Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi kwa upande wangu naona kinacho waponza simba ni kuwekeza zaidi kwenye maneno, kuliko vitendo.Tate Mkuu ukikaidi utapigwa2 Fene Stephen Ngalya Chelu sky soldier Shadeeya najua nyinyi watani basi msikose kupitia humu kutoa michango yenu
Unafiki huu.Mimi mzalendo wa soka na ni shabiki huru sipo huwa nakanyagia popote bila unafiki.
Hata mimi nimeliona tumewekeza sana kwenye ngonjera huku watani zetu Yanga wakijipanga kiufundi na kivitendo zaidi.Mimi kwa upande wangu naona kinacho waponza simba ni kuwekeza zaidi kwenye maneno, kuliko vitendo.
Na wasipobadilika, aisee watasahau kuifunga Yanga na pia kuchukua ubingwa wowote ule kwenye hii miaka ya karibuni.
Yaani wanachonga mno! Kejeli nyingi! Na hii ni kuanzia kwa CEO wao Barbara, Msemaji wao Ahmed Ali, na mashabiki wao kwa ujumla. Wapunguze kuchonga! Na badala yake wacheze mpira. Kwa miaka ya karibuni, simba wamewekeza sana katika mpira wa maneno nje ya uwanja! Halafu wakiingia uwanjani, mambo yanakuwa tofauti kabisa.
Ona walivyo mvimbisha kichwa Enock Inonga kwa kumkamia kwake Mayele, na kilichomkuta jana!
upopoma wa mashabiki wa simba ni kutumia muda mwingi kufuatilia mambo ya Yanga! masahabiki wa yanga huo upopoma huwa hatunao na ukiona tumeufanya ni kwa reply tu... mfano mzungu wenu m'bovu lakini hakuna shabiki wa yanga aliyejaribu kumfuatilia na kupost ubovu wake hadi tumeona mauno yake jana uwanjani na kushika shika watu kama mchezaji wa mieleka.!Ningependa moja moja kuwapongeza watani zetu Yanga kwa ushindi wa jana.
Baada ya kufanya tathimini yangu fupi mitandaoni na vijiweni nimegundua kuna mabadiko makubwa kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kutokana na mambo wanayojadili kuhusu timu yao.
Nikianza na Yanga haswa hapa Jf kwenye jukwaa lao utakuta wanajidili kikosi chao na kutathimimi mapungufu na maboresho hata hapa Jf demigod pamoja na upopoma wake lakini alianzisha uzi wa kuiushauri klabu yake kuwa isiweke kambi nje ya nchi badala yake iwe hapa hapa kwani muda walioanza kambi ni sio rafiki hatimaye uongozi ukafanya hivyo japo sina uhakika kwamba mawazo walitoa kwenye uzi wake hapa jukwaani.
Tukirudi upande wetu misimu ya nyuma tulikuwa na mtindo wa kujadili wachezaji na mwendo wa timu kwa ujumla hata msimu ukiisha hapa Jf tutakutana na nyuzi kibao za napendekeza na maboresho nk lakini hali imeanza kubadilika tokea msimu uliopita kuanza mashabiki wa Simba tumekua tukitumia nguvu kubwa na kujadili na kushadadia mambo ambayo hayana msingi kwa klabu sisemi kama ni ubaya kujadili ili kunogesha mambo ila tumekithirisha mno mifano naweka hapo chini;
1. Habari za ng'ombe wa Mayele mpaka kungundua mbavu zake zina mpangilio upi.
2. Sopu and Sakho cup ilikuwa kama tumebeba Uefa vile.
3. Rank za CAF. Kama zinadumu milele au fifa ndio wametoa.
4. Sakata la Manara.
5. Jezi mpya za Yanga ikafikia hatua mpaka kugundua msikiti na Hamza .
6. Kuliponda Kombe alilobeba Yanga NBC Premier League kea kusema ni blender wengine eti kama mchoro wa virus.Wakati huo wachezaji wanabweteka kwa kuona Sawa maana nguvu imehamia kuponda Kombe kuliko kuwafanya wajute kukosa ubingwa.
7. Ongezeeni wadau.
#GuyuMoya#GuvuMoya
#UziTayari
Hawa walibeti ndio maana paniki wanazo za kutosha.Sisi hatuna uvumilivu kabisa yaani panic ya halView attachment 2323597i ya juu
Afadhali umelitambua hilo kakaJamani Simba wenzangu haraka tumuwahi njaakalihatari naona anaelekea kuchanganyikiwa sasa kila muda anaandika nyuzi za malalamiko halafu pumba tupuView attachment 2323594
Greatest Of All Time umesema ukweli kuwa kuna mashabiki mambumbumbu kabisa mfano hai huu hapa.