Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mbowe amejitahidi sana kufanya siasa za kistaarabu siku zote, bila kutambua kuwa ustaarabu unakuwa na maana, na unaweza kuleta matokeo chanya kwa mtu ambaye ni mstaarabu. Kumfanyia ustaarabu mhuni, jambazi, muuaji, ni kupoteza muda, na wala hutapata matokeo unayoyatarajia.
CCM ni chama milichosheheni wahuni, watu waongo, watekaji, wauaji na wevi wa mali za umma na kura. Je, ukiwapelekea ustaarabu, unadhani watauchukuliaje?
1) Mwenyekiti ambaye ndiye kiongozi mkuu wa CCM anasema kuwa watu hata wakipigia kura kungine, kura zitahesabika CCM.
2) Watu wanatekwa, wanauawa, wanatupwa porini, mwenyekiti wa CCM anasema kuwa hakuna utekaji, hizo ni drama. Yaani drama za kufa au kuumizwa vibaya kama yule aliyepigwa risasi kichwani na risasi kutokea mdomoni, kwake hizo ni drama!!
3) Mwenyekiti wa CCM anatamka kuwa katiba ni kijitabu tu. Maana yake ni kitu kidogo kisicho na maana, na yeye halazimiki kukifuata hicho kijitabu. Mantiki ya hiki ni kuwa yeye hafuati katiba wala sheria.
4) Kiongozi wa UVCCM anasema wazi kuwa watu wanaowakosoa viongozi, wakipotea, polisi wasiwatafute, maana yake ni kuwa ni wao watakuwa wamewateka na kuwaua.
4) Kiongozi mwandamizi wa CCM aliyekuwa waziri anazungumza kwa majigambo kuwa kura za wananchi hazichagui viongozi, viongozi wanachaguliwa na wanaohesabu kura. Huku tunajua kuwa wanaohesabu kura wanateuliwa na Mwenyekiti wa CCM.
5) Kiongozi mteule wa Rais, DC wa Longido, anasema wazi kuwa ushindi wa CCM unapatikana kwa kutumia Serikali kwa kuwateka watu na kuwapeleka maporini.
6) Katibu mkuu wa CCM anasema kuwa CCM inatumia dola kushinda uchaguzi.
7) Waziri wa TAMISEMI? anasema wazi kabisa kuwa eti mwaka 2024, kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, ni lazima CCM ishinde vijiji, vitongoji na mitaa yote.
Hivi kweli chama na Serikali yenye falsafa za namna hii, ukienda kwa ustaarabu wa hadithi na ngojera nyingi, zinaweza kubadili chochote?
Sasa tunashuhudia vijana, wazee wa CHADEMA, wakitekwa na kuuawa mmoja baada ya mwingine, Mwenyekiti akiendelea na matamshi kuwa watachukua hatua za kisheria!! Hivi Mbowe ni mgeni na mahakama za Tanzania? Yeye mwenyewe baada ya kubambikiwa kesi ya ugaidi, alitolewa kwa kauli tu moja ya Rais kuwa mwachieni sasa, akaachiwa, akatoka. Hii ina maana Rais akitaka, hata leo hii anaweza kuiagiza mahakama kuwa Mbowe mwekeni ndani miaka miwili, atatafutiwa kesi, atafungwa.
7) Rostam, aliyekuwa mweka hazina na mfadhili wa CCM, mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, anasema wazi kuwa majaji na mahakimu buwa wanapewa maelekezo na Serikali katika kutoa hukumu.
8) Spika wa Bunge la CCM, anasema kuwa Bunge lipo chini ya Serikali, lazima lifuate matakwa ya Setikali.
9) Jaji mkuu anawahutibia na kuwapa maelekezo majaji kuwa hukumu zao zizingatie matakwa ya Seikali.
Hapo unaamini kuna mahakama? Unaweza kupeleka kesi ya mauaji yaliyofa ywa na dola kwenye mahakama, ikahukumu dhidi ya dola?
Mahali tulipofikia, Mbowe ana machaguo mawili tu:
1) Kuongoza mapambano dhidi ya udhalimu wa CCM kwa lugha ambayo CCM itaelewa kuwa wananchi hawapo tayari kuendelea kudhulumiwa kwa namna mbalimbali. Hapa kuna gharama, tena siyo ndogo, lakini hili lina uhakika wa kuketa matokeo.
2) Kutamka kuwa hatuna uwezo wa kupambana na wadhalimu hawa wa CCM, tuwaache wafanye chochote wanachotaka bila ya kuhoji, kukosoa, wala hakuna haja hata ya kufanya uchaguzi, tuwaache CCM wagawane nchi na rasilimali zake, kadiri wapendavyo, ilimradi sisi tuamke salama.
Lakini kukaa katikati, yaani si moto si baridi, siyo chaguo. Tukiendelea na haya tunayoyafanya sasa, tutaendelea kushuhudia kupotea kwa uhai wa wenzetu, sisi tukiendelea na tlaatlaah zisizobadili chochote. Na siku nyingine, zamu zetu za kupotezwa zitawadia.
Mahakami ni kupoteza muda. Kesi ya juzi tu kuhusu vijana waliotekwa na vyombo vya usalama, ambao mawakili waliiomba mahakama itoe amri kwa polisi wawafikishe waliowateka mahakamani haraka, mahakama ikasema kuwa hakuna ushahidi. Halafu leo tena, baada ya watu wale wale kumteka na kumwua Ally, Mbowe anasema CHADEMA watachukua uamuzi wa kwenda mahakamani!! Ni mahakama ya wapi? Mahakama hizi ambazi zipo kwenye mfumo huo huo wa watekaji na wauaji au mahakama za ahera?
Ushauri wangu, Mbowe mchango alioutoa kwa Taifa hili na kwa CHADEMA, umeonekana, lakini kwa nyakati hizi, na kwa mazingira ya nchi yetu, anahitajika kiongozi mpambanaji hasa. Mbowe sahizi, pengine angefaa sana kwenye nafasi ya mlezi wa chama, na shughuli yake zaidi iwe ni mahusiano ya kimataifa. Nchi imefikia hatua mbaya kabisa kuliko kipindi chochote kwenye uhai wake. Katika usalama wa watu, ni aheri hata wakati wa mkoloni, watu walikuwa salama zaidi kuliko wakati huu. Watu wanaamka asubuhi, hawajui kama mpaka jioni watakuwa hai. Watu wanaanza safari hawajui kama watafika huko waendako.
View: https://www.youtube.com/live/z9D-bTDYzB8?si=3krPZ3uNWUNHVV38