Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Umeanza vizuri sana, ila hako kakipengele mnakosema Watanzania hawataki uwekezaji mnakosea sana, nyinyi ndio mnakuwa wapotoshaji kuliko hata hao mnaowaita wapotoshaji., njaa zenu na ujinga wenu unarigharim taifa.
 
Kanywe uji kwanza.
Sera za kijamaa ndizo sera gani hizo?
Nitajie sera mbili tu za Kijamaa Tanzania Ati za kumkumbuka Nyerere...toa peleka Upotoshaji wako sehemu nyingine.
Alafu mtu anapinga Ujamaa alafu anatoa mfano wa China....; Ndio maana nikawauliza mashirika mangapi yanayofanya kazi vizuri duniani ni state owned ?

Watu wanashindwa kujua practically hakuna Socialism au Capitalism ni mixed economies na China mfumo wake ni Market Socialism..., Na kama unaongelea welfare huenda hata USA kuna welfare programs kuliko hata huku (Food Stamps, Council Houses, Minimum wages Law n.k.); Watu wanashindwa kuelewa haya mambo ni kama recipe unachukua huku na kule kulingana na mazingira yako.... Ni features za Socialism ndio zimeipa capitalism a Human Face...

Tukichukulia mfano wa China Market Socialism au Capitalism (ambapo issue kubwa ni ushindani competition) Sijui hawa walioleta hii Mada wanasema nini kwa kumpa DP World Exclusivity hapo Competition inatoka wapi ?!!!
 
Kanywe uji kwanza.
Sera za kijamaa ndizo sera gani hizo?
Nitajie sera mbili tu za Kijamaa Tanzania Ati za kumkumbuka Nyerere...toa peleka Upotoshaji wako sehemu nyingine.
Kumtafuta Prof Shivji mwenye kuamini katika masuala ya ujamaa ni ujamaa wenyewe huo, anakuja na kudai kuwa mkataba haujaandikwa popote eti sisi tunapata nini.

Kasahau kuwa ile ni framework tu, ni skeleton tu na inachukua yale ya msingi pekee. Hata kudai kuwa mwarabu anataka kupewa nchi ni sehemu ya hulka za kijamaa zenye lengo la kujenga hoja ya kumkwepa adui bepari, yale yale mambo ya kupinga unyonyaji ya hayati Baba wa Taifa.

Kwa sasa hivi hiyo ni mindset iliyopitwa na wakati. Tuna dunia yenye kutazama maslahi mapana ya nchi yanaweza kufanikishwa vipi, kuna suala la bima za afya zenye kuhitaji kuongezwa ubora kila kukicha.

Kuna suala la elimu za wanafunzi kuanzia wa shule za msingi mpaka vyuo vikuu zenye kuhitaji kuhudumiwa kila kukicha, kuna suala la kumalizia miradi aliyoiacha hayati JPM na kuanza mipya.

Yote hayo yanataka pesa ili yaweze kufanikishwa. Na sehemu ya ubunifu wa kupata pesa nyingi ni kupitia ufanisi wa bandari inayoendeshwa kisasa yenye gharama ndogo za kutoa huduma na tija nyingi na ya haraka kwa wateja wanaoitumia.
 
Ila wachina hawakuingia mikataba mibovu na pia rushwa kule adhabu ni kifo.
 
Kiuhalisia huu ubepari tunaouona ndio Ujamaa.
 
Kiuhalisia huu ubepari tunaouona ndio Ujamaa.
Kama People's welfare zinashika hatamu far and farmost na sio profit at all costs hio ndio socialism yenyewe.....,

Kama kampuni zinalazimishwa ziuze shares kwa kila Tom, Dick and Harry; Mishahara unapangiwa ulipe ngapi na mtu afanye kazi masaa mangapi.... Hio huwezi kuita Market Forces hata siku Moja....

Watu wana-equate Ujamaa na Umasikini au Ujamaa na Police State au Ujamaa na kila jambo baya...; Wanashindwa kuelewa kule Marekani mabenki yalivyofirisika Kodi za Mwananchi zika-take over ili kuwakomboa sijui huo ndio Ubepari wenyewe !!??? UK National Health Insurance; Na watu wanapigwa kodi balaa lakini kila kiumbe akiugua yupo covered kwa afya (Sasa huo Bepari wa kweli angeuita Legalized Robbery AKA Robbing the Rich to Feed the Poor).....

In short its Total Confusion and people choose to believe what they want to believe Ingawa Hakuna Duniani a 100 percent Capitalistic State na kama Issue ni State Owned - katika Makampuni Duniani yanayofanya vizuri na yametokea China majority ni State Owned..., Hivi hii Halotel iliyopo huku ni mali ya nani kama sio State Owned ? Hata hio Dubai, tofauti tu ni kwamba mali ya Taifa inamilikiwa na watu / familia / masultani ukiangalia kwa jicho la kwamba Sultanate ndio state yenyewe basi hata DP World ni State Owned...
 
Kumtafuta Prof Shivji mwenye kuamini katika masuala ya ujamaa ni ujamaa wenyewe huo, anakuja na kudai kuwa mkataba haujaandikwa popote eti sisi tunapata nini.
Nani huyo aliyeenda kumtafuta Profesa Shivji? Serikali ya Tanzania? Manake tukizungumzia sera tuna maana na Sera iliyoridhiwa na Serikali au inayofuatiliwa na Serikali...wewe umeona wapi Serikali imeenda kumtafuta Profesa Shivji kwenye shauri hili? Unaendeleza upotoshaji tu! Unawezaje kusema Profesa anadai Mkataba haujaandikwa.

Eh bwana eh ni jibu swali langu....
Sera za kijamaa ndizo sera gani hizo?
Nitajie sera mbili tu za Kijamaa Tanzania?
Irrelevant
Kwa sasa hivi hiyo ni mindset iliyopitwa na wakati. Tuna dunia yenye kutazama maslahi mapana ya nchi
Hayo juu ni Matusi tu kama yalivyokuwa matusi ya bandiko kuu la mada....Hivi unafikiri Watanzania wanahitaji watu wakuja kuwaelekeza namna ya kutafuta masilahi yao...
yanaweza kufanikishwa vipi, kuna suala la bima za afya zenye kuhitaji kuongezwa ubora kila kukicha.
Irrelevant
Kuna suala la elimu za wanafunzi kuanzia wa shule za msingi mpaka vyuo vikuu zenye kuhitaji kuhudumiwa kila kukicha, kuna suala la kumalizia miradi aliyoiacha hayati JPM na kuanza mipya.
Irrelevant
Yote hayo yanataka pesa ili yaweze kufanikishwa.
Aha Masuala yanayohitaji Pesa! Kwanini usiwashauri waanze kwa kupunguza matumizi yasiyo na umuhimu....mfano mdogo wa hayo Ma V8
Na sehemu ya ubunifu wa kupata pesa nyingi ni kupitia ufanisi wa bandari inayoendeshwa kisasa yenye gharama ndogo za kutoa huduma na tija nyingi na ya haraka kwa wateja wanaoitumia.
Ufanisi wa kuwatupilia mbali Wafanyakazi...au?

Wacha hizo, hii ni Nchi inayojitambua, haya matusi yenu hayata wafikisha popote. Amini hivyo.

Jibu maswali yangu
Na umwache kumtumia Raisi J.K. Nyerere.(R.I.P) kueneza upotoshaji...mpe heshima yake na uandike yale yaliokweli
 
Sera za kijamaa ni zile zenye kuona uwekezaji mkubwa bandarini kama vile ni kurudisha utumwa katika karne hii. Kuamini katika serikali kubwa inayojaa urasimu mwingi ni kuendeleza sera za kijamaa.

Tusipoteze muda mwingi, siku sio nyingi kunakwenda kusainiwa mikataba kati ya DPW na wadau wa masuala ya biashara na utakuwa ni mwanzo wa mapinduzi ya kiuendeshaji hapo bandarini.

Hizi tantalila nyingi hazina maana. Zaidi ya uwekezaji mkubwa kufanyika bandarini na kubadili kabisa mitazamo ya kizamani inayosumbua vichwa vyetu.
 
Ulianza vizuri, ila kwenye bandari tatizo Siyo uwekezaji Bali ni masharti ya mkataba.
 
Ulianza vizuri, ila kwenye bandari tatizo Siyo uwekezaji Bali ni masharti ya mkataba.
 
Ndio china chini ya ujamaa ilifeli kabisa under Mao Zedong ila uchumi umekua mkubwa baada ya kukubali kuachana na ujamaa na ku embrace ubepari yaani wakaruhusu nyenzo za uchumi zishikiliwe na watu binafsi.

Deng alifungua nchi wakaja mabeberu kutoka magharibi ndio wakajaza viwanda huko China na mwishowe china ikafunguka kwa Dunia.

Nimeshakueleza hata Dp world Kuna bandari za china na Hong Kong wamepewa kuziendesha alafu unatumia mfano wa china kupinga mwekezaji kupewa bandari Dar? Are you serious?

Ona North Korea au Cuba ni failures sababu ya kung'ang'ania ujamaa na kuona kama private sector ni Wezi.

Mjadala wetu uwe juu ya mkataba wenye maslahi ila sio kupinga mwekezaji kwenye bandari. Sasa kama tumeshindwa chini ya CCM kwa miaka 60 muujiza Gani huo utatusaidia bandari iwe na ufanisi ghafla.
 
Usijaribu, narudia, Usijaribu Uzalendo wa Mtanzania. Usifikiri watu wamelala nchi hii.
Tatizo ni hizo fursa anazopoteza wakati majirani wanataka kuitumia bandari yake.

Anajaziwa ujinga mwingi mtanzania wa kawaida na kupoteza hata akili ndogo ya kushindwa kuyaelewa masuala ya kawaida yenye kumhusu yeye na hatima ya maisha yake.
 
1. Nani anahoji uwekezaji kwenye bandari kuongeza ufanisi? Kwa nini mnakimbilia huko badala ya kujadili masharti yanayohusiana na uwekezaji huo?
Hizo bandari za Marekani nao waliingia mikataba mibovu kama tunayotarajia sisi kuiingia?
Nani anaunga mkono haya makubaliano kama yalivyo? Mimi napinga wanaosema bandari eti isiendeshwe na mwekezaji wao hawajali mkataba uwe mzuri au vipi wao hawataki KABISA mtu asiye mTanzania kuendesha bandari.

Ndio nimesema kama NIDA tu tumefeli kuchapisha tu kitambulisho hivi Leo hii hiyo tender akipewa Microsoft tuandamane eti nchi imeuzwa?

CCM imefeli Sasa kwa miaka 60 kufanya mambo basic kabisa, mzigo wa siku 5 unatumia siku 30 kutolewa Tena mpaka uhonge alafu unatoka povu eti iendelee kuendeshwa na TPA? hivi tupo serious kweli?

Kama tumefeli basi tusaidiwe maana hakuna namna Sasa.
 
Ukiona kila kitu tunashundwa maana yake ofis kuu ndo inashindwa ,na haina haja ya kwepo hapo juu
Hata huu mjadala ni maamuzi ya ofisi kuu, tungeweza kuona wanasaini tu mikataba pale ikulu wakiwa wamevaa masuti na tukaishia kupiga makofi.

Tusiidharau ofisi kuu.
 
Ndio waliingia kwenye social market economy ambapo Kuna soko huria ila makampuni mengi ya serikali nayo Yana compete humo na sio eti monopoly ya serikali kwenye Kila biashara.

Na ndio maana 70% ya GDP huko China ikawa kwenye sekta binafsi yaani makampuni binafsi whether ya wachina au wawekezaji kutoka nje.

Nchi inaweza kuwa na wachapa kazi na wasomi ila wakakosa mitaji na teknolojia ila kupitia wawekezaji ndio Sasa wachina nao wakaiba teknolojia (Hili unalojua) na kujifunza teknolojia maana Moja ya sera ilikua ni kwamba ukifungua biashara china basi ni lazima uta disclose teknolojia Yako kwa serikali after 3 years lakini pia ujenge uwezo kwa wachina waweze endesha taasisi na sio kuajiri tu expatriates.

So mtaongea mengi ila Mao was a failure kiuchumi hasa baada ya janga la Great leap forward but Deng ndio alijenga uchumi unaouona Sasa kwa kuruhusu sekta binafsi ikamate nyenzo za kiuchumi.

Na ndio maana hapa tunapoongea DP World na makampuni mengine yamepewa tender za kuendesha bandari huko China.
 
Aah mkuu wangu hapa umeteleza, sio tu maendeleo ya china yaliletwa ila mpaka Sasa maendeleo ya china yanategemea mataifa ya nje.
Hakuna taifa ambalo ni kisiwa kila taifa linategemea pengine Dunia ni Moja; Huwezi kutegemea nchi ipo Jangwani au kisiwa kidogo alafu kijitosheleze kwa chakula; wanafanya wanachoweza na mengine wanaagiza (Global Trade) ndio maisha hayo hata wewe kwenye nyumba yako huwezi kujitosheleza unategemea wengine....
Hivi unafahamu china inashusha thamani ya pesa yake Ili kupata wawekezaji wengi zaidi? haiko sustainable maana Haina strong middle income kulinganisha na US.
Hapana china is a producing country kwahio kushusha thamani yake ya pesa ni ploy bidhaa zake zinakuwa cheaper kuliko mataifa mengine hence watu kuendelea kununua sana kwao unaongelea china haina Soko ?!!! Hivi unajua population ya China ? (wewe mihogo yako ikipendwa na wachina wakainunua sana you are sorted) USA anamtegemea China anunue Soya sio kwamba hawezi kupata pengine (ndio maana Trump alikuja juu kwamba tunanunua zaidi from China kuliko wanavyotuuzia) ila hakujua mzizi wa fitina ni working ethics ya wachina (they work harder, cheaply and faster) unadhani hata Iphone na makampuni mengi kupeleka assembly zao China ni sababu ya kuwaogopa ? (Nope they Deliver !!!)
Sasa kama wages za china zipo chini unadhani bila investment za nje wata survive vipi?
Ndio maana juzi hapa kuna mtu alikuwa anaequate umasikini wa mtanzania na dollar amount nikwambia anapotoka; Kuna mdau kijijini hata laki kwa mwaka hapati ila kwa elfu ishirini tu anakula bata (gongo na kucheza ngoma) mwaka mzima huyu jamaa anakula milo mitatu ukiwa Dar hio laki hata usafiri tu huenda isitoshe (wakati huyu mdau anatembea)...; usiongelee wages ndogo ungelea sustainable income....
Ukweli usemwe bila ubepari ulioletwa na Deng Xiaoping hakuna china yenye maendeleo. Kama ni kazi, Mao Alipiga sana kazi na watu walilima sana ila hatukuona uchumi kama huu wa Sasa.
China sio Mabepari China wana Market Socialism....; Narudia tena Duniani hakuna 100 percent Ubepari wala 100 percent Socialism kuna Mixed Economies...; Labda nikuulize Ujamaa ni nini na Ubepari ni nini (Je ni Kampuni kuwa state owned) ? Je ni market forces ? na Socialism ni welfare au ni Uzembe, Police State, na kutokuwajiba ? Ukijibu hayo nadhani utaanza kuanglia mambo practically na sio nadharia za kwenye makabrasha....
 
DPW sio tu kapewa tender huko China, kakamata biashara za Congo na Rwanda na yeye ndio chanzo cha kujengwa kwa reli ya SGR ili ije ipitishe mzigo mpana wa transit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…