KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Kwa kuanzia, kazi hii aliyoifanya huko nyuma, na ambayo watu wengi hawaifahamu, inafaa itengenezewe namna ya kuieneza hata kabla ya kampeni hazijaanza.Kama uliweza kuwatetea watu mahakamani huko Tarime Nyamongo, Geita, Ulyankulu, Kahama na kila walikoonewa, hakika ni shetani pekee anayeweza kukunyima kura.
Tundu Lisuu amedhalilishwa sana na wapuuzi, kwa kupachikwa neno 'Msaliti'. Hili linatakiwa lifutwe kabisa kwa kuonyesha kazi ngumu sana aliyokuwa akiifanya katika kuwatetea wanyonge hata kabla ya kuwa ndani ya siasa.
Kazi ya kutengeneza namna na kueneza habari hii inapaswa ifanyike kitaalam kuvuta hisia za mwanchi wa kawaida awali kabisa ya kampeni.