Uchaguzi 2020 Ujio wa Tundu Lissu utatufanya tukapige kura

Uchaguzi 2020 Ujio wa Tundu Lissu utatufanya tukapige kura

nditolo

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
3,731
Reaction score
4,271
Tundu Lissu ndio tumaini pekee la sisi wanyonge kukombolewa. Ni yeye pekee anayeweza kwa mara nyingine tukaamka vitandani asubuhi kwenda kupanga foleni kwa ajili ya kupiga kura kama tulivyofanya 2015. Tulipiga kura 2015 kwa matarajio kuwa mzee Lowassa atasimamia mabadiliko tuliyokuwa tukiyahitaji kwa miaka mingi.

Ujumbe kwa CCM na polisi yenu ni kuwa Mzee Kikwete kwa miaka yake 10 alijenga barabara na madaraja mengi nchi nzima lakini hakuifanya iwe turufu maana alikuwa akijuwa kuwa hata huku ujerumani wakati wa Hitler, kulijengwa miundombinu na viwanda vingi lakini uuwaji alioufanya kwa watu haukuhalalisha yeye kubaki madarakani.

Tundu Lissu tunakujuwa sana njoo nyumbani ili maovu yawe wazi, tumeumizwa sana, watu wengi wamepotezwa sana. Katiba mbovu wanufaika ni wanaojipendekeza tu na kwenda huko lumumba na ajira zipo lumumba tu.

Kama uliweza kuwatetea watu mahakamani huko Tarime Nyamongo, Geita, Ulyankulu, Kahama na kila walikoonewa, hakika ni shetani pekee anayeweza kukunyima kura.

Lissu njoo wafanyakazi wamenyanyaswa sana, wamepuuzwa sana, wamedhurumiwa sana bado wana mishahara ya Jakaya.

Tulikuombea umepona.

Waliotaka kukuuwa walikufukuza ubunge na kukukata mshahara yote hiyo ilikuwa ni kuhakikisha hauponi tu. Sasa aibu yao.

Lissu njoo tutakuja kukupokea hapo JNIA.

Lissu ni TUMAINI JEMA
 
Hizi pirika za sasa hivi ni sawa na sherehe za wanyama wengine wote kasoro Simba aliyejeruhiwa! Huyo akitia timu, sherehe hiyo inakuwa ya tofauti kabisa 😀
 
Mapokezi yake hiyo jumatatu, yatasababisha watu kutokuwepo kazini. Tutaenda kumpokea mkombozi wetu. Tumeishi maisha magumu sana, maisha ya vitisho, kuonewa, kupuuzwa bila utaratibu.

Lissu njoo aliyesimamia upigaji risasi ameondolewa kwenye nafasi yake. Kifupi hana ulinzi, kule kwetu kuna mtu anaitwa KIBHUMBA anaweza kukulipia kisasi kwa gharama ya bia mbili tu za Calsburgh
 
Mzee baba Ana wasiwasi Sana, ukisikiliza hotuba zake kwa makini utagundua anahofia uchaguzi

Tena hautaki kabisa, ama ikibidi uwepo yeye asishindane na mtu. Na wanaccm wenzake wameshajua kuwa jamaa anaogopa ushindani, ndio maana kila mwanaccm akija na uzi humu jukwaani, ni aidha Magufuli awe mwenyewe, au Lisu aende segerea. Kimsingi anajua yote hadi aliyoyafanya toka awamu hii ikae madarakani yatawekwa wazi, na hayuko tayari kwa hilo.
 
Ni rahisi kwa Tz kuitawala Marekani kuliko Magufuli kuanguka 2020!

Ni kweli kabisa, lakini ashindane, tena sio kushindana tu, bali ashindane kwa haki. Tena ashindane na Lissu.Hapo ndio tutaona uwezo wake, na kura zake halisi. Kama atalogwa akubali ushindani wa haki, uchaguzi huu hata akishinda utamuacha na fedheha sana, na mambo mengi atabidi atekeleze hasa maendeleo ya watu, na kuheshimu demokrasia. Kubwa zaidi kuliko yote, ushindani huu utamfanya iwe ngumu kwake kubadili katiba ili akae madarakani zaidi ya miaka 10.
 
Ukweli mbaya, Tundu Lissu ndio mgombea pekee wa upinzani anayeweza kutufanya tukapige kura. Kama mgombea hatakuwa Tundu Lissu, ni ngumu sana wapiga kura wa ukweli wa upinzani kujitokeza kupiga kura.
 
Back
Top Bottom