Kwa jumla, kuna wabunge 435 katika Baraza la Wawakilishi na maseneta 100, hivyo jumla inakuwa hivi,
- 435 (wabunge) + 100 (maseneta) = 535.
- Kisha, kuna wajumbe wawili kutoka eneo la Washington, D.C., hivyo kuleta idadi kamili ya wajumbe kuwa 538.
District of Columbia ina wajumbe watatu [3], siyo wawili.
535+3=538.
Wajumbe hawa wanaweza kutofautiana kutoka jimbo moja hadi jingine. Kwa mfano, jimbo kubwa kama California lina wajumbe wengi zaidi kwa sababu ya idadi yake kubwa ya watu, wakati majimbo madogo kama Vermont yana wajumbe wachache.
Ova
Maelezo mazuri.
Inafurahisha kuona walau wapo watu humu ambao kidogo wana uelewa wa mfumo wa uchaguzi mkuu wa urais ulivyo nchini Marekani.
Maana kuna watu wengine humu hawajui, na mbaya zaidi, hawajui kama hawajui.
Ukiwaeleza kuwa wanavyoelewa ni makosa, wanashupaza shingo na kuleta ubishi.
Hawajui tofauti ya national popular votes na state popular votes.
Hawajui ni votes zipi ndizo zinazoamua mgombea apate EV za jimbo.
Ukiwaeleza kwamba demokrasia ya Marekani siyo ‘direct democracy’, bali ni ‘representative democracy’, ndo unazidi kuwachanganya.
Ukienda ndani zaidi na kuwaeleza kwamba, Marekani siyo demokrasia [America is not a democracy] bali ni constitutional federal republic, ndo unawapoteza kabisa na watakubatiza majina yote!
Nyongeza: electoral college votes za jimbo huongezeka na/au hupungua kuendana na idadi ya watu/ wakazi waliopo jimboni.
Mfano, jimbo la California, Abraham Lincoln alipata kura 4 mwaka 1860. Kwenye uchaguzi wa 1864 akapata kura 5.
Mwaka 1980, Ronald Reagan alipata kura 45. Mwaka 1984 akapata kura 47.
Mwaka 2000 Al Gore alipata kura 54.
Hillary Clinton 2016 na Joe Biden 2020, walipata kura 55.
2024, California ina electoral votes 54.
Hapo utaona zimepungua. Hiyo ni kutokana na jimbo kupungukiwa wakazi na hivyo kupoteza kiti kimoja cha bunge la wawakilishi.
Kuongezeka au kupungua kwake, kunafuatia matokeo ya sensa.
Sensa ya mwisho Marekani ilikuwa 2020. Matokeo ya sensa hiyo yalitolewa 2021.
Ndo maana Joe Biden 2020 alipata EV 55. Lakini mwaka huu 2024, zimepungua na kuwa 54.