Los técnicos
JF-Expert Member
- Sep 14, 2014
- 3,031
- 2,668
Nje na masuala ya kiimani, kuna tatizo lolote kuwa na tume huru?Mmh!mambo ya kanisa unaleta JF.sawa ahsante kwa mtazamo lakin kura ya mtu ni siri.Hakuna KKKT anayelazimishwa kuwa CDM wala CCM wala chama chochote.Huo uzushi peleka huko lumumba.
Wanachofanya maaskofu ni kukemea uovu iwe kwenye chama chochote.Lengo ni kuona nchi inaenda mbele.Bila kuua,kuteka,kutesa,kubakiza kesi wengine n.k
NB:sijui kwa nini umeandika kwa herufi kubwa.Au ndo kuonesha msisitizo?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha najua unayo familia yakianza unajifungia hutaki hata kutoka nje, hivi ninyi mnasubili nani aanzishe wakati wewe upo? Anza wewe jitoe muhanga kama yule mwarabu alivyofanya wengine wakafuatia, sasa wewe unataka lakini hutaki kuanza, wakitangaza kuandamana wewe unaagiza chips na bia unasubili kutizama kwenye runiga.
Unajiona uko sahihi kweli?Duh...!
Kumbe...
Ndio maana chama fulani kimeshika majimbo fulani maeneo ya KKKT predominantly areas!
Kumbe mambo yenyewe ni haya!.
Hili ni angalizo zuri, na litasaidia sana!.
Tena litatusaidia kwasababu kikawaida kule juu kabisa, akiwa Mkristu huwa ni lazima awe Mkatoliki, sasa hawa KKKT wanavyo anza kujiorganize hivi, wanapaswa kuishia huku huku chini kwenye ubunge tuu, sasa wakiingia tamaa na wao wakatamani kule juu itakuwaje?!. Bora hili tumelijua mapema na huu ndio uzalendo wenyewe wa kweli kwa taifa lako.
P
Mkuu nimesoma bandiko lako Mara 2 sijakuelewa kabisa, umekosea mkuu, unaweza kuleteta ushabiki lakini ukapandikiza mbegu za chuki miongoni mwa wananchi,
Unajiona uko sahihi kweli?
Kwa hiyo kuwa mzalendo Tanzania ni kuwachagua katoliki na waislamu tu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mtu kakuandikia au ni wewe mwenyewe???!!!
Paschal Mayalla acha kabisa kuongelea udini, usije ukasababisha machafuko mtandaoni humu
Analysis ya kibwege kuwahi kutolewa na MTU mwenye akili kama wewe.
Unapoleta humu jua pia kuna wa kkkt wa Rc wasabato waislamu nk kama ungekuwa na akili ungepeleka sehemu husika ila sababu ni majungu ndo mana umeleta humu
Sent using Jamii Forums mobile app
You believe that?PSumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."
Wanabodi, Swali hili niliwahi kuliuliza huko nyuma, thread iliunganishwa na thread yenye statement ya "tunanyemelewa na udini"!. Ile thread ni ya statement, mimi thread yangu ni ya swali, niliuliza "Je huu udini, Ukanda na Ukabila unaozungumzwa ni kweli upo na una exist in reality au ni dhana...www.jamiiforums.com
It's not an issue of beliefs, it's a fact.You believe that?
Hebu iweke wazi hiyo imani yako.It's not an issue of beliefs, it's a fact.
P
KWA MUDA MREFU NIMEKUWA KATIKA SHUHUDA KWA WATU, NDANI NA NJE YA NCHI KUHUSU MWENENDO WA KANISA LETU, VIONGOZI WETU KATIKA KANISA NA HATA KUHUBIRI MAMBO AMBAYO KWAYO, KKKT LIMELELEWA MIAKA MINGI ILIYOPITA.
SISHANGAI MABADILIKO NDANI YA KANISA, ILA MABADILIKO YANAPOKIUKA MISINGI YA DINI, IMANI, MAADILI NA MAFUNDISHO YAPASA KUYAKEMEA BILA KUPEPESA MACHO.
NIMEWAHI KUSEMA JUU YA MWENENDO WA MCHUNGAJI WANGU *SAMWEL PALLANGYO* AMBAYE KWA SASA ANATAKA KULICHAFUA KANISA KWA SABABU ANATAKA KUWA ‘YUDA’. AMESHAWISHI KONGAMANO LIFANYIKE TAREHE 29/12/2019 NA LITASHIRIKISHA NDUGU ZAKE WALIOMPA FEDHA.
KANISA LINAPOAMUA KUFANYA BIASHARA ZA NAMNA HII, LINAHARIBU TASWIRA YA KANISA LA KIKRISTO KWA UJUMLA.
BABA ASKOFU DKT. SHOO UPO, KWA NINI YEYE AFANYE VIKAO VYA SIRI VYA KUTAKA MAGEUZI NDANI YA KANISA NA NCHI BILA MAASKOFU WOTE KUFAHAMU JAMBO HILI? JE HARIDHISHWI NA MKUTANO MKUU WA KANISA AU HALMASHAURI KUU? TUNAPOKUTANA MAKUMIRA NA KUYAJADILI MAMBO YETU KATIKA KANISA MBONA HUWA HAYASEMI AMBAYO MOYO WAKE UNAYATAKA? URATIBU WA MAMBO KWA NJIA ZA SIRI KULIHUSISHA KANISA LENYE UONGOZI JE, SI SHAMBI HIYO?
KWA AMBAO BADO HAMJASHIRIKISHWA, JIANDAENI.
ANALITUMIKIA KANISA NA ANATUMIKIA CHAMA CHA SIASA KUPITIA KANISA. ANALIPWA FEDHA, ANASHAWISHI WAUMINI MMOJA MMOJA. MIONGONI MWETU TUNALAZIMISHWA KWA SABABU FULANI FULANI BILA KUJALI KWAMBA KANISANI WAPO WAUMINI WA VYAMA MBALIMBALI.
ANAHIMIZA KUFUATA MSIMAMO WA CHAMA CHA SIASA AMBACHO KATIBU WAKE MKUU AMEMUAGIZA AHAKIKISHE KKKT INAUNGA MKONO BAADHI YA MAMBO YAO, KAMA SIO YOTE.
KWA WALIOZALIWA KABLA YANGU, SIAMINI KATIKA MTAZAMO HUU. KAMA MUNGU ALIPANGA JAMBO KUTOKEA, LITATOKEA. BINADAMU KULAZIMISHA MAMBO NI ISHARA MBAYA HASA MBELE YA MADHABABU.
JOHN MNYIKA ANAPOANZA KUTOA MAELEKEZO NDANI YA KANISA LA KKKT TENA KUPITIA MCHUNGANI AMBAYE YUPO CHINI YA VIONGOZI WAKUU WA KANISA KATIKA NGAZI YA USHARIKA, JIMBO NA DAYOSISI NI ISHARA KWAMBA TUNA WATU AMBAO WANAWEZA KULITUMIA KANISA KUTUVURUGA.
HEBU TUKUMBUKE KIKAO CHETU CHA MWISHO PALE MAKUMIRA, BABA ASKOFU UTANISAIDIA, MAENEO AMBAYO WENGI WALIYAPIGIA KELELE NI MIGOGORO NDANI YA KANISA.
BILA KUJADILI ATHARI ZAKE, SAMWELI ANAINGIA NADHIRI YA KUYATUMIA MADHABAHU KWA AJILI YA KUTAKASA FEDHA AMBAZO ZITALETWA KANSANI KWA KAZI ZA KAISARI. MUNGU TUMPE YAKE NA KAISARI TUMPE YAKE.
SISI TULIO KATIKA KANISA TUNA WAJIBU WA KUOMBA AMANI, UTULIVU NA MSHIKAMANO WAKATI WOTE. MIGAWANYIKO SI JADI YETU, ONENI KAZI TUNAYOPATA KATIKA MAENEO YENYE MIGOGORO KATIKA KANISA LETU LA KKKT. HATA MUNGU AKISHUKA LEO, ANAWEZA KUTUHUKUMU KWELI KWELI.
MADAI YA KISIASA YAKIANZA KUINGIA KANISANI TUTAWAGAWA WATU. HUWEZI KUINGIA KATIKA IBADA YA TAREHE 1/1/2020 NA KUSEMA “SASA TUNATANGAZA RASMI KUWA TUNATAKA TUME HURU YA UCHAGUZI”.
KANISA LINA VIPAUMBELE VYAKE, NA VYAMA VYA KISIASA VINA VIPAUMBELE VYAKE. TUJIKITE KATIKA DHAMIRA ZA KIROHO KULIKO DHAMIRA ZA KIMWILI.
HATA WARAKA TUNAOSHIRIKI KUUANDAA KAMA KANISA,TUNAWEZA JITIA DOA JEKUNDU KATIKA VAZI LA THELUJI. TAREHE 1/1/2020 UWE MWANZO MWEMA WA MWAKA 2020 LAKINI ENDAPO TUTAKUBALI KUTUMIKA, TUTAHARIBU KANISA.
NAWASIHI SANA VIONGOZI WETU WOTE KATIKA NGAZI MBALIMBALI: WAKUU SHARIKA ZETU, MAJIMBO, DAYOSISI, MKUTANO MKUU NA HALMASHAURI KUU HEBU MWAKA 2020 UWE MWAKA WA MAPATANO NDANI YA KANISA NA SIO MIGAWANYIKO.
TUTUNZE NADHIRI KATIKA KAZI YETU YA KANISA ILI NEEMA ZA MWENYEZI MUNGU ZISHUKE KWETU NA VIZAZI VYETU, SASA NA HATA MILELE.
MUNGU AWABARIKI!
_MSHARIKA MWENZENU, KKKT - USHARIKA WA ARUSHA MJINI_
No sio imani, it's a factHebu iweke wazi hiyo imani yako.
Unaamini uraisi ni wa wakatoliki na waislamu tu hapa tz?
Sent using Jamii Forums mobile app
Taratibu mkuu. Heb jaribu kuishi kwenye nchi nyingine za kiafrica.Naomba nikujuze tu kwa hali ya sasa ya kisiasa nchini inatisha mnooo, na kama sio tu uvumilivu wa Watanzania ambao Mungu katujalia sasa hivi tungekua tunajadiri habari nyingine kabisa.
Aliyepaswa kuisimamia haki ndiye anayepokonya haki za wengine. Je ni nani atamkemea? Waache viongozi wa dini wawakemee na wawambie ukweli. Ukisema vipaumbele vya kanisa vifuatwe, nitashangaa kama amani, utulivu na haki itakua sio kipaumbele cha kanisa. Au vipaumbele vyenu ni makusanyo ya sadaka na kufungua miradi ya kanisa?
Mmekariri kuwa wenye kuonywa ni wazinzi na waasherati tu? Kwenye makanisa Huko ndiko kwa sasa kuna upenyo wa kufikisha ujumbe kwa Viongozi wakubwa.
Kwa hiyo Mangula, Lowasa, Msuya Mpango, Slowslow ni CDM. Haaah huu Ubaguzi wa madhehebu kiboko. Lakini CDM ni chama dume wajemeni kinawatoaga mipovu wapinzani wake Hadi Raha. Chama chenyewe hakuna ruksa ya kufanya siasa hadharani for 4 years now. Hivi kingekuwa kinafanya siasa za majukwaani ingekuwaje.Taratibu mkuu. Heb jaribu kuishi kwenye nchi nyingine za kiafrica.
Jaribu kuishi SA, Uganda, Kenya, Ethiopia, Congo, Rwanda, Msumbiji, Nigeria, Senegal , Cameroon au hata Libya na ukipenda angalia nchi nyingine kama china, Rusia, Iran, Saud Arabia, Mexico na nchi kibao za ulaya then ndo uje hapa kuandika unayoandika.
Ni wazi kuwa wanachofanya hawa maaskofu ni uharibifu wa nchi na ni utovu mkubwa wa nidham. Inaweza kuleta kiama kwa kanisa. Inaweza kuleta mvurugano ndan ya kanisa.
Usidhan KKKT lina wanachadema tu. Wapo pia wana CCM. CCM nayo ikiamua kuwatumia wanachama wake effective ndan ya Kanisa unadhan nn kitatokea. Kanisa litavurugika hilo..
Mtoa mada anaongea kwa akili pana na uelewa mpana wa mambo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Taratibu mkuu. Heb jaribu kuishi kwenye nchi nyingine za kiafrica.
Jaribu kuishi SA, Uganda, Kenya, Ethiopia, Congo, Rwanda, Msumbiji, Nigeria, Senegal , Cameroon au hata Libya na ukipenda angalia nchi nyingine kama china, Rusia, Iran, Saud Arabia, Mexico na nchi kibao za ulaya then ndo uje hapa kuandika unayoandika.
Ni wazi kuwa wanachofanya hawa maaskofu ni uharibifu wa nchi na ni utovu mkubwa wa nidham. Inaweza kuleta kiama kwa kanisa. Inaweza kuleta mvurugano ndan ya kanisa.
Usidhan KKKT lina wanachadema tu. Wapo pia wana CCM. CCM nayo ikiamua kuwatumia wanachama wake effective ndan ya Kanisa unadhan nn kitatokea. Kanisa litavurugika hilo..
Mtoa mada anaongea kwa akili pana na uelewa mpana wa mambo.
Sent using Jamii Forums mobile app
[/QUOT
Kanisa Kuomba tume huru ya uchaguzi kuna shida gani mpaka waumini wagombane??