Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Issue sio umiliki wa serikali issue ni ufanisi, tatizo la serikali zetu hazina ufanisi kabisa embu niambie taasisi Gani ya serikali yetu Ina ufanisi? Zote zimeoza Sasa why ulazimishe tu umiliki wa serikali hata kama hakuna ufanisi?

TTCL na Vodacom ni mbingu na ardhi, ATCL na Precision ni mbingu na ardhi, kiufupi hakuna government entity inaizidi private sector kwa ufanisi. Hata kampuni kama Deloitte na PWC zinaizidi ufanisi TRA na NAO kwenye ukaguzi.

Nadhani mfumo wa uendeshaji taasisi za serikali ubadilike, ziwe za mikataba zenye KPI otherwise hawa mafisadi hawana uchungu na chochote sababu bandari iingize hasara au faida hawana Cha kupoteza na mishahara ipo pale pale.
Hicho ndicho tunakipigia kelele
Hizi taasisi za serikali tunazodai tuziendeshe mbona Sasa tumeshindwa
Hebu nenda kwenye shule za serikali ambazo Nyerere alizitaifisha kutoka kwa wahindi na wazungu,kaangalie miundombinu yake leo ilivyo,
Wakati hizo shule zinataifishwa watoto wa viongozi walikua wanapelekwa huko,leo hii hakuna Kiongozi anaetamani kumpeleka mtoto wake huko ,lakini akitokea mtu akasema tubinafsishe hizi shule ,watatokea kina tibaijuka ambayo watoto wao wanasoma huko Kemibos wake kupinga,na vile tu mazwazwa anapata washangiliaji
Hebu angalia UDART leo ilivyo ,ni usafiri au upuuzi ,ila akija Kiongozi akasema kua nabinafsisha huu usafiri kwa waarabu ,wataibuka kina polepole wanaopanda V8 kuja kupiga soga,ila kwa vile hao wanaopanda hizo mwendokasi akili zao zipo kama mbuzi maana wanavyorundikwa hamna tofauti na mbuzi,watamuunga mkono
Ajabu sana nchi hii,haishangazi kuona viongozi wanaamua waibe wawezavyo maana hata akiinuka wa kuwapigania wanajazwa ujinga na kumuona aduin
 
Nimeshuhudia Warundi wakiingizwa usiku pale NIDA Chang'ombe kwenda kutoa alama za vidole kulikuwa na afisa wa NIDA na Mlinzi wa SUMA JKT kila Mrundi aliliwa jiwe tatu 300,000 daadeki halafu kuna watu humu wanalilia uzalendo kwe kwe kwee😆😆
Mimi Kuna mdada nilikutana nae kwenye hizi kazi zetu ,Sasa akatoa kitambulisho Cha NIDA kipya kabisaa,nikamuuliza umekipata lini ,akijidai mwaka Jana sijui juzi,ila nikiangalia kile kitambulisho ni hv vipya,nikamdodosa weee ,mwisho akaniambia kua ni wiki mbili tu ila alitoa laki 2
Tumeoza kila sehemu
 
Tumeoza kila sehemu
Kwahiyo tumuachie huyu Mama "auze" angalao tupate huduma bora, kwamfano makampuni ya kimataifa yalipouziwa leseni za mawasiliano tu TTCL ndio hiyooo inakata roho nina imani hata hii Bandari mambo yatabadilika sana saana.
 
Magufuli ameuza ardhi ya Tanzania kwenye kampuni ya Hoima Pipeline huku Wana wakiwa kimyaa hatutapata transit fees kwa kila barrel na hakuna Ndezi aliyefungua mdomo.
 
Magufuli ameuza ardhi ya Tanzania kwenye kampuni ya Hoima Pipeline huku Wana wakiwa kimyaa hatutapata transit fees kwa kila barrel na hakuna Ndezi aliyefungua mdomo.
Wewe uliyejua hivyo ulifanya nini?
Mbona hukulileta hilo lijadiliwe, angalau hapa tu JF?

Mkuu 'Imhotep', nadhani sasa ni wazi wewe ni walewale wasiokuwa na hili wala lile; maana inaelekea uko kila mahala.

Haya, tueleze sasa wewe hizo habari za Tanzania "kutopata 'transit fees' kwa kila 'barrel'" ziko vipi. Hizi habari umezipata wapi na lini?
 
China ina mfumo gani ? Kati ya China na sisi Ni nani ana Makampuni mengi ya State ? Aisee badala ya kuwaza ni vipi Kampuni zetu zitafuka maji kama tu hawa Halotel ambao wamekuja mpaka huku kufanya kazi tunawaza ni nani aje atufanyie vitu....
 
Well sijui hao wengi lkn ukiona wengi wanapinga ina maana hawataki kwa nini muwalazimishe wakati wengi hawataki?
Hata vyama vingi wengi walikataa, waTanzania wengi ni wajinga, waoga, na wajuaji ndio maana hata JPM alituburuza sababu alijua akisubiri maoni atacheleweshwa.
Demokrasia ni kusikiliza wengi
Ni kweli ndio maana mjadala ulienda bungeni na makubaliano yakawekwa wazi enzi za awamu zingine makubaliano yalifanyika gizani bila mtu kushirikishwa terms za mkataba.

tumeshaumizwa sana hivyo tutakuwa ni wajinga kama tusipotaka kuwa waangalifu kwani wanaotetea dp world ndio wale wale pia waliotetea kuuzwa kwa shirika la reli kwa wahindi, ndio wale wale waliotetea uwekezaji wa migodi ya dhahabu ambapo sasa yamebakia mashimo na hakuna tulichofaidika, hivyo its human kama ulishaumizwa kuwa mwangalifu …
Sheria zimebadilika sana mkuu, JPM licha ya kutomkubali ila walau aliweka sheria ngumu kwa mwekezaji hasa permanent sovereignty and natural resources act, sheria za local content na transfer pricing, sheria za umiliki 16% za undillutable shares. So hata tukiibiwa sio kirahisi kihivyo tofauti na enzi zile.

By the way tunachopaswa ni kuweka sawa mkataba lakini sio Kupinga bandari kubinafsishwa. Maana hata bila kubinafsishwa TPA itakufa tu kama ilivyokufa TTCL au ATCL!! Hata hao TRC hata isingebinafsishwa ingekufa tu maana hakuna taasisi ya umma inayofanya biashara huwa ipo competent
 
China ina mfumo gani ? Kati ya China na sisi Ni nani ana Makampuni mengi ya State ? Aisee badala ya kuwaza ni vipi Kampuni zetu zitafuka maji kama tu hawa Halotel ambao wamekuja mpaka huku kufanya kazi tunawaza ni nani aje atufanyie vitu....
Mkuu hata china na Hong Kong mbona Kuna bandari na terminal zipo chini ya Dp World.

Nadhani mjadala uwe mkataba uwe rafiki ila kubinafsisha hakukwepeki maana tumefeli kwa miaka 60. Hata JPM na ukali wote ule alishindwa bandari unadhani nani kwa serikali hii ataweza?

Mfano tu NIDA nmejisajili miaka 5 Sasa Sina NIDA mpaka Leo, hivi wakisema vitambulisho vichapwe na kampuni ya kizungu mtapinga? Tumeshindwa acha tusaidiwe maana hatuwezi.
 
Ni ajabu sana kwa mtu mwenye akili kudhanikwamba maendeleo yaliyopo China yameletwa na watu kutoka nje. Hii akili siyo ya kawaida kabisa
Aah mkuu wangu hapa umeteleza, sio tu maendeleo ya china yaliletwa ila mpaka Sasa maendeleo ya china yanategemea mataifa ya nje.

Hivi unafahamu china inashusha thamani ya pesa yake Ili kupata wawekezaji wengi zaidi? haiko sustainable maana Haina strong middle income kulinganisha na US.

Sasa kama wages za china zipo chini unadhani bila investment za nje wata survive vipi?

Ukweli usemwe bila ubepari ulioletwa na Deng Xiaoping hakuna china yenye maendeleo. Kama ni kazi, Mao Alipiga sana kazi na watu walilima sana ila hatukuona uchumi kama huu wa Sasa.
 
Mkuu hata china na Hong Kong mbona Kuna bandari na terminal zipo chini ya Dp World.

Nadhani mjadala uwe mkataba uwe rafiki ila kubinafsisha hakukwepeki maana tumefeli kwa miaka 60. Hata JPM na ukali wote ule alishindwa bandari unadhani nani kwa serikali hii ataweza?

Mfano tu NIDA nmejisajili miaka 5 Sasa Sina NIDA mpaka Leo, hivi wakisema vitambulisho vichapwe na kampuni ya kizungu mtapinga? Tumeshindwa acha tusaidiwe maana hatuwezi.
Nimemuuliza huyo jamaa anayeongelea Ujamaa (China ina mfumo gani) Na Hivi unajua katika top 100 World Performing Companies ambazo zinatokea CHINA 71 percent ni state owned....

Kwahio hapa issue sio kwamba haiwezekani bali tumeshindwa kutokana na wizi / unaccountability; China wana Market Socialism kuna kampuni za Serikali nyie mje na zenu ila kunakuwa na competition (competition hii ndio inafanya state owned companies zisibweteke) Kwahio hata hii DP World ni Mali ya Nani ? Ushajiuliza ?!!! Kwanini na SIsi Tanesco isiende kupeperusha bendera huko Timbuktu ? Ni mtizamo tu (Penye nia pana Njia); Hao Halotel unadhani ni Kampuni ya Nani ?!!
 
Aah mkuu wangu hapa umeteleza, sio tu maendeleo ya china yaliletwa ila mpaka Sasa maendeleo ya china yanategemea mataifa ya nje.

Hivi unafahamu china inashusha thamani ya pesa yake Ili kupata wawekezaji wengi zaidi? haiko sustainable maana Haina strong middle income kulinganisha na US.

Sasa kama wages za china zipo chini unadhani bila investment za nje wata survive vipi?

Ukweli usemwe bila ubepari ulioletwa na Deng Xiaoping hakuna china yenye maendeleo. Kama ni kazi, Mao Alipiga sana kazi na watu walilima sana ila hatukuona uchumi kama huu wa Sasa.
"Sijateleza" popote, na unajua siwezi kukubaliana na hilo wazo la kufikiri China maendeleo yake yanaletwa toka nje.
Ni hivyo hivyo nisivyokubali ujinga huo wa kufikiri maendeleo yetu ni lazima tutegemee uwekezaji toka nje. Hii ni dhana potofu kabisa.

Najua mnapenda sana kukimbilia wazo la kufikiri kwamba watu wanaposema hivyo wanapinga uwekezaji, jambo ambalo siyo kweli

Kuhusu hilo la China kutegemea nchi zingine; unaweza kunipa mfano wa nchi inayojitosheleza yenyewe kwa kila kitu duniani?
Kutegemeana ni jambo la kawaida; lakini kutegemea, kama mnavyokuhimiza nyinyi ndilo tatizo kuu kwetu.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Vipi kuhusu NIDA, ATCL, Huduma duni na slow za Halmashauri, TANESCO, Hospitali za serikali, TBC, TRA n.k nako kubinafsishwe??
Ukiona mtu anauliza swali kama hili maana yake ndio wajinga wenyewe nyie.
 
"Sijateleza" popote, na unajua siwezi kukubaliana na hilo wazo la kufikiri China maendeleo yake yanaletwa toka nje.
Ni hivyo hivyo nisivyokubali ujinga huo wa kufikiri maendeleo yetu ni lazima tutegemee uwekezaji toka nje. Hii ni dhana potofu kabisa.

Najua mnapenda sana kukimbilia wazo la kufikiri kwamba watu wanaposema hivyo wanapinga uwekezaji, jambo ambalo siyo kweli

Kuhusu hilo la China kutegemea nchi zingine; unaweza kunipa mfano wa nchi inayojitosheleza yenyewe kwa kila kitu duniani?
Kutegemeana ni jambo la kawaida; lakini kutegemea, kama mnavyokuhimiza nyinyi ndilo tatizo kuu kwetu.
Ondoa kwanza dhana ya ujamaa kwanza kichwani, hivi unajua zaidi ya 80% ya bandari za US ziko serviced na kampuni za nje? Same to UK Wana service bandari zao na private sector from uarabuni Ili kuongeza ufanisi.

Hata hao china hawakufanikiwa Hadi walipoifungua nchi Yao kuvuta wawekezaji walishusha Kodi, walitenga special economic zones, walishusha thamani ya pesa n.k yote hayo Ili kuongeza uchumi.
 
Haya ndiyo mambo ya upotoshaji mnaotumia kuwafunga macho watu wasiokuwa na uelewa wa mambo.

1. Nani anahoji uwekezaji kwenye bandari kuongeza ufanisi? Kwa nini mnakimbilia huko badala ya kujadili masharti yanayohusiana na uwekezaji huo?
Hizo bandari za Marekani nao waliingia mikataba mibovu kama tunayotarajia sisi kuiingia?
Mazingira ya Marekani ni sawa na haya ya kwetu? Marekani wanazo bandari ngapi?

Hawa DPWorld ujuzi huu wao waliuokota wapi, au uliwashukia tu toka peponi?
Kwa hiyo nasi inatubidi tusubiri hadi hapo tutakaposhukiwa ndipo tuanze kujitutumua kuanza kufanya mambo yetu?
Hiyo itakuwa lini, na kama hao hao DPWorld wanataka tuwategemee wao milele!

Inakuwa mbaya zaidi, viongozi wanaposahau kabisa kushughulikia maswala ya kujenga uwezo wa wananchi wao, na badala yake wanakuwa watu wa kutembeza bakuli kutafuta wawekezaji hata katika mambo tunayoweza kuyamudu wenyewe.

Kwani hapa hatuna sekta binafsi. Wakulima wetu, siyo sektA BINAFSI HADI MTU ATOKE NJE? hUU NAO UTAUITA "uJAMAA"?

2. Hilo la Ujamaa, elewa tu kwamba hakuna nchi yoyote isiyokuwa na ujamaa.
Hii kasumba ya kukariri vitabuni na kuacha kuelewa hali halisi ni tatizo kabisa. Achana na mambo ya Ubepari/Usocialist, hakuna mahali popote mfumo mmoja ndio unaoendesha maisha ya nchi.

Ubepari ulishakufanyia kitu gani wewe binafsi?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hata hao china hawakufanikiwa Hadi walipoifungua nchi Yao kuvuta wawekezaji walishusha Kodi, walitenga special economic zones, walishusha thamani ya pesa n.k yote hayo Ili kuongeza uchumi.
Kwa hiyo kufanya haya ndio "ubepari"?

China amefuata ubepari ndiyo sababu kaanza kupata maendeleo?

Wananchi wake hawakujua lolote hadi ubepari lipoingia China?

Hayo makampuni ya ujenzi yaliyoenea duniani kote toka China, ujuzi wa kufanya kazi zao hizo ililazimu wasubiri ubepari kuingia China?
Walipojenga TAZARA ililazimu wakaazime ubepari kwanza ndipo wawe na uwezo wa kufanya hivyo?
 
Acha kutusumbua hapa! Ingia hata YouTube uone hali ya China ilivyokuwa kabla ya mabadiliko ya Sera aliyofanya Den Xiapoing. Kwa kifupi ilikuwa hohehahe
 
Haya ndiyo mambo ya upotoshaji mnaotumia kuwafunga macho watu wasiokuwa na uelewa wa mambo.

1. Nani anahoji uwekezaji kwenye bandari kuongeza ufanisi? Kwa nini mnakimbilia huko badala ya kujadili masharti yanayohusiana na uwekezaji huo?
Hizo bandari za Marekani nao waliingia mikataba mibovu kama tunayotarajia sisi kuiingia?
Mazingira ya Marekani ni sawa na haya ya kwetu? Marekani wanazo bandari ngapi?

Hawa DPWorld ujuzi huu wao waliuokota wapi, au uliwashukia tu toka peponi?
Kwa hiyo nasi inatubidi tusubiri hadi hapo tutakaposhukiwa ndipo tuanze kujitutumua kuanza kufanya mambo yetu?
Hiyo itakuwa lini, na kama hao hao DPWorld wanataka tuwategemee wao milele!

Inakuwa mbaya zaidi, viongozi wanaposahau kabisa kushughulikia maswala ya kujenga uwezo wa wananchi wao, na badala yake wanakuwa watu wa kutembeza bakuli kutafuta wawekezaji hata katika mambo tunayoweza kuyamudu wenyewe.

Kwani hapa hatuna sekta binafsi. Wakulima wetu, siyo sektA BINAFSI HADI MTU ATOKE NJE? hUU NAO UTAUITA "uJAMAA"?

2. Hilo la Ujamaa, elewa tu kwamba hakuna nchi yoyote isiyokuwa na ujamaa.
Hii kasumba ya kukariri vitabuni na kuacha kuelewa hali halisi ni tatizo kabisa. Achana na mambo ya Ubepari/Usocialist, hakuna mahali popote mfumo mmoja ndio unaoendesha maisha ya nchi.

Ubepari ulishakufanyia kitu gani wewe binafsi?
Umezaliwa mwaka gani kwanza! Maana hapa tunaweza tukawa tunabishana na toto la mwaka 2000 ambalo halijui hata kipindi nchi yetu ilipita stage ya kufunga mkanda
 
Back
Top Bottom