Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Sasa kwa nini na wewe unapinga uwekezaji wa Bandari?
Sipingi uwekezaji, hata kama wangeweza kubinafsisha kila sekta na taasisi ni sawa tu ila lazima terms ziwe na faida zaidi kwa raia wazawa. Wawekezaji wamekuwepo kwenye Gesi na madini, hivi viwili vimekuwa kwa wawekezaji kwa muda mrefu tu ila ukifika kunapochimbwa hayo madini na gesi ni ufukara mtupu, hakuna barabara wala maji. Ambako hawana hayo madini wana afadhali.

Kama wataweza kumpa muwekezaji NIDA na mkataba ukaonyesha atatoa vitambulisho kwa raia halali tu kwa muda usiozidi mwezi mmoja mimi nitasapoti.

Kama watampa muwekezaji ATCL na mkataba ukamtaka ashushe nauli za ndege kama enzi za Fastjest mimi nitasapoti.
 
Imeuzwaje? Huo ndo ujinga unaoongelewa kwenye huu uzi!!

Labda niambie Bandari imeuzwaje na imeuzwa shilingi ngapi?

Raisi wako amesema Serikali haifanyi Biashara hivyo mashirika yetu kuuzwa kwa state run foreign Governments, hiyo ndiyo irony yenyewe, Mashirika makubwa ya karibia nchi zote yako controlled na States na hii ni Dunia nzima, kwetu yanagawiwa kwa foreigners …
 
Serikali imeshatumia muda wa kutosha kuelezea kuhusu bandari.

Walipofikia wasiotaka kuelewa awawezi elewa ni sawa na kumuwekea mtu picha ya simba unamuuliza anaona nini, anakwambia tembo. Hao ndio waliobaki awataki kuelewa.

Kuendelea kutoa elimu kila siku ni kupoteza muda. Mpaka huruma jana kwenye club yaani wakili anajibu swali kwa maelezo, anapewa fursa mtu mwingine ya kuuliza swali anauliza kitu kile kile.

Huko sasa ni kutwanga maji kwenye kinu, hao waliobaki wameshaamua kutoelewa ni muda wa kufunga kurasa ya kutoa elimu na kuendelea na shughuli zingine za serikali huo mradi wabishi wasubiri matokeo.
 
Sipingi uwekezaji, hata kama wangeweza kubinafsisha kila sekta na taasisi ni sawa tu ila lazima terms ziwe na faida zaidi kwa raia wazawa. Wawekezaji wamekuwepo kwenye Gesi na madini, hivi viwili vimekuwa kwa wawekezaji kwa muda mrefu tu ila ukifika kunapochimbwa hayo madini na gesi ni ufukara mtupu, hakuna barabara wala maji. Ambako hawana hayo madini wana afadhali.

Kama wataweza kumpa muwekezaji NIDA na mkataba ukaonyesha atatoa vitambulisho kwa raia halali tu kwa muda usiozidi mwezi mmoja mimi nitasapoti.

Kama watampa muwekezaji ATCL na mkataba ukamtaka ashushe nauli za ndege kama enzi za Fastjest mimi nitasapoti.
Shida yako ndugu yangu ni ubinafsi. Unataka mwekezaji apewe sehemu zilizokuathiri wewe tu ila sehemu zingine ambazo zinaweza kutuvusha na kutufanya kuwa nchi ya mfano kiuchumi hutaki apewe unasema terms.

Labda nikuulize terms zipi za mkataba wa IGA huzitaki na kwa nini?

Je ufafanuzi uliotolewa kwenye hizo terms unaukubali?
 
Serikali imeshatumia muda wa kutosha kuelezea kuhusu bandari.

Walipofikia wasiotaka kuelewa awawezi elewa ni sawa na kumuwekea mtu picha ya simba unamuuliza anaona nini, anakwambia tembo. Hao ndio waliobaki awataki kuelewa.

Kuendelea kutoa elimu kila siku ni kupoteza muda. Mpaka huruma jana kwenye club yaani wakili anajibu swali kwa maelezo, anapewa fursa mtu mwingine ya kuuliza swali anauliza kitu kile kile.

Huko sasa ni kutwanga maji kwenye kinu, hao waliobaki wameshaamua kutoelewa ni muda wa kufunga kurasa ya kutoa elimu na kuendelea na shughuli zingine za serikali huo mradi wabishi wasubiri matokeo.
Nimesikiliza ule mjadala hadi nimesikitika. Nchi hii ujinga ni tatizo kubwa sana
 
Raisi wako amesema Serikali haifanyi Biashara hivyo mashirika yetu kuuzwa kwa state run foreign Governments, hiyo ndiyo irony yenyewe, Mashirika makubwa ya karibia nchi zote yako controlled na States na hii ni Dunia nzims, kwetu yanagawiwa kwsma foreigners …
Shirika gani limegawiwa kwa Foreigners?
 
Enzi za Mao, China ilikuwa nchi ya kikomunisisti iliyoamini katika Sera za Ukomunisti.

Pamoja na Ukomunisti wa China, Rais wa kwanza wa China, Mao aliamini kuwa ni lazima apeleke vijana nje ya China wakajifunze Dunia inaendaje na ikoje ili warudi kufanya mabadiliko China.

Moja ya vijana hao alikuwepo Den Xiapoing ambaye alikuja kuwa Rais wa China baada ya Mao. Den alipelekwa Ulaya na akajifunza sana namna uchumi wa Ulaya ulivyokuwa unaenda.

Alipokuja kurudi China, Den alianzisha mfumo wa Private Property na Uwekezaji wa Sekta binafsi katika mfumo wa Uchumi wa China. Kipindi chake ndo makampuni mengi ya Marekani yalienda kufungua viwanda na kufanya uwekezaji China.

Kwa wachina wengi walimuona Deng ni msaliti wa Mao kwa kuwa wengi walikuwa wanaamini kila kitu ni cha wachina na mwekezaji kutoka nje ni mwizi. Den aliwajibu haijalishi kama paka ni mweupe au ni mweusi ili mradi anakamata panya basi huyo anatufaa

Pamoja na wachina kupata shida kuelewa Sera za Den Xiapoing ila leo ndo wachina wanamsujudu kama The Father of Modern China.

Ukiacha China kuna nchi za Singapore na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao Dubai ni nchi mojawapo za umoja huo.

Hizi nchi nazo miaka ya 1960 ilikuwa kama sisi! Ila watawala wao walipata akili kuwa kwa akili za kuwaza sisi ndo sisi hatutafika popote. Kupitia rasilimali ya mafuta Dubai walibadilisha Sera zao kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi. Leo hii kila mtu Duniani anakwenda kutalii Dubai na si kwa sababu ya mafuta tu ila kutokana na namna ikivyojengwa , inavyopendeza na ilivyo na uchumi mkubwa na maendeleo makubwa.

Ukija Tanzania. Hapa ndo shida ilipo. Nchi hii ilianzishwa katika misingi ya kijamaa. Misingi hii iliwaaminisha watu kuwa kila kitu ni Serikali na Serikali ni kila kitu. Mfumo huu ambao unaamini katika state capture umedumaza akili za Watanzania wengi sana kiasi ambacho kuna Watanzania leo hawajifunzi hata dunia ikoje, inaenda wapi na itakuwa wapi miaka hata 50 mbele.

Akili hizi zinaamini kuwa Sera ya uwekezaji ni kuuza nchi, Uwekezaji ni uuzaji wa nchi. Sera hii imewafanya Watanzania kuwa nyuma sana. Nchi yetu kuwa nyuma sana, mifumo yetu ya huduma kuwa nyuma sana.

Leo hii Tanzania, unatoka Dar hadi Kigoma kwa masaa zaidi ya 15 kwenye treni ambayo muda wowote unaweza kuambiwa leo hakuna usafiri. Ndani ya hiyo treni vyoo vichafu, huduma ni mbovu ila mtanzania hana shida ili mradi tu inamilikiwa na Serikali

Leo hii nchi yetu ina bandari zinayoweza kuhudumia ipasavyo nchi hadi 8 zinazotuzunguka, ila meli zinakaa wiki 2 hadi 3 kushusha mizigo, wafanyabiashara wanapoteza mizigo yao, hakuna mapato makubwa nchi inaweza kupata na kufanya maendeleo makubwa ila watu wanaona sawa tu ili mradi iwe chini ya Serikali. Hawajali hata wakiambiwa meli zinakimbia zinaenda Bandari za nchi jirani ili mradi waone au wasikie Serikali ndo mmiliki. Huu ni ujinga uliotukuka sana.

Kibaya zaidi pamoja na ujinga huu wa Watanzania, nchi jirani zinazotuzunguka zinakimbia sana ili kukamata fursa za kiuchumi sisi tusiwe na kitu. Rwanda amejenga Bandari kavu kubwa sana ili mizigo ya Congo Mashariki ipite kwake . Bandari hii kawapa wawekezaji. Sasa Rwanda anajenga uwanja wa Ndege mkubwa zaidi Afrika Mashariki ambao utaendeshwa pia na Sekta binafsi.

Huku Kenya amejenga Bandari ya Lamu ambayo ataiendesha kwa sehemu kubwa kupitia sekta binafsi, Msumbiji kaomba vikosi vya Rwanda vilinde Bandari zake ili wawekezaji waweze kuwekeza na zifanye biashara. Hawa wakifanya haya Serikali ikichukua hatua kuboresha utendaji wa Bandari kuna watu wanaaza kusema nchi inauzwa.

Serikali ikiwasikiliiza hawa watu kuna hatari kubwa sana huko mbeleni nchi yetu kuja kuwa kituko cha mwisho zaidi kuliko hata sasa, kutokana na kusikiliza wajinga huku nchi ikitakuwa ikimbie iendane na mabadiliko ya Dunia ya sasa.

Kwa Dunia inavyokwenda sasa, Tanzania haipaswi kurudi nyuma tena! Ujinga usipewe tena nafasi Tanzania!

Haya ndio madhara ya kupata madaraka kwa njia ya kupora chaguzi. Matokeo yake viongozi wanakuja na mipango bila kushirikisha wananchi, wakiamini wananchi ni kama watoto wa chekechea, hivyo wanatakiwa kuwafanyia lolote la kuwaletea maendeleo kwa utashi wa viongozi, na sio kwa mashauriano na wananchi. Inshort wananchi hawana imani na viongozi, na wala sio suala la ujinga.

Hapa tulipo wananchi hawana imani na viongozi, huku viongozi wakijifanya wana nia njema ya kuwakomboa wananchi. Kama kweli bandari zinabinafsishwa kutokana na kukosa ufanisi, ni sekta nyingi sana hazina ufanisi, kwanini hizi hazibinafsishwi? Kwakuwa serikali ina amini ina akili ila wananchi ndio wajinga, waweke nikataka hadharani kila mtu aone, na hakuna kuingia mkataba wowote bila wananchi kuridhika.
 
Wapi duniani limewai kufanya jambo baada ya wananchi wote kuridhia?
 
Hata Leo tumechelewa kuzibinafsisha
Vipi kuhusu NIDA, ATCL, Huduma duni na slow za Halmashauri, TANESCO, Hospitali za serikali, TBC, TRA n.k nako kubinafsishwe??
 
Kuna kitu muhimu katika uzi wako umekiacha tena kwa makusudi.

China hawakukaribisha Wawekezaji tu bila kuangalia Maslahi yao. Kitu cha kwanza walisomesha vijana wao na kwa hiyo Wawekezaji walipoenda China kulikuwa na sharti la kuajiri vijana wao. Vijana walioajiriwa walipopata mitaji wakaanzisha viwanda vidogo vidogo vya vipuri na ikawa progressive mpaka kuweza kutengeneza mitambo mikubwa. Na Serikali Ilikuwa inadhaibiti kwa manufaa ya Wananchi wake

Kwa hiyo China walikaribisha Wawekezaji wakiwa na nia ya kupata mtaji, ujuzi, exposure na teknolojia na matokeo yake China kwa sasa Wamewapita Sana Hao Wawekezaji na Wanashindana nao huko Duniani kwa mauzo ya bidhaa na huduma.

Kuhusu Falme za Kiarabu nayo iko hivyo, pamoja na Biashara ya Mafuta, Wawekezaji wote wa kigeni lazima wawe na Washirika wazawa hata kama hao wazawa hawana mitaji inabidi wapewe hisa za mkopo. Hali hiyo imepelekea Nchi hizo kushamiri kiuchumi.

Haya sasa Njoo kwenye nchi yetu. Ni mkakati gani umewekwa wa kufanya Uwekezaji wa Wageni kumnufaisha Mtanzania mmoja mmoja au Taifa kwa ujumla wake?
Kuna sheria ya local content mbona pia sheria ya natural resource and permanent sovereignty. Mfano inaongelea mambo ya capacity building, kuajiri wazawa, kuwapa capacity taasisi za ndani mfano TPDC walipewa hisa kwenye gesi ya Mtwara na pia wamewezeshwa na wenyewe Kuna vitalu wanachimba wenyewe. Pia serikali inapewa 16% undillutable shares hata kama haiweki mtaji!!

Mikakati ipo tatizo ni Kasi ya utekelezaji tu.
 
Unachanganya mambo, Kampuni karibia zote kubwa za China ni state owned, hapa kwetu raisi wako anasema Serikali haifanyi biashara na kuuza Kampuni zetu zote cha ajabu zaidi anauzia Kampuni ambazo ni state owned huku akitukataza Serikali yetu kufanya biashara sasa kama Serikali kuendesha Kampuni ni haramu iweje auze Bandari zetu kwa foreign Governments?

Umetaja Singapore, nani ana own Bandari ya Singapore? Ni foreigners au Singoporean Government?
Issue sio umiliki wa serikali issue ni ufanisi, tatizo la serikali zetu hazina ufanisi kabisa embu niambie taasisi Gani ya serikali yetu Ina ufanisi? Zote zimeoza Sasa why ulazimishe tu umiliki wa serikali hata kama hakuna ufanisi?

TTCL na Vodacom ni mbingu na ardhi, ATCL na Precision ni mbingu na ardhi, kiufupi hakuna government entity inaizidi private sector kwa ufanisi. Hata kampuni kama Deloitte na PWC zinaizidi ufanisi TRA na NAO kwenye ukaguzi.

Nadhani mfumo wa uendeshaji taasisi za serikali ubadilike, ziwe za mikataba zenye KPI otherwise hawa mafisadi hawana uchungu na chochote sababu bandari iingize hasara au faida hawana Cha kupoteza na mishahara ipo pale pale.
 
Enzi za Mao, China ilikuwa nchi ya kikomunisisti iliyoamini katika Sera za Ukomunisti.

Pamoja na Ukomunisti wa China, Rais wa kwanza wa China, Mao aliamini kuwa ni lazima apeleke vijana nje ya China wakajifunze Dunia inaendaje na ikoje ili warudi kufanya mabadiliko China.

Moja ya vijana hao alikuwepo Den Xiapoing ambaye alikuja kuwa Rais wa China baada ya Mao. Den alipelekwa Ulaya na akajifunza sana namna uchumi wa Ulaya ulivyokuwa unaenda.

Alipokuja kurudi China, Den alianzisha mfumo wa Private Property na Uwekezaji wa Sekta binafsi katika mfumo wa Uchumi wa China. Kipindi chake ndo makampuni mengi ya Marekani yalienda kufungua viwanda na kufanya uwekezaji China.

Kwa wachina wengi walimuona Deng ni msaliti wa Mao kwa kuwa wengi walikuwa wanaamini kila kitu ni cha wachina na mwekezaji kutoka nje ni mwizi. Den aliwajibu haijalishi kama paka ni mweupe au ni mweusi ili mradi anakamata panya basi huyo anatufaa

Pamoja na wachina kupata shida kuelewa Sera za Den Xiapoing ila leo ndo wachina wanamsujudu kama The Father of Modern China.

Ukiacha China kuna nchi za Singapore na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao Dubai ni nchi mojawapo za umoja huo.

Hizi nchi nazo miaka ya 1960 ilikuwa kama sisi! Ila watawala wao walipata akili kuwa kwa akili za kuwaza sisi ndo sisi hatutafika popote. Kupitia rasilimali ya mafuta Dubai walibadilisha Sera zao kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi. Leo hii kila mtu Duniani anakwenda kutalii Dubai na si kwa sababu ya mafuta tu ila kutokana na namna ikivyojengwa , inavyopendeza na ilivyo na uchumi mkubwa na maendeleo makubwa.

Ukija Tanzania. Hapa ndo shida ilipo. Nchi hii ilianzishwa katika misingi ya kijamaa. Misingi hii iliwaaminisha watu kuwa kila kitu ni Serikali na Serikali ni kila kitu. Mfumo huu ambao unaamini katika state capture umedumaza akili za Watanzania wengi sana kiasi ambacho kuna Watanzania leo hawajifunzi hata dunia ikoje, inaenda wapi na itakuwa wapi miaka hata 50 mbele.

Akili hizi zinaamini kuwa Sera ya uwekezaji ni kuuza nchi, Uwekezaji ni uuzaji wa nchi. Sera hii imewafanya Watanzania kuwa nyuma sana. Nchi yetu kuwa nyuma sana, mifumo yetu ya huduma kuwa nyuma sana.

Leo hii Tanzania, unatoka Dar hadi Kigoma kwa masaa zaidi ya 15 kwenye treni ambayo muda wowote unaweza kuambiwa leo hakuna usafiri. Ndani ya hiyo treni vyoo vichafu, huduma ni mbovu ila mtanzania hana shida ili mradi tu inamilikiwa na Serikali

Leo hii nchi yetu ina bandari zinayoweza kuhudumia ipasavyo nchi hadi 8 zinazotuzunguka, ila meli zinakaa wiki 2 hadi 3 kushusha mizigo, wafanyabiashara wanapoteza mizigo yao, hakuna mapato makubwa nchi inaweza kupata na kufanya maendeleo makubwa ila watu wanaona sawa tu ili mradi iwe chini ya Serikali. Hawajali hata wakiambiwa meli zinakimbia zinaenda Bandari za nchi jirani ili mradi waone au wasikie Serikali ndo mmiliki. Huu ni ujinga uliotukuka sana.

Kibaya zaidi pamoja na ujinga huu wa Watanzania, nchi jirani zinazotuzunguka zinakimbia sana ili kukamata fursa za kiuchumi sisi tusiwe na kitu. Rwanda amejenga Bandari kavu kubwa sana ili mizigo ya Congo Mashariki ipite kwake . Bandari hii kawapa wawekezaji. Sasa Rwanda anajenga uwanja wa Ndege mkubwa zaidi Afrika Mashariki ambao utaendeshwa pia na Sekta binafsi.

Huku Kenya amejenga Bandari ya Lamu ambayo ataiendesha kwa sehemu kubwa kupitia sekta binafsi, Msumbiji kaomba vikosi vya Rwanda vilinde Bandari zake ili wawekezaji waweze kuwekeza na zifanye biashara. Hawa wakifanya haya Serikali ikichukua hatua kuboresha utendaji wa Bandari kuna watu wanaaza kusema nchi inauzwa.

Serikali ikiwasikiliiza hawa watu kuna hatari kubwa sana huko mbeleni nchi yetu kuja kuwa kituko cha mwisho zaidi kuliko hata sasa, kutokana na kusikiliza wajinga huku nchi ikitakuwa ikimbie iendane na mabadiliko ya Dunia ya sasa.

Kwa Dunia inavyokwenda sasa, Tanzania haipaswi kurudi nyuma tena! Ujinga usipewe tena nafasi Tanzania!
Well said 🖐🏿🖐🏿🖐🏿
 
Issue sio umiliki wa serikali issue ni ufanisi, tatizo la serikali zetu hazina ufanisi kabisa embu niambie taasisi Gani ya serikali yetu Ina ufanisi? Zote zimeoza Sasa why ulazimishe tu umiliki wa serikali hata kama hakuna ufanisi?

TTCL na Vodacom ni mbingu na ardhi, ATCL na Precision ni mbingu na ardhi, kiufupi hakuna government entity inaizidi private sector kwa ufanisi. Hata kampuni kama Deloitte na PWC zinaizidi ufanisi TRA na NAO kwenye ukaguzi.

Nadhani mfumo wa uendeshaji taasisi za serikali ubadilike, ziwe za mikataba zenye KPI otherwise hawa mafisadi hawana uchungu na chochote sababu bandari iingize hasara au faida hawana Cha kupoteza na mishahara ipo pale pale.
Kazi ya Serikali ni kukusanya kodi, kusimamia Sheria na kutoa huduma za msingi tu. Hayo mengine Serikali mnaionea
 
Back
Top Bottom