Nijuavyo
Wabunge = 435(kutoka kwenye kila jimbo kulingana na idadi ya watu)
Maseneta = 100(wawili kutoka kwenye majimbo 50 bila kujali idadi ya watu)
Washington DC = 3(Sheria ya 23 ya mwaka 1961, inawapa Nafasi 3 za ma electors japo sio Jimbo)
Juma Wajumbe = 538.
Kila chama kabla ya uchaguzi kinachagua Wawakilishi(Electors)wake katika majimbo yao ya kiuchaguzi, baada ya hapo wanasubiri uchaguzi wa Popular votes.
Wananchi wakipiga kura kumchagua Raisi technically wanawachagua pia ma Electors wao kulingana na Chama.
Kwahio katika jimbo Mkiongoza kura za Raisi, basi na jimbo hilo mnabeba nafas zote za ma electors...
Yaani kwa mfano California, Democratic akishinda Popular votes,
Basi na wajumbe wake wote 54 wanakua wamepita kupitia kura za raisi.
Hivyo basi, inabidi uwashawishi wananchi wakupigie kura, ili ushinde jimbo flani, uchukue viti vyote vya ma Electors hatimaye ufikishe 270 ambapo unakua mshindi,
Hiihaijalishi idadi ya kura za wananchi umepigwa(hii inawezekana kwa kuchaguliwa na wananchi wengi kutoka majimbo machache eg California, Texas, Florida, NY) mwenzako akachaguliwa na wananchi wachache katika majimbo mengi ambapo jumla ya ma electors ikazidi ya wale wa majimbo ya watu wengi).
Kwa hio basi, hakikisha wananchi wengi wanakuchagua, LAKINI ZAIDI kutoka maeneo(majimbo) MENGI TOFAUTI,
Bila kusahau majimbo yenye wapiga kura wengi yana faida ya kupata Ma electors wengi kwa mkupuo.
Mfano ukishinda majimbo 12 yale yenye watu wachache, Mwenzako akishinda California tuu, amekupiga.