DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Ukiona Manyoya ujue kaliwa..Kwa muda mrefu, Askari wa JWTZ wamekuwa wakilaumiwa kwa kujichukulia Sheria mikononi mwao. Kwa kuwa wao ni wanajeshi, wanaamini kwamba wanaweza kupiga watu makofi mtaani hovyo bila kuulizwa na mtu.
Pengo la uhusiano mnalolitengeneza kati yenu na raia wa kawaida, mtakuja kuliona nyakati zijazo. Na mtambue kuwa uwezo wenu wa kuilinda hii nchi unategemea ushirikiano kamili na wananchi.
Hatuombi mabaya yatokee lakini siku nchi hii ikipitia kwenye misukosuko ya kiusalama, mkipita mitaani katika kutekekeza majukumu yenu, mtakutana na sisi raia wa kawaida ambao awali mlikuwa mkitupiga hovyo.
Mkiishiwa chakula, hatutawapa
Mkiishiwa maji, hatutawapa
Mkitumia ubabe Kama mlivyojizosha tutawawekea sumu.
Katika serikali ya awamu ya tano, tulishuhudia chuki kubwa Kati ya raia wa kawaida na jeshi la Polisi baada ya maaskari hao kutumia mamlaka vibaya na ubabe wa kishamba, Nadhani hiyo chuki imepungua awamu hii.
Nia yangu Ni njema Kama raia mwema, natumai haki yangu ya kikatiba kuwashauri. Badilikeni Masoja, Tanzania yenye ulinzi imara inaanza na raia wema, Kisha Maaskari. Sisi ni wengi Kuliko nyie hivyo bila sisi hamtaweza kuilinda hii nchi.
Mkuu wamekutemesha Bungo 😅😅