Ujumbe kwa Prof. Assad: Hatutaki Rais anayesikiliza kila mtu na la kila Mtu!

Ukionekana unaleta namna gani vp unashughulikiwa tu hata Kikwete alimshughulikia Ulimboka.
 
Kinachoonekana nchi yetu ilishatekwa. Mabeberu waliwekeza kwa watu kiasi kwamba walitegemea enzi za Dkt Magufuli wakisema kitu basi wasikilizwe ili mambo yao ya kuiibia nchi yaendelee, na ndicho Dkt Magufuli aliwahi kusema serikali yake haiambiwi kitu na mtu yeyote, wakakasirika sana. Sasa kwa Mama inaonekana wanatamani sana tena sana akubali kila aina ya ushauri kitu ambacho ni hatari sana
 
Ulichokieleza ni wote tunahitaji kubadilika ili tuweze kuyafikia mabadiliko tunayohitaji ila ubaya ni kwamba huwa hatuhitaji kubadilika ila tunataka mabadiliko na ndio maana tunalilia katiba mpya kwa kudhani kwamba kila kitu kitajiseti tu chenyewe.
 
Mi nilijiuliza kitu kimoja! Why Prof Assad ameitwa kwenye kikosi kazi na si Ludovick Utouh? Nikakumbuka kuwa "Anaemlipa mpiga zumari ndiye anaechagua wimbo".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno yako tu yanaonyesha una chuki ya kwako dhidi yake..kiongozi hachaguliwi kufurahisha mtu mmoja mmoja! Pili, si mara ya kwanza bei za mazao kushuka, hata huko nyuma zmewahi kushuka! lkn ni nani kati ya viongozi wote alikuwa mtetezi wa kweli wa wakulima? Uhusiano gani uliharibika, mbona AfDB wamefadhili miradi mingi kipindi chake kuliko wakati wowote..ni ujinga kutetea uhusiano wa kinafiki na kinyonyaji kiongozi mwenye uchungu na hali ya maisha ya watu wake na rasilimali za nchi hawezi kukubali uhusiano wa kudharauriana! Wajibu mkubwa wa serikali na kiongozi mkuu ni kuzuia mfumuko wa bei na si kupandisha mishahara..kwanza kuthubutu tu kuanzisha JNHPP, SGR, madaraja makubwa, meli na vivuko nk inahitaji ujasiri wa aina yake, yeye aliweza, mbona wengine walishindwa..hakuna mtu ataishi milele hapa take that note! everyone will die, be t ulikuwa mwema sana, uliuwa wengine, vyovyote..huhitaji kukumbushwa jambo hili km una akili timamu! Kiongozi huwezi ukawa na furaha kuongoza nchi imejaa udhalimu kila mahali tena wa wazi..nadhani ulikuwa unamsikia yeye hakuwa anaogopa kifo, nani mwingine ulimsikia anasema hivyo! aliyoyafanya yalitosha kwa muono wa aliyemuumba na kumjalia kupata hiyo nafasi..hiyo siyo kesi yetu, tumia vzr akili ulizopewa kijana usije kufuru bure kwa chuki zisizo na kichwa wala miguu..
 
Watoto wa mjini muda wenu huu kutamba megeni nchi mtakavyo, Jiwe alikuwa mshamba ndio maana alikuwa anawazingua na kuwafanya mupitie kipindi kigumu. Unajua Jiwe alikuwa anazingua aliifunga nchi kwa ushamba wake ila sasa mama kafungua si unaona hata panya road nao wamepata uhuru wao achilia hao wauza ngada waliyokuwa wamefulia unga hakuna mateja hawakuwa na jinsi kuacha unga, sasa hivi siwaoni kule muhimbili sijui ndio wamerudi walipotoka.

Ila mama yupo vizuri ndio raha ya watoto wa mjini.
 
Sidhani kama Prof. Assad alimaanisha hivyo,kuwa tuwe na Rais anayemsikiliza kila mtu. Kumekuwepo na madhara makubwa sana ya kuwa na viongozi wasioshaurika viongozi wanaodhani na kuamini wao wana akili kuliko watu wote. Hata mipango/miradi yao mingi ni ya kukurupuka pamoja na kuwa na nia njema. Nia njema haihalalishi njia mbovu. Lakini naamini wapo watu walioshauri kwa utalaam walikuwa nao na hawakupewa nafasi.
Nilichoelewa anachomaanisha ni kuwa na mfumo imara wa kumdhibiti Rais dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka.
Marekani ingekosa mfumo imara,watu Kama Rais Trump kwa yale aliyokuwa akijiapiza kuyafanya akichaguliwa kuwa Rais, sijui kama hata nyie mnaoishi huko mngesalimika na bila shaka na ule ukuta wa kuitenga Mexico ungekuwa umeisha.
Mfumo imara utamlazimisha Rais kuheshimu sheria na katiba ya nchi.
Mfumo imara hautaruhusu kuunda sheria kandamizi, kama za vyombo vya habari, au kuunda sheria za kulinda watu wasishtakiwe wakiwa madarakani ndo tunajikuta na watu Kama kina Ndugai anafanya anachotaka kwenye mhimili mzito Kama bunge kisa anayo kinga.
Mfumo imara utazaa bunge huru,leo bunge letu linategemea na nani ni spika kwa wakati huo, angalia kwa kesi zile zile alivyoamua Ndugai na kesi zile zile anavyoamua Tulia.
Mfumo imara utatupa mahakama huru, angalau kidogo kama mahakama zilee chini ya Mzee Nyalali au Barnabas Samata,ulikuwa huwezi kuwaona kwenye shughuli zozote za propaganda,siyo hawa wa sasa, mara kwenye makinikia na wao wapo,halafu sijui kama wenye hayo makinikia,hawaridhiki unawategemea waziamini mahakama zetu,wakati umemuona CJ yuko kiti cha mbele anasikiliza anatikisa na kichwa kwa huzuni. Mfumo imara utatupa tume ya uchaguzi huru siyo hii ambayo nayo inaushangaa uchaguzi wa 2020 ulivyoendeshwa.
Mfumo imara utaweka mipaka ya kiutendaji kwa vyombo vyetu vya dola.
Polisi au JWTZ watajihusisha na majukumu yao ya kikatiba tu na kamwe haitawezekana kuwatumia kisiasa.
Mfumo imara utawapa wananchi heshima kuwa wao ndio wamiliki wa nchi hii na raslimali zake, na siyo kuambiwa eti Rais ametoa fedha za mradi huu kana kwamba ni za kwake na ni hisani yake,utaondoa kauli za kuzimu kama zile,eti mkichagua upinzani hatuwaletei maendeleo,kauli za kibaguzi na wizi mkubwa,unawanyima maendeleo wakati na wao ni wachangiaji wazuri wa pato la nchi kupitia Kodi zao.
Mfumo imara utajenga watanzania wenye kujiamini,wenye kujua haki zao na kuzisimamia na siyo,tabia ya sasa ya kuwa na watu wanafiki wasioaminika,kwao ni kujipendekeza kwenda mbele kisa Rais aliyeko ni kabila lake, au wa dini yake au chama chake.
Tunatamani kuwa na wasomi angalau kidogo wa enzi zile za kina Prof. Chachage, Haroub Othman, Mwesiga Baregu, Mwaikusa na wengine ambao wakikutana Nkurumah hall mpaka nchi jirani zinafuatilia.
Tuwe na wataalam wenye exposure ya kutosha kusimamia raslimali zetu, na siyo tunayoyashuhudia sasa. Tunao wahandisi wazuri midomoni wape kazi sasa ushangae. Bidhaa nyingi tunazoona toka china ukisikia wanaozitengeneza hata diploma kama wanazo ni wa kuhesabu. Hivyo lazima tuwajengee uwezo wataalam wetu kwa kukusudia.
Ni ngumu sana kuamini Maendeleo yetu yatategemea wawekezaji kutoka ulaya na Asia bila kuhakikisha tunawawezesha watu wetu kupata utalaam na wao kuwa na uwezo wa kuanzisha viwanda wenyewe. Wakati Saab scania wanafungua tawi lao hapa Tanzania 1972, pia na Brazil walianzisha, leo ya kwetu imekufa wakati ya Brazil wanatengeneza scania 95% ni 5% tu wanaagiza Sweden.
Hatuwezi kujilaumu na kujuta bado tunayo nafasi ya kufanya vizuri zaidi.
Tupiganie tupate mfumo imara.
 
Naona hukumuelewa Prof. Mussa Assad.

Yeye hakumaamisha kwamba Rais anapaswa kumsikiliza kila mtu hapana, Tatizo kubwa ni Rais kushindwa kuwasikiliza wataalamu. Kuwa Raisi Haina maana unamfahamu kila kitu.

Kila Nyanja ina wabobezi wake kitaaluma, na ni lazima tuheshimi ushauri wa kitaalamu tunaopewa na wenye taaluma zao.

Huwezi jiamulia Tu as if Hii nchi ni familia yako. Ikiwa wanaukoo hukaa kikao kushauriana kwa pamoja na kufikia muafaka iweje nchi yenye watu zaidi milioni 60 iamuliwe na akili ya mtu mmoja?
Matokeo ya maamuzi binafsi yasiyozingatia weledi tumeyaona.
Zamani nilikuwa nakuelewa sana Mzee Wangu Mwanakijiji Ila siku hizi sijui umekuwaje.
 
Kwa jinsi mifumo yetu ilivyo, unategemea uende mahakamani kushtaki utawala mbovu wa kiongozi hasa kwa ngazi ya urais? Watu walivunjiwa nyumba hapo kukiwa na zuio la mahakama, na aliyeagiza hayo ni rais. Mkuu naona unaongea nadharia ukihisi tumesahau. Huenda ulikuwa mfaidika wa uovu ule hivyo huamini ukweli uliopo. Naona kama unanipotezea muda, nikianza kuweka ushahidi hapa utakuwa huna lolote jipya zaidi ya kusema yaliyopita si ndwele.
 
Assad angekuwa jasiri asingekanusha siku ile Ikulu kuwa hatukuibiwa 1.5T
 
Hata jengo la TANESCO lilivunjwa pale ubungo..dalili za a corrupt society ni matumizi yasiyofaa ya court injunction, moja ya sifa mbaya za watu wa nchi hii ni ukiukaji wa sheria makusudi, mf. uvamizi wa maeneo makusudi.. wakiambiwa wanakimbilia kuweka zuio mahakamani..jambo la maendeleo ya nchi liko juu ya ubinafsi wa wachache, kiongozi hodari hahitaji kufundishwa hili..ningekuwa nakupotezea muda huo muda unaotumia kila siku kumtukana mtu tena asiyekuwepo si ungeutunza ukusaidie kufanya mambo ya maana kuliko kuupoteza hapa..wewe orodhesha maovu usilete hoja mufilisi unauliza maswali na kujibu mwenyewe..dunia ya leo si lazima muhalifu umshitaki kwny mahakama za ndani ndio maana kuna mahakama ya Africa hapa, hata ile ya the Hague ipo kwa ajili ya jinai zinazofanywa na viongozi dhidi ya watu wake.
 

Yeye mwenyewe alikuwa jizi la kura sasa sijui ni uadilifu gani alikuwa anasimamia. Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika.
 
Assad angekuwa jasiri asingekanusha siku ile Ikulu kuwa hatukuibiwa 1.5T
Kwani ile iliibiwa? Ilikuwa inaeleweka imetoka wapi na imekwenda wapi, ule siyo wizi kwa definition ya neno 'wizi'.
 
..tunataka Rais anayepanda HAKI.

..Jpm alikuwa kiongozi asiyependa haki, alikuwa na hulka ya ukatili.
 
Mzee umeibukia wapi
 
hivi wabongo tunataka Rais wa aina gani? anaesikiliza au asiesikiliza? tusifungane midomo tupige kura tujuane!!
Sidhani kama Magufuli alikuwa hasikilizi. Mara ngapi tuliona anasikiliza vilio vya watu kila anapokuwa ziarani sehemu mbalimbali?? Kuna wa kusikiliza ila kuna wa kutimua hapo hapo. Nakumbuka kuna mkurugenzi ama das aliwahi kujikanyaga maelezo akampa nafasi mwingine kuelezea na akamsikiliza vizuri hadi huyo aliyetoa maelezo ndo akapewa uongozi wa juu na kumvua aliyeshindwa. Danadana hatuzitaki
 
Eti hasara. 😁😁 tunajua chadema hasara yenu ni kutokuingia mjengoni tu. Hakuna machungu ya taifa hapa, kama mliyemuita mwizi mlimteua agombee urais na kumnadi kwa mbwembwe zote mnayo machungu na nchi hii kweli?
 
Jibu lako lina maana kuwa Magufuli alikuwa hasikilizi, lakini siyo kweli kwani kuna mifano mingi sana inayoonyesha akiwa anasikiliza ushauri. Tatizo la Assad ni kuwa alitaka Magufuli amsikilize na achukue ushauri wake yeye moja kwa moja, jambo ambalo siyo kweli, kwani Magufuli naye alikuwa na analytical skills za kujua namna ya kuacheive malengo yake. Ukimpa ushauri ambao hauko kwenye malengo yake anakuachia hapo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…