Nadhani mleta mada kuna nanna haufahamu uchaguzi wa USA kiuhalisia, ni kama umekaririshwa fulani au ameandika kinadharia mnoo hata kama alichokiandika kuna chembechembe za ukweli.
Kwa kifupi sana, mfumo wa uchaguzi wa USA kumpata raisi wake huamuliwa na wamerekani wenyewe kwa wingi wao na wala sio kweli kuwa mshindi huamuliwa na wajumbe wa Electoral college! Ukishinda Popular votes katika majimbo mengi na muhimu zaidi basi wewe tayari ni mshindi. Kura za wajumbe wa Electoral college ni hitimisho la mchakato wa kura za Popular vote za kila jimbo. Kwanini nasema hivyo, waza haya.
1. Uchaguzi wa USA rasmi (ambapo Popular votes hupigwa) utafanyika siku ya jumanne (5/November) na katika hali ya kawaida kufikia jioni ya siku ya jumatano (6/November) tayari mshindi wa kiti cha urais wa USA atakuwa tayari amejulikana kwa kila mtu dunia nzima, wakati upigaji wa kura za wajumbe wa Electoral college zitakuja kufanyika wiki kadhaa huko baadaye. Kama wajumbe wa Electoral college (independently) huamia mshindi wa urais wa USA, kwanini mshindi ajulikane kabla ya kura zao kupigwa?
2. Hakuna mgombea yoyote wala chama chochote katika USA kinachoweza kupoteza hata dakika moja kuwafuata hao wajumbe wa Electoral college kikiomba kura zao. Yaani hakunaga kampeni za kuwashawishi hao wajumbe wa electoral college. Sio kwamba inakatazwa bali kimsingi hakuna mantiki ya kufanya hivyo.
Sasa Kama hao wajumbe ndio huamua nani awe rais, kwanini wagombea na vyama vyao wasitumie kila resource kuwashawishi hao wajumbe kuliko kutumia hizo resource kusaka popular votes ambazo 'haziamui' nani awe rais?
HITIMISHO LANGU.
Mchakato wa uchaguzi wa USA kumpata mshindi hauna tofauti yoyote ya kimsingi na chaguzi zingine za nchi nyingi za kidemokrasia ya moja kwa moja, tofauti chache zinazoelezwa zipo katika sayansi ya kutafsiri walio wengi ni kina nani au wamepatikanaje. Kwa mfano, katika uchaguzi wa Tz, mshindi wa kiti cha urais ni lazima apate zaidi ya 50% ya kura zote halali, na mshindi wa kiti cha ubunge au udiwani ni yule mwenye kura nyingi zaidi ya wagombea wengine (hata kama mshindi amepata chini ya 9% ya kura zote).