Ujue uchaguzi wa Marekani (USA) na jinsi rais wake anavyochaguliwa

Umeamua kung'ang'ana na usichokijua muda si mrefu utaumbuka hongera lakini kwa kuonyesha msimamo wa kusimamia kile usichojua
 
Kwa Tanzania umekosea, mshindi wa rais ni yule anayepata kura nyingi bila kujali amepata asilimia ngapi hii ni baada ya kipengele Cha asilimia 50+ kuondolewa
 
Lakini Electoral College imeshatoa Marais watano walioshindwa Popular vote wa karibuni wakiwa George Bush na Trump.
Kuna kitu hakjakiweka sawa katika maelezo yake ndio maana hata wewe umeingia wasiwasi ukauliza swali lako. Kwa ninavyofaham mimi raisi hupatikana kwa kura 270+ za delegates ambao yeye kawaita mabwanyenye. Lakini hizi kura hupatikanaje? Kila Jimbo la marekani Kati ya hayo 50 Lina Idadi ya delagates wake. Mgombea akishinda popular votes za Jimbo husika, anapewa kura zote za delegates kwa Idadi yao kwenye hilo jimbo. Na kwa sababu majimbo yanatofautiana winginwa delegates mgombea anaweza kushinda kwa gepu dog tu kwenye majimbo yenye delagates wengi na akashindwa mbali mno kwenye majimbo yenye delagates wachache kiasinkwamba ukijumlisha popular votes mgombea huyo anakuwa amepata kura nyingi lakini delegates wachache Hivyo anakuwa ameshindwa na mtu mwenye popular votes chache

Mfano majimbo A, B na C. Jimbo A linawapiga kura 13 na delegates 2, Jimbo B wapiga kura 20 delegates 3 na Jimbo C Lina wapiga kura 50 na delegates 6. Mgombea X akapata kura 11 za Jimbo A, kura 16 za Jimbo B na kura 23 za Jimbo C. Mgombea huyu atakuwa amepata popular vote 50. Wakati huo huo mgombea Y kapata kura 2 za Jimbo A, kura 4 za Jimbo B na kura 27 za Jimbo C, Hivyo atakuwa na jumla ya popular votes 33.

Kwa kigezo cha popular votes, mgombea X atakuwa na kura 50 wakati mgombea Y ana kura 33.

Tukirudi kwenye delagates, mgombea X kashinda majimbo A na B na Hivyo kujipatia Kura 2 za delegates wore wa Jimbo A na kapata kura zote 3 za delegates wa Jimbo B, Hivyo anakuwa na jumla ya kura 5 za mabwanyenye.

Kwa upande wa mgombea Y, kashinda Jimbo A na B hivyo Hana kura youote huko ila kashinda Jimbo C lenye delegates 6. Hivyo kwakuwa Katina ya marekani inamtambua mshindi kuwa ni yule mwenye kura nyingi za delegates basi mgombea Y ndio atakuwa mshindi
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri Sima70
 
Electoral college votes zinapatikana baada ya mgombea kushinda popular votes nyingi kwenye uchaguzi hivyo kila jimbo linatoa mgombea wa chama chama ambacho mgombea husika amepata kura nyingi

Kuna majimbo makubwa yana watu wengi kama Frorida ukisha huko popular votes unapata idadi kubwa ya wajumbe watakao kupigia kura ya electoral college votes
 
Very thank you
 
Lakini Electoral College imeshatoa Marais watano walioshindwa Popular vote wa karibuni wakiwa George Bush na Trump.
Kweli tupu unaweza shinda popular votes ukashindwa kwenye electoral college votes ukapoteza nafasi
 
Uko vizuri wewe jamaa hongera kwa ufafanuzi mzuri
 
naomba jawabu kati ya donard trump na hilal Clinton nani alipata kura nyingi kimajimbo usemavyo na akatangazwa RAIS wa marekani?
Hilal Clinton alipata kura nyingi za wananchi Donald Trump akapata kura nyingi za majimbo kwa kuwa yeye alishinda yale majimbo nyeti yanayotoa wajumbe wengi wa electrol Votes ndio maana alitangazwa mshindi kipindi hicho
 
Uko vizuri mdogo wangu
 
kwa kuwa yeye alishinda yale majimbo nyeti yanayotoa wajumbe wengi wa electrol Votes ndio maana alitangazwa mshindi kipindi hicho
Majimbo hayo siyo nyeti au muhimu eti kwa vile yana wajumbe wengi. Umuhimu wake ni kwamba yana wapiga-kura shindani kwa vyamba vyote; mgombea fulani akizubaa kidogo tu basi inakula kwake.

Nevada ina electoral votes 6 na Wisconsin 11. Haya mawili ni majimbo ya ushindani. Kwa upande mwingine New York (28) na California (54) hayamo kwenye kundi hilo la majimbo nyeti, licha ya wingi wa electoral votes.
 
Kwa nini sasa New York na California hapo kwenye ushindani?
 
Kwa nini sasa New York na California hapo kwenye ushindani?
Kwa sababu ni ngome ya chama cha Democrats. Wapiga-kura wengi ni wa huo mrengo wa kushoto.

Lakini yale majimbo saba (Arizona, Georgia, Michigan, Nevada, North Carolina, Pennsylvania na Wisconsin), yenyewe yana takriban idadi sawa ya wapiga-kura kwa vyama vikuu shindani.

Au kwamba wapiga-kura wake hawafungamani na chama chochote - wanazingatia maslahi mapana ya taifa lao. Kwa hiyo jinsi wanavyoshawishiwa kisera ndivyo wanavyopiga kura. Ndiyo maana Trump kakomba hayo yote awamu hii.

Hii ni tofauti na majimbo ambayo ni ngome (ama ya Democrats au Republicans), ambapo hata sera ziwe mbaya mbovu kiasi gani, wao wataimba ngonjera ileile: ^sisi tumeipenda wenyewe; na wavimbe wapasuke...!^
 
Asante mkuu kwa darasa lakini sasa kama majimbo hayo yanatoa wajumbe wengi wa electrol votes si zingembeba mgombea huyo wa Democrats akishinda popular votes?
 
Asante mkuu kwa darasa lakini sasa kama majimbo hayo yanatoa wajumbe wengi wa electrol votes si zingembeba mgombea huyo wa Democrats akishinda popular votes?
Ndiyo zimembeba sana. Kwani huoni Kamala alipiga hadi 226?

Angeshinda pia majimbo mengine matatu tu (North Carolina-16, Pennsylvania-19 na Wisconsin-10) katika yale 7 ya ushindani, angefikisha electoral votes 271. Hivyo angetangazwa kuwa mshindi wa urais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…