Ujumbe kwa Prof. Assad: Hatutaki Rais anayesikiliza kila mtu na la kila Mtu!

Nadhani Kuna watu wamesahau kabisa Baba wa Taifa alipoonya sana la Rais kupewapewa ushauri bila kuwa na msimamo wake. Kinachoendelea sasa ni kujaribu kumtega Rais Samia ili asiwaulize au kuwakatalia. Ni mtego mbaya sana.
hahahaha. Kwamba mtego atauruka kwa style ya kwamba 'kila mliloniambia nimewasikiliza na kufanya.mbn mnanilaumu sasa'

Hahahaha ni 'ufyatu'
 
Ni ujinga wa kiwango cha juu sana kulaumu na kukashifu awamu ya tano bila kwanza kutambua hali ya nchi ilipokuwa imefikia kabla ya awamu ya tano kuingia madarakani..kuwa kiongozi si lazima uwafurahishe unaowaongoza na hasa km akili ya wengi kila mmoja anafikiria tumbo lake na kwamba yupo hapa duniani kwa ajili yake na familia yake!
 
Rais ni lazima atafute na apime na kutekeleza ushauri wa kitaalamu! Sio kuja na wanganga wa kienyeji na maombi kutatua matatizo ya kitaalamu, si sahihi!
 
Who was Magufuli..he was nobody! Try to see beyond a person.
Siku katiba mpya ikija..ije na guidance kuwa, tukichagua RAIS mpya, hapo ikulu na taasisi yote ya urais nayo iwe na watu WAPYA wote! aliyetuumba hajawahi kuumba SUPERMAN..miaka 60 toka uhuru bado tunawaza na kubehave km taifa la miaka 18..hatuwezi kuwa wajinga wa kiwango hicho.
 
Aisee....basi bora hiyo katiba mpya ndiyo tuiapishe iwe rais!
Hahitajiki mtu pale au sivyo!
 
Mkuu, lakini kwa vigezo vyote vya utawala bora, makini na wenye kujali katiba, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali, ufyatu ulikuwa wa kiwango cha juu sana katika utawala wa awamu ya tano. Na hapa ndipo kilipokuwa chanzo kikuu cha uwepo wa hoja fyatu kutoka kwa wasomi mbalimbali.
 
Rais siyo secretary wa kutekeleza tu anachoambiwa, ni hatari kwa nchi kuwa na rais wa aina anayomtaka Assad.

Kwanza uelewe hao wanaoitwa wasomi ndio waliochangia kiasi kikubwa kuifikisha nchi kwenye wimbi kubwa la ufisadi na ubadbirifu wa mali za,umma kupitia sera mbovu na mikataba mibovu.
awamu ya swahba wake Assad (JK) ndio ililiyoiharibu nchi kwa mikataba mibovu ya madini, gas na manunuzi lakini tafuta katika ripoti za Assad za ukaguzi huwezi kkukuta anakosoa. Angekuwa mkweli bbasi angekuwa anailaumu serikali ya JK kwa madhila makubwa mbalimbali aliyoisababishia nchi.

Assad ni Zitto mwingine wote maajenti wa udini na ufisadi katika koti la usomi na utaalamu
 
Nimemwambia mtoa mada kama anadhani Mama anasikiliza kila kitu aende na yeye akampe ushauri wake..

Ukifuatulia hata ziara za Rais amekuwa akiruka viunzi vingi vya mambo binafsi ya watu kuchongeana..

Mfano juzi kuna mbunge kamchongea DED ,Rais kajibu tuu kwamba watu wafuate taratibu na sheria..

Mwendazake mpenda sifa angehemka na kufanya maamuzi waliyoita papo kwa papo huku yakiwa ya kukurupuka na kuumiza watu..

Rais Samia akiona jambo linahitaji consultations au hana ufahamu nalo mara nyingi huwa anasema nalichukua,huwa hakurupuki.
 
Hatujaelewana
 
Nimecheka Sana ,mzee mwanakijiji anampiga bit prof, nchi ngum sana
 
Kwa hiyo waachwe wasomi muingie nyie mburula au?

Mambo ya Wazalendo wa Chato haya 👇

View attachment 2232652
Kwa hiyo waachwe wasomi muingie nyie mburula au?

Mambo ya Wazalendo wa Chato haya 👇
Attribute namba moja ya msomi ni kuwa objective sio subjective katika kujadili issue; pili anatakiwa ausimamie ukweli bila kujali gharama yake. Msomi wa kweli haongozwi na tumbo kayika kujadili issue ya umma.

Hao unaowaita wasomi in fact wamekaa darasani muda mrefu lakini sio wasomi.. Indicaator mojawapo ni kukubali kuwa subcontracted kumchafua Magufuli.
 
Kwanza unaposema MAAMUZI YA KUUMIZA WATU una maana gani? Mtumishi anapokuwa mzembe au mwizi hakuna watu wanaoumia kwa yeye kuwa hivyo? Kwa nini unahukumu reaction ya tatizo badala ya kuhukumu tatizo limetokeaje..kama hupendi reaction za papo kwa papo be careful na kazi, usifanye makosa! Unatenda kosa halafu unataka uulizwe wakufanye nini baada ya kukosea..hakuna kitu cha hivyo mahali popote.
 
Assad hajui kutofautisha kati ya kusikilizwa na kukubaliwa. Unaweza kutoa mawazo yako yakasikilizwa lakini yasikubaliwe. Yeye alitaka mawazo yake yakubaliwe tu, na hiyo ni weakness kubvwa sana kwa Assad.
 
Tena kiuhalisia walitaka si asikilize ushauri wa kila mtu, Bali walichotaka ni kumfanya asikilize ushsuri wa kila mpumbavu aliyejiona ana nguvu Fulani, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Taasisi, Siasa, Wafanyabiashara, Wawekezaji, Matajiri, nk...

Makundi yote hayo yalitaka kumpanda kichwani wasijue ni Kisiki Kizito. Matokeo yake ndio kutengeneza hoja mufilisi kupitia vibaraka wao kama Assad.

Ni wa kupuuzwa tu.
 
Wenzetu hao ni zaidi ya katiba, hata tukiwa na katiba kama yao bado hatuwezi kuwa kama wao.
Tuanze kujifunza kuheshimu katiba iliyopo ili tuweze kupata faida ya katiba mpya ikija.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…