Ujinga, Umaskini na Maradhi ni mtaji mkuu wa wanasiasa wa Tanzania


alafu we vp? we ni wa buku saba nini
 
Mwaka mambo mapya, buku 10 kwa saa 1 siku hizi, hujuwi tumeingia mwaka wa uchaguzi? Kalagabaho.

Ukiona chama kimefikia hatua ya kuajiri vichaa wakukitetea badala ya kufanya mambo ambayo yatafanya jamii ikitetee kwa mazuri yake.we jua chama hicho kinapumulia mashine.
 
juhudi za Mtu binafsi ni MUHIMU. Lakini nafasi ya VIONGOZI ni ya nini?
 
Mada hapa ni tatizo kwa WANASIASA kuwekeza kwenye ujinga , umaskini na maradhi! Swali Je tuondokane namna gani na tatizo hili? Kama watu hawajali KANUNI , taratibu, sheria, na hata kuheshimu maamuzi ya wananchi huko ni kuwekeza kwenye ujinga wetu. Kama tunahonga na kufanikiwa malengo yetu. Huko ni kuwekeza kwenye umaskini wa watu. Hatua gani zichukuliwe tuanze kuthamini utu wa mtu na kuheshimu waliowachagua na kufanya maamuzi kwa MISINGI ya HAKI ?
 
juhudi za Mtu binafsi ni MUHIMU. Lakini nafasi ya VIONGOZI ni ya nini?

Kuongoza.

Katika kanuni za kukubali kuongozwa ya kwanza ni kuwa kiongozi halaumiwi. Ndiyo maana mimi hupenda kuwa kiongozi na sipendi kuongozwa.
 

Ndiyo maana nikasema, unangoja mtu akuchukulie hatua kwa ujinga wako?

Kama tunaongelea uongozi Tanzania, kiongozi mkuu wa mwisho ni Jakaya Kikwete, na naam, Kikwete hakuna mahala unaweza mtoa dosari katika uongozi wake ukilinganisha na wa kabla yake, kama papo hebu leta tupachambuwe.
 
Mtaji wa ccm, nape aliwauliza watu tanga eti mnataka maji au katiba, wale watu wakajibu majiiiiii....! Mnataka barabara au katiba, wakajibu barabaraaa..! Umeme au katiba, umemeeee! Katiba itawasaidia nini nyie watu hakunaaaa.....! Kama si uenda wazimu ni nini?
 
Siku zote MTU yeyote asifurahie kisiasa kuchaguliwa na mtu mjinga asiyejua kwa nn anakuchagua,kesho huyo mtu mjinga kutokana na ujinga wake anaweza kumchagua kichaa kuwa kiongozi na utamlaumu lkn sio kosa lake ndivyo alivyo andaliwa kufanya hivyo.

Ndio maana tunaona kwa macho yetu viongozi wengi wawakilishi wa watu (WABUNGE)wanaishi Dar es salaam kwa sababu wanajua waliowachagua ni mambumbumbu mablanketi kumi na hata wasipoenda kabisa majimboni mwao ukifika wakati wa uchaguzi watachaguliwa tena,viongozi wa namna hii watambue kuwa wanachofanya ni UNYAMA uliopitiliza usio na chembe ya huruma kwa watu waliomwamini.

Serikali ina jukumu zito la kuwapa watu ELIMU ili kujenga utambuzi wa kwa nini wachague viongozi,na lipi jukumu la viongozi kwa maslah mapana ya watu na TAIFA kwa ujumla ili kuleta maendeleo kwa haraka zaidi kama zilivyo nchi nyingine duniani.
 
maisha bora ama bora maisha?? nazani ni bora maisha!!! maisha bora ni wezi wa ESCROW.
 
Siku zote MTU yeyote asifurahie kisiasa kuchaguliwa na mtu mjinga asiyejua kwa nn anakuchagua,kesho huyo mtu mjinga kutokana na ujinga wake anaweza kumchagua kichaa kuwa kiongozi na utamlaumu lkn sio kosa lake ndivyo alivyo andaliwa kufanya hivyo.

nimekuelewa kabisa.
 

mungu aliye hai akulinde sana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…