Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Acha kutusumbua hapa! Ingia hata YouTube uone hali ya China ilivyokuwa kabla ya mabadiliko ya Sera aliyofanya Den Xiapoing. Kwa kifupi ilikuwa hohehahe
Wewe utakuwa ni mpuuzi sana. Ninaijua vyema sana hali iliyokuwa nayo Marekani siyo miaka mingi iliyopita. Nimeishuhudia mwenyewe, sikuambiwa kama unavyofanya hapa.

Na bado najua utakuwa huelewi ninacholenga katika kukujibu hivi.

Kila ukiandika unazidi kujionyesha ni kiasi gani ulivyo mtupu kabisa.
 
Umezaliwa mwaka gani kwanza! Maana hapa tunaweza tukawa tunabishana na toto la mwaka 2000 ambalo halijui hata kipindi nchi yetu ilipita stage ya kufunga mkanda
Sina tena lolote la maana ninaloweza kutumaini kulisikia/kulisoma toka kwako.
 
Kuna wakati unaweza kujiuliza hivi ni kweli watu wote wanaopinga uwekezaji wa DP wameusoma mkataba wa makubaliano? Jibu ni jepesi sana, asilimia kubwa ya wanaopinga huenda hawausoma hata huo mkataba. Lakini kwanini watu wapinge tu hata bila kujua vizuri kilichopo kwenye mkataba? Jibu ni jepesi sana, historia ya mikata ya nyuma imewafundisha. Kama mikataba kama ya gas na kupitishwa kwa hati ya dharura Nini ilikuwa hatma yake, nenda kwenye migodi, turudi kwenye Reli na Muhindi, viwanda na wawekezaji tuliona viwanda vikifa. Hayo ndio yamewafanya ht wasiosoma mkata huo kujikuta wanaupinga tu.
 
Kuingia ubia na uwekezaji sio kuuza.
 
Wanaopiga makelele humu JF wengi wao hawajawahi hata kuitoa vespa pale bandarini wakajua ni milolongo ipi iliyopo kikazi.

Wengi ni makasuku wa wenye pesa zao, baadhi wanapewa pesa na wapigaji wa bandari waliozoea maisha ya ubwete ya kupata pesa chafu za mifumo isiyo rasmi.

Serikali ina mkono mrefu, na ikitaka kufanikisha jambo inaloona lina manufaa kwa taifa na itafanikisha tu iwe jua iwe mvua.

Tuna fukwe yenye urefu kilomita 1420, Kenya wanaionea wivu siku zote. Rais Kagame alisema wazi kabisa kwamba akipewa bandari ya Dar hii nchi inakwenda kuwa ya uchumi wa kiwango cha juu.

Samia kaamua kutembelea hoja kama hizi za kina Kagame za kunufaika na rasilimali tuliyopewa na Mungu, hawa wanaopiga hizi kelele upo mwisho wao unakuja.
 
Kuwa controlled na state ndio kumeonyesha kila aina ya udhaifu wa uendeshaji.

Ufisadi na uzembe unaowapa wafanyakazi ile jeuri ya kujua kuwa wanafanyia kazi serikali yao hivyo hakuna baya litakalowakumba.
 
Hilo suala la mishahara yao kuwa pale pale licha ya uvivu wao kazini na wizi wa mali ya umma ndio kichaka cha hawa wengi wanaopinga uwekezaji wa DP.

Wanakuja na sera za kijamaa za kumkumbuka Nyerere wakitaka kazi ifanyike kimazoea pale bandarini, hakuna atakaye kubaliana na upuuzi huo. Wanaletewa mwekezaji mpya mwenye teknolojia za kisasa na kama hawawezi kazi basi wapishe wengine.

Tusifuge umaskini kwa kigezo cha kukimbilia uzalendo na utaifa wetu. Sera za ujamaa za miaka iliyopita zisiendelee kutumika kutetea status quo pale TPA, ni muda wa mabadiliko kuwakumbuka wote wanaofanya kazi kimazoea.
 
Ukiona kila kitu tunashundwa maana yake ofis kuu ndo inashindwa ,na haina haja ya kwepo hapo juu
 
Watu kama wale uwezi kuwaelimisha tena; huko serikalini inatakiwa waseme inatosha. Ni muda wa kufunga huo ukurasa, wengi washaelewa inatosha, waliobaki awataki kuelewa.
Kila kitu kina muda wake, na hiyo kesi waliyofungua hao mawakili inakwenda kutupiliwa mbali huko mahakamani.

Huyo Mwabukusi awe mwangalifu sana na mwenendo wake, yanaweza kumkuta yale yale yaliyomkuta Ulimboka miaka ile ya JK.
 
Umeongea vitu vya msingi sana .sasa mtu kama samia anakula bure anavaa bure .anakula bure kwa kodi zetu , lakini kamwe hawwzi kuumiza kichwa kutatua hayo mambo yeye anapenda vitu virahisi sana
 
Saa100 hata sikumoja hatakaa aingie mkataba wenye maslahi kwetu ,kwa kuwa ni raisi mvivu kuumiza kichwaa chake ,yeye bora liende
 
Usilinganishe uwekezaji wa china na Tanzania. Unajua athari za devaluation kwenye uwekezaji unaofanyika Nchini? Hatunufaiki na uwekezaji ambao dola chache zinawekezwa kuvuna midola mingi kwa wageni huku sisi tunapata pesa kidogo ya kidogo kisa devaluation. Kama tunataka win win wasiwekeze kwa fedha zetu. Waajiri watanzania , walipe Kodi kwa dola, walipe waajiriwa wao kwa dola. Kuna migodi mingi Dhahabu zinabebwa na ndege usiku. Lakini watu wanapiga Cha juu. Mifumo ya uwekezaji kwetu haitulipi kama Nchi. Ni vizuri tuwe na mifumo dhabiti ambayo haitaruhusu ndege kupaa mgodini moja kwa moja kwenda nje. Ukaguzi uwe wakutosha na charging zifanyike kuhakikisha sent ya mtanzania inabaki.
 
Kanywe uji kwanza.
Sera za kijamaa ndizo sera gani hizo?
Nitajie sera mbili tu za Kijamaa Tanzania Ati za kumkumbuka Nyerere...toa peleka Upotoshaji wako sehemu nyingine.
 
Hatujakataa wawekezaji tunakataa aina ya mkataba yaani haueleweki.
Mbaya zaidi mama anawapa wajomba zake urithi wa bara.
 
Wamechukuana na Kina kitenge wakaenda DUBAI alafu wakarudi hela zimejaa mifukoni then siri ikavuja ya mkataba wanatulazimisha tuwaelewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…