Hatua zinahusu nini?
Fanya bidii yako binafsi kushindana na yote hayo yatakuondokea. Unangoja mtu akuchukulie hatua kwa ujinga wako?
Nyie ndiyo mnawaponza wasiojuwa Kiswahili vizuri, wanaanza kupiga hatua kutoa Geita sijui wapi huko wanajuwa wakifika Ikulu kila kitu safi, wakaishia rumande.
Bidii ya mtu mmoja mmoja humaliza matatizo yake binafsi, tunamaanisha kuwapa lishe bora, kuwapa elimu na maradhi bora watu wa familia husika... Elimu bora ni shule na vyuo bora...... shule na vyuo bora sio mali ya muhusika ila ni mali ya Serikali na taasisi fulani..... na ukumbuke huyu mtu hulipa kodi nyingi sana ili apatiwe zile huduma ambazo ni public kwa gharama nafuu na kwa misingi ya taifa husika ili lijengwe na watu husika. Kama huyu mtu anatakiwa ajibidiishe na afanye kila kitu mwenyewe basi hakuna haja ya kuwa na serikali wala watu kukatwa kodi kwani hapa kila mtu atajibidiisha mwenyewe na kuwa na serikali yake ili ajilinde, aiishi kwenye nyumba bora akiwa na solar yake au generator yake full time, huyu mtu atachimba kisima chake mwenyewe na kutreate maji yake kwa sulphur/mawe/shabu, huyu mtu atanunua gari la 4*4 ili apite kwenye barabara mbovu ( wazungu watatuletea tu magari na meli zao za michangani kwani tutakuwa hatuna bandari)... kama wanachukua kodi zetu na wanaweka kodi kwenye bidhaa na tunalipa, wanakusanya kodi kwenye viwanda na wanataka tujibidiishe ili tumudu zile public service ambazo ni makukumu yao basi wasichukuwe kodi zetu, kila kitu kisiwe na kodi na tusiwe na serikali ili kila mtu ajiongoze mwenyewe...
Mwananchi anamajukumu yake na Serikali ina majukumu yake,,, kazi ya mwananchi ni kufanya kazi, kulipa kodi na kuangalia familia yake na yeye mwenyewe.. kazi ya Serikali ni kutawala watu wote, kukusanya kodi na kuzifanyia kazi stahiki kwa maendeleo ya nchi,,, sasa kama unataka mwananchi kufanya kazi ya serikali mfano kujenga maabara basi haina haja ya kuwa na serikali....
Mwananchi anaweza kujibidiisha akawa na hela/utajiri na akalipa kodi lakini akiugua hospitali hazina madawa, shule hazitoi elimu bora na maeneo mengine hazipo, umeme hauwaki, barabara hazipitiki na maji hakuna sasa hapo nani atakuwa ameshindwa kazi SERIKALI /MWANANCHI...
DADA FAIZAFOX HAMNA NAMNA YAKUITOA CCM KATIKA UMASIKINI WA TANZANIA NA WATANZANIA KWA UJUMLA MAANA WANAKUSANYA KODI NYINGI KILA MAHALI,, MISAADA KWA WAHISANI, KODI KWENYE MADINI HALAFU WANASEMA WATU WAJIBIDIISHE WAKATI 85% YA KODI INATOKA KWA WANANCHI.....SASA SIJUI WANGEKUWA HAWAJIBIDIISHI HIYO KODI INGETOKA WAPI???
HIVI DADA UPO TANZANIA KWELI HAPA NA UNAONA YANAYOTOKEA PHYSICALLY AU UNAONGEA TU NA HUIJUI HALI HALISI YA HUKO NAMANYELE, ENDASAKI, ENDAGAW, UJIJI, MASUMBWE, KATORO, NK??