Ujumbe muhimu: Mashabiki wenzangu wa Simba tulifeli hapa

Ujumbe muhimu: Mashabiki wenzangu wa Simba tulifeli hapa

Nijitese kwa stress kisa nini ?
04a6db32a1a8409983dcf7a0307af364.jpg
 
Tate Mkuu ukikaidi utapigwa2 Fene Stephen Ngalya Chelu sky soldier Shadeeya najua nyinyi watani basi msikose kupitia humu kutoa michango yenu
Mimi kwa upande wangu naona kinacho waponza simba ni kuwekeza zaidi kwenye maneno, kuliko vitendo.
Na wasipobadilika, aisee watasahau kuifunga Yanga na pia kuchukua ubingwa wowote ule kwenye hii miaka ya karibuni.

Yaani wanachonga mno! Kejeli nyingi! Na hii ni kuanzia kwa CEO wao Barbara, Msemaji wao Ahmed Ali, na mashabiki wao kwa ujumla. Wapunguze kuchonga! Na badala yake wacheze mpira. Kwa miaka ya karibuni, simba wamewekeza sana katika mpira wa maneno nje ya uwanja! Halafu wakiingia uwanjani, mambo yanakuwa tofauti kabisa.

Ona walivyo mvimbisha kichwa Enock Inonga kwa kumkamia kwake Mayele, na kilichomkuta jana!
 
Hata mimi nimeliona tumewekeza sana kwenye ngonjera huku watani zetu Yanga wakijipanga kiufundi na kivitendo zaidi.
 
Ningependa moja moja kuwapongeza watani zetu Yanga kwa ushindi wa jana.

Baada ya kufanya tathimini yangu fupi mitandaoni na vijiweni nimegundua kuna mabadiko makubwa kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kutokana na mambo wanayojadili kuhusu timu yao.

Nikianza na Yanga haswa hapa Jf kwenye jukwaa lao utakuta wanajidili kikosi chao na kutathimimi mapungufu na maboresho hata hapa Jf demigod pamoja na upopoma wake lakini alianzisha uzi wa kuiushauri klabu yake kuwa isiweke kambi nje ya nchi badala yake iwe hapa hapa kwani muda walioanza kambi ni sio rafiki hatimaye uongozi ukafanya hivyo japo sina uhakika kwamba mawazo walitoa kwenye uzi wake hapa jukwaani.

Tukirudi upande wetu misimu ya nyuma tulikuwa na mtindo wa kujadili wachezaji na mwendo wa timu kwa ujumla hata msimu ukiisha hapa Jf tutakutana na nyuzi kibao za napendekeza na maboresho nk lakini hali imeanza kubadilika tokea msimu uliopita kuanza mashabiki wa Simba tumekua tukitumia nguvu kubwa na kujadili na kushadadia mambo ambayo hayana msingi kwa klabu sisemi kama ni ubaya kujadili ili kunogesha mambo ila tumekithirisha mno mifano naweka hapo chini;

1. Habari za ng'ombe wa Mayele mpaka kungundua mbavu zake zina mpangilio upi.

2. Sopu and Sakho cup ilikuwa kama tumebeba Uefa vile.

3. Rank za CAF. Kama zinadumu milele au fifa ndio wametoa.

4. Sakata la Manara.

5. Jezi mpya za Yanga ikafikia hatua mpaka kugundua msikiti na Hamza .

6. Kuliponda Kombe alilobeba Yanga NBC Premier League kea kusema ni blender wengine eti kama mchoro wa virus.Wakati huo wachezaji wanabweteka kwa kuona Sawa maana nguvu imehamia kuponda Kombe kuliko kuwafanya wajute kukosa ubingwa.

7. Ongezeeni wadau.
#GuyuMoya#GuvuMoya

#UziTayari
upopoma wa mashabiki wa simba ni kutumia muda mwingi kufuatilia mambo ya Yanga! masahabiki wa yanga huo upopoma huwa hatunao na ukiona tumeufanya ni kwa reply tu... mfano mzungu wenu m'bovu lakini hakuna shabiki wa yanga aliyejaribu kumfuatilia na kupost ubovu wake hadi tumeona mauno yake jana uwanjani na kushika shika watu kama mchezaji wa mieleka.!
#nchi~imetulia
 
Aliyewapa ushindi Utopolo jana ni kocha.Baada ya kuwatoa Chama, Kanoute na Mkude timu ikapoteana na middlefield ikafa na kuwa expose centrebacks.Hakufanya homework yake vizuri.
 
Baada ya kujiuliza washambuliaji wetu wanakwama wapi nguvu tulihamishia kumkashifu Mayele
IMG_20220722_090202.jpg
 
Mashabiki wamepagawa kabisa
Screenshot_20220814_165853.jpg

.
Screenshot_20220814_165801.jpg
 
Back
Top Bottom