuagiza mafuta kutoka Russia.

Hatua hiyo imechukuliwa wakati kuna hali ya kutoelewana kuhusu malipo kwa kutumia sarafu ya Russia.

Hatua ya umoja wa ulaya kuanza kutekeleza onyo la mapema la uwezekano wa kutokea uhaba wa gesi, ni ishara ya moja kwa moja ya kutokea uhaba wa mafuta kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Waziri wa uchumi wa Ujerumani Robert Habeck, ameambia waandishi wa habari kwamba chumba cha dharura kitaundwa ndani ya wizara hiyo, akiongezea kwamba timu itakayosimamia swala hilo itahusisha wanachama kutoka kwa wizara hiyo, wasimamizi wa mafuta nchini humo na wadau kutoka sekta binafsi.

Katika hatua inayoonekana kama juhudi za kuimarisha sarafu yake ambayo inaendelea kupoteza thamani, Russia imesema kwamba itaweka mikakati ifikapo March 31, ambapo nchi ambazo zimetajwa kwamba sio rafiki, zile ambazo zimeiwekea vikwazo, zitalipia gesi yake kwa kutumia sarafu ya Russia na wala sio Euri wala dola ya Marekani.

Moscow inatarajiwa kuzindua kanuni mpya kuhusu malipo ya gesi kesho alhamisi.

Kremlin imesisitiza kuhusu mfumo kwa malipo ya gesi kwa umoja wa ulaya, baada ya mawaziri kutoka nchi 7 tajiri duniani kutaja mpangilio huo kuwa usiokubalika.

Uvamizi wa Ukraine imepelekea Russia kuwekewa vikwazo kadhaa na kupelekea sarafu yake kushuka kwa thamani huku Ulaya ikisitisha uagizaji wa mafuta na gesi kutoka Russia.

VOA Swahili
Ujerumani imeingizwa cha kike na USA
 
Wewe unadhani Ulaya hawakujua hili la Gas na mafuta kuwa litawapa shida kwa muda fulani but in long run watakuwa wamejiondoa kwenye utumwa wa Gas ya Russia? Kwanza hata leo wakiamua kupata mbadala wanao ambao ni Makaa ya Mawe halafu tuone hiyo Gas Urusi atamuuzia nani.
Unadhani ni rahisi hivyo? Acha kuwaza kama mtoto mdogo.
 
Kwa urussi anampa gesi bure kwamba ulaya akigoma yeye urussi hati hasara unajua revenue urussi atakayopoteza kama ulaya wakigoma kununua gesi na mafuta kutoka urusi uingeongea unachoongea
Unachafua michango ya watu kwa kihoja kilekile. Halafu umeandika kama vile Russia ndiye aliyeanza league ya vikwazo.
Yeye kajibu kubalance athari. Punguza mahaba yako kwa wamagharibi ili uone uhalisia wa mambo.
 
SASA KAMA HAWAPEWI BURE,SI WANUNUE
Mbona urussi ameongeza deadline kama kweli anajiamin si alisema tarehe moja ndo mwisho mbona ameongeza deadline

Mpaka Leo nchi za ulaya hazifuata matwaka yake na bado anaruhusu gesi iflow ulaya
 
Unachafua michango ya watu kwa kihoja kilekile. Halafu umeandika kama vile Russia ndiye aliyeanza league ya vikwazo.
Yeye kajibu kubalance athari. Punguza mahaba yako kwa wamagharibi ili uone uhalisia wa mambo.
Na wewe punguza mahaba kwa Russia na Putin hili ni jukwaa huru, kama wewe ulivyokua na uhuru wa kuwa upande wa Putin na mim pia Nina uhuru wa kuchagua upande
 
Wateja hawakosekani,je utawauzia kwa bei na kiwango kikubwa kama kile ulichokuwa unauza Ulaya na vipi kuhusu miundombinu hizo gharama za kujenga miundombinu mipya atagharamia nani?

Gas inasafirishwa hata kwa meli au hujui mkuu
 
Gas inasafirishwa hata kwa meli au hujui mkuu
Utasafirisha kwa kiwango gani na kwa muda upi huo ili kusiwe na shortage kwenye soko? Na ujue Marekani ana Gas na mafuta ila kuisafirisha kiwango cha kuhimili mahitaji ya soko la Ulaya ndio changamoto kubwa.
 
Sasa hivi kama una pesa ya madafu umeifungia ndani unaenda kuchange kwa Ruble tu halafu unatulia zako kusikilizia mshindo mkuu.
Shida ni kuipata hio Ruble kwenye hizi bank na bureau zetu.
 
Sasa hivi kama una pesa ya madafu umeifungia ndani unaenda kuchange kwa Ruble tu halafu unatulia zako kusikilizia mshindo mkuu.
Shida ni kuipata hio Ruble kwenye hizi bank na bureau zetu.
Aikambe.
FPNEQC4XoAM_K-1.jpg
 
Makaa Ya mawe pia Ulaya Wanamtegemea Urusi kama hufahamu. Russia ni Nchi ya Pili duniani baada ya US kwa Makaa ya Mawe.
Duuuh...! Ndiyo pro USA na EU watambue ile tafsiri ya ecosystem si katika biology tu bali hata kiuchumi duniani tunaitumia bila kupenda [emoji6][emoji28]
 
Wewe unafikiria kweli, gesi itakosa wateja? Urusi akishusha bei kama alivyofanya atapata wateja wengi, india na china zinaweza kua substitute nzuri tu. Ndio maana USA kaanza kumpiga mkwara India.
Ama kwanini USA alikimbilia Venezuela kuongea na Rais wake amuuzie gesi [emoji848] mahaba ni utumwa mbaya sana na nauchukia mno maana unaweza kukutoa akili hata kukutesa na kukupatia BP, vidonda vya tumbo, msongamano wa mawazo hadi ukagongwa na gari, mshtuko wa ubongo hadi ukaparalaizi mwili mzima

Sasa hicho ndicho kinachowatesa pro USA na EU [emoji1]
 
Back
Top Bottom