Ungekuja kutoa malalamiko yako sehemu husika ili upate haki yako jeshi ni la wananchi ni mali yenu sote.
Shida siyo kutoa malalamiko,yaani mtu anipige makofi,nije nitoe malalamiko,dawa ni kupambana kadri unavyoweza,kama utapigwa sawa,kama utampiga sawa.Wananchi waache unyonge,mwanajeshi akikuzingua eti anataka kukupiga,usipigwe kizembe,pambana kadri unavyoweza.Hakya-Mungu siwezi kukubali uniaibishe hadharani,halafu niende kwa wakubwa ukaombe msamaha faraghani,aisee sikubali.
Jiulize kwanini Rostam Aziz alipotuhumu mahakama kuwa haziko huru,aliambiwa na chama cha majaji,aombe radhi vilevile alivyotuhumu,yaani kama aliita vyombo vya habari kutuhumu,basi aite vyombo vya habari kukanusha na si vinginevyo,angesema akanushe faraghani,nani angejua kakanusha?
Narudia tena,mwanajeshi asiye na nidhamu,akinizingua,namimi namzingua,ni heri tupambane nionekane nimepambana,siyo kupigwa kizembe.